Ni kawaida kwa wafanyakazi wa Serikali. Hujali zaidi mishahara yao, ndugu zake wakiathirika direct na ama kama kuna kiongozi wake muadilifu atajua (Kama atapata taarifa za uzembe). Kwa mantiki hiyo angalia:-
1. Ujenzi wa barabara na kituo cha mwendo kasi Jangwani! Sasa hakitumiki, sijui kinahamishwa lakini kwa gharama za walipa kodi maskini!.
2. Mipango miji kuwa na tabia ya kuwapimia watu maeneo baada ya kuwa wamejenga na kuwa na miji shagla baghala bila mpangilio wala mifumo sahihi ya miundo mbinu ya huduma.
3. serikali kutokujali uvamizi ama ujenzi katika maeneo yasiyoidhinishwa, baada ya ujenzi kukamilika, wanapeleka umeme, maji, soko, barabara na kodi za majengo wanachukua, halafu baadaye huyo mtu anaambiwa, bomoa umejemba eneo la wazi, ama bonde n.k.
4. Mengine naogopa kuyasema kwa kuwa na mimi ninafamiia inayonihitaji.