Meya wa Manispaa ya Morogoro waambie mgambo wako waache kukamata wamachinga kibabe watasababisha uvunjifu wa amani

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Kiukweli hapa Tz kwa sasa tunaishi kwa kunyanyaana na kuoneana sana

Vyombo vya Dola hasa polisi na mgambo wanawaonea sana wananchi wa kawaida

Tumeshuhudia Dar mgambo akimpiga mwananchi kisa tu masuala ya usafi,yani kutumia njia halali ya kutatua kero imeshindikana hadi nguvu itumike!!

Leo napita hapa Morogoro mjini karibu na stand ya daladala nakutana na watu kibao wanapiga kelele,kuangalia,nilichokiona kimenisikitisha sana

Kijana mfanyabiashara akapigwa na kuburutwa na mgambo zaidi ya 10,yani MTU mmoja anapigwa na mgambo zaidi ya 5

Kina mama wanalia na kusema siku hizi wanaishi kama wapo Burundi,kiukweli imeisikitisha sana

Sasa wewe Meya wa manispaa kama umewatuma hawa mgambo wako kupambana na wafanyabiashara wanaotafuta riziki wakalishe watoto wao,waambie watumie njia halali ,njia hii wanayoitumia ipo siku wananchi watachoka na kusababisha uvunjifu wa Amani

Na kingine watz hatuna umoja yani mgambo 5 wanatishia kundi la watu 100 wanashindwa kupambana nao,huu ni uonevu na unyanyasaji

Hali hii itakuja kuleta vurugu mbeleni zisipotumika njia za kistaarabu kudeal na hawa wafanyabiashara.
 
Acha wapate haki yao,ukipanda pilipili usitegemee kuvuna embe,wanavuna walichokipanda,nipo Morogoro mwaka was sita sasa,walizoea kwa akina mama kupewa kanga nyepesi na vilemba,na vijana kujaziwa mafuta Lita mojamoja,nashukulu Mbunge wao amejiweka pembeni na siasa,anawatazama tu.
 
Back
Top Bottom