Waziri Kangi Lugola ameipindua Bendera ya Taifa

Baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani Mh Kangi Lugola amebuni vazi lake jipya ambalo amebandika Bendera ya Taifa kifuani upande wa kushoto, kulia na pia kwenye mikono na kama hiyo haitoshi anatembea na ilani ya CCM ambapo amenukuliwa akisema akifa azikwe na ilani ya chama hicho ya wakati huo kwakuwa kwake hakuna Ilani kama ya CCM na anapenda kutembea nayo katika utelelezaji wa shughuli za Kiserikali.

Lakini ukiangalia vizuri hilo vazi lake ni kuwa utagundua amegeuza mkao wa Bendera ya Taifa aliyoibandika upande wa kulia wa vazi lake ameipindua badala ya mistari ya njano na nyeusi kuelekea juu ikitokea kona ya chini upande wa kushoto kuelekea kona ya juu kulia yeye kaiweka ikitokea kona ya juu kushoto kuelekea kona ya chini kulia. Ile iliyopo upande wa kushoto ndio imekaa kwa usahihi hivyo hata hiyo ya kulia inapaswa aiweke kama hiyo ya kushoto.

Haitakiwi kuigeuza hiyo bendera kwa namna yoyote ile. Amwambie fundi wake airekebishe vinginevyo anazidi kujiabisha.

36836040_1940956792634972_6709772448692174848_n.jpg
Huyu jamaa natamani Masoud Kipanya amchore! Hilo tu ndo nasubiria!
 
Mzee kapa mzuka umempanda hivi, hamini kama yeye ndio tumempa dhamana ya ulinzi wa raia na mali zake ndani ya inchi, so msishangae kesho akamka kashona kanzu ya bendera ya taifa, au kumrisha wafungwa wavae sare za ccm.
 
Bavicha mjifunze kuwa uongozi ni hekima sio mavazi ya kiuanamitindo
 
Baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani Mh Kangi Lugola amebuni vazi lake jipya ambalo amebandika Bendera ya Taifa kifuani upande wa kushoto, kulia na pia kwenye mikono na kama hiyo haitoshi anatembea na ilani ya CCM ambapo amenukuliwa akisema akifa azikwe na ilani ya chama hicho ya wakati huo kwakuwa kwake hakuna Ilani kama ya CCM na anapenda kutembea nayo katika utelelezaji wa shughuli za Kiserikali.

Lakini ukiangalia vizuri hilo vazi lake ni kuwa utagundua amegeuza mkao wa Bendera ya Taifa aliyoibandika upande wa kulia wa vazi lake ameipindua badala ya mistari ya njano na nyeusi kuelekea juu ikitokea kona ya chini upande wa kushoto kuelekea kona ya juu kulia yeye kaiweka ikitokea kona ya juu kushoto kuelekea kona ya chini kulia. Ile iliyopo upande wa kushoto ndio imekaa kwa usahihi hivyo hata hiyo ya kulia inapaswa aiweke kama hiyo ya kushoto.

Haitakiwi kuigeuza hiyo bendera kwa namna yoyote ile. Amwambie fundi wake airekebishe vinginevyo anazidi kujiabisha.

36836040_1940956792634972_6709772448692174848_n.jpg

Achana na juha huyo.
 
Nashangaa cjui imekuwa kasumba ktk wizara hii hvi ni lazma wavae nguo zenye bendera? Wanatuaminisha kuwa ndo wazalendo ....hatari sana
 
ila inatosha jamani kajirekebisha. umeona suti aliyopokelea ofisi? wenye link watupie hapa tufunge mjadala
 
Back
Top Bottom