Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo akisimulia mkasa wa Maderva wa Tanzania walivyokwama kuendesha magari Qatar licha ya kuwa ni wahitimu wa Chuo cha NIT, alisema hayo Mei 7, 2025 alipokutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari, Dar es Salaam.
Video: Wapo Media
==================================
WAZIRI KOMBO AKUTANA NA WAHARIRI DAR, AELEZA MWELEKEO MPYA WA SERA YA MAMBO YA NJE
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na Wahariri wa vyombo vya Habari na kuelezea mwelekeo mpya wa Sera ya Mambo ya Nje Toleo la Mwaka 2024, ambayo ni muendelezo wa sera ya mwaka 2001 na kuongeza kuwa maboresho hayo, yamelenga kuiwezesha Tanzania kukabiliana na changamoto za wakati uliopo na wakati ujao katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, Balozi Kombo ameeleza kuwa maboresho hayo yamelenga kulinda maslahi ya taifa kwa msingi wa uhuru, haki za binadamu, demokrasia, ujirani mwema, na diplomasia ya uchumi na kuongeza kuwa maboresho hayo yamejikita kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa, kushirikisha diaspora, kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili kama bidhaa ya taifa, kuingiza masuala ya mazingira, jinsia, vijana, na uchumi wa buluu.
Amebainisha kuwa mafanikio ya utekelezaji wa sera ya mambo ya nje ambayo aliyataja kuwa ni pamoja na kuimarika kwa ujirani mwema na ushirikiano wa kimataifa na kuongeza kuwa kulikuwepo na changamoto kama uhalifu wa mipakani, ukosefu wa mwongozo kwa diaspora, na kutotumika vya kutosha kwa Kiswahili.
Amesema Sera ya Mambo ya Nje toleo la mwaka 2024 itazinduliwa rasmi tarehe 19 Mei 2025 na utekelezaji wake unahusisha wadau mbalimbali, ukiwemo mkakati mahsusi wa kushirikisha Watanzania waishio nje, kukuza utalii, kuongeza masoko ya bidhaa, na kuimarisha ushawishi wa Tanzania kimataifa.
Amesema utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 imeleta manufaa kwa nchi na kutaja manufaa hayo kuwa ni Pamoja na kuimarika kwa ujirani mwema, kuimarika kwa ushirikiano wa kikanda na kimataifa, kushika nafasi za uongozi katika taasisi za kimataifa, na Tanzania kuwa mwenyeji wa taasisi za kikanda na kimataifa.
Amesema maboresho hayo yamelenga kuongeza uzingatiaji wa mila na Katiba, kuweka mfumo wa uratibu wa mikataba, kushirikisha diaspora wa Tanzania, kutumia Kiswahili kama bidhaa, na kuingiza masuala ya uchumi wa buluu, mazingira, jinsia na vijana.