Waziri Jerry Slaa, Mtumishi wa Wizara yako akinunua ardhi ikawa na mgogoro, ni kigezo cha kumsimamisha kazi?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,003
20,680
Kidogo nimeshangazwa na habari inayotembea mtandaoni, mtumishi wa wizara ya ardhi anadai kununua ardhi, ardhi ikawa na mgongano na mtu mwingine, je hii ni sababu ya kumsimamisha kazi? Kwamba watumishi wa wizara wakinunua ardhi mitaani, ikawa na mgogoro hata wa mipaka, anasimamishwa kazi?

Kwa nini wasielekezwe mahakamani? Kusimamishwa kazi ni njia ya kumtisha aachie kiwanja? Maana upande wa pili kuna mbunge wa CCM.

Baadae akienda mahakamani kupiinga kusimamishwa kazi, mahakama iseme alipwe mamilioni, unampelekea deni Samia?

Kununua ardhi mitaani huko kama mtu wa kawaida anavyonunua, ikawa na mgogoro, ni kosa la kiutumishi?
 
Huwa nashindwa kuelewa kwann swala la Mipaka ya Ardhi linatatuliwa na Mwanasiasa. It's beyond me.

Hilo swala lina taratibu zake za kutatuliwa kwa mujibu wa sheria... Ila recently Kuna ka wimbi ka Siasa kudhani ndio final say.
Na shida kubwa inajipika ...wasiasa wanachofanya wanavuta shuka..wanasahau kuna mahali wanawafunua watu.
 
Yeah.....halafu anaiingiza serikali kwenye liability kwamba ndiyo ilitoa uamuzi,na mtu anashitaki akiijumuisha na kuidai fidia
 
TUNAWAJUA NINYI NI WEZI NA WAHUNI,,mshughulikiwe kisiasa,,
Hujui unalolisema.
Na Wala hakuna anayepinga wenye mwenendo mbovu kushughulikiwa na mamlaka za kinidhamu zilizopo kimfumo.

Ila kamwe personal choices haziwezi kuwa sababu ya yeye kumsimamisha Mtumishi kazi.

Mwisho wake utakuwa nini?! Na kwa nani? Na Daktari akihusishwa kwenye kiwanja chenye mgogoro naye asimamishwe?!

Vipi kuhusu mwalimu? Askari? Afisa nyuki? Haina mantiki hata kidogo. Sioni uhusiano wa kazi ma mgogoro wa kiwanja..na mbaya zaidi Afisa wa Simiyu mgogoro uko Mwanza halafu unamsimamisha kazi...kwa uhusiano upi?!
 
  • Thanks
Reactions: apk
Hiyo ni sawa na Lecturer kumpenda mwanafunzi wake!! Huwezi kufanya kazi wizara ya ardhi then ununue ardhi yenye mgogoro!! Hajua procedure za ununuzi wa ardhi??
 
Huwa nashindwa kuelewa kwann swala la Mipaka ya Ardhi linatatuliwa na Mwanasiasa. It's beyond me.

Hilo swala lina taratibu zake za kutatuliwa kwa mujibu wa sheria... Ila recently Kuna ka wimbi ka Siasa kudhani ndio final say.
Na shida kubwa inajipika ...wasiasa wanachofanya wanavuta shuka..wanasahau kuna mahali wanawafunua watu.

Mbona hamtatui sasa kama mnazijua hizo taratibu?
 
Hiyo ni sawa na Lecturer kumpenda mwanafunzi wake!! Huwezi kufanya kazi wizara ya ardhi then ununue ardhi yenye mgogoro!! Hajua procedure za ununuzi wa ardhi??
Shida nadhani hakuna anaelewa kinacholalamikiwa. Lecturer wa UD akiwa kwenye mapenzi na Mwanafunzi wa IFM unamfukuza kazi kwani anamfundisha?!
 
Mbona hamtatui sasa kama mnazijua hizo taratibu?
Shida huwezi kumsimamisha Mfanyakazi wa Simiyu kwa Mgogoro wa Mwanza. Akiwa Mwanza ni Mtanzania kama watanzania wengine. Ukifika Simiyu muwajibishe kama Mtumishi.

Tusitete haya. Yanaigharimu serikali. Nyuma ya pazia huwa wanarudi kazini, wanalipwa stahiki zao na wanasiasa hutawasikia wakija kuwakumbusha au kuomba msamaha kamwe.

Nadhani inabidi tuanze kuwaweka kati walipe wao gharama uone kama utasikia haya. Sisi ndio walipa Kodi tusipende watu wanaotuseti kufeli in the long-run huku wakijipatia umaarufu wa wakati huo ..kwa expense ya Kodi yetu.

Sanuka
 
Hata ukiwa mtumishi wa uma kusema umenunua ardhi ya kitapeli sikueliwi nakuona ni mjinga sana.
Migogoro ni mingi sana Mtaalamu..kikubwa tuombe Uzima.

Kuna syndicate ina watu nyeti wanapoka Ardhi kwa nguvu kupitia Migogoro. Inawezekana hii huifahamu.. Sasa nakupa Leo.

Walengwa na targets wa ishu kama hizi ni watu wenye kipato cha kati na chini wanaomiliki Ardhi katika maeneo prime. Najua ulikuwa haufahamu.

Sasa kaa kwa kutulia baada ya miaka mitano nenda kaangalie aliyeje ga kwenye viwanja kama hivi vya Mwanza vinavyogombewa.. utakuta ni Mh. Sana tuu au tajiri Mkubwa.

Na wanasiasa ndio mafuta na grisi ya syndicate hiyo.

Tunaposhangilia tujue huko tunakoisho kunakuwa prime na jidubwana nalo linakuwa kwa size na appetite... Tujitathmini.
 
Back
Top Bottom