Bomoa Bomoa ya TANROADS Morogoro Road Dar Es Salaam

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,533
Bomoa Bomoa ya makazi, nyumba, majengo na mali Morogoro Road Kuanzia Ubungo mpaka Kiluvia.

Leo mbunge wa Kibamba John Mnyika alikuwa na mkutano na wananchi wa jimbo lake kuhusiana na barua zilizosambazwa hivi siku 10 zilizopita kwa wakazi wa maeneo kutoka Kimara Mjini mpaka Kiluvia na TanRoads na alama za kutaka nyumba, majengo na mali kubomolewa kwa kuwa zinasemekana ziko kwenye hfadhi ya barabara ya Taifa.

Barua hizi zimetolewa na TanRoads MKoa wa Dar Es Salaam na mazungumzo ya watu yamechukua mkondo usio makini na kulifanya hili ni jambo la kisiasa.

Wengi wanaongea bila kujua undani wa jambi hili na zaidi ni ushabiki usio na mantiki.

1. Miaka ya 70,80,90 Serikali iligawa maeneo along Barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo a kuendelea hadi Kiluvia kutokana na wananchi waliopoteza makazi maeneo kadhaa ya jiji na hata kusaidia kupanuka kwa jiji.

2. Asilima kubwa 75% ya waliojenga nyumba, majengo ni halali na hata kwenye ramani za mipango miji za wizara ya ardhi, hizo nyumba na maeneo hayako kwenye Road Reserve.

3. Kwa mujibu wa wizara ya ardhi, eneo qualifying kuwa road reserve ni kati ya mita 30 hadi 60 kutoka katikati ya barabara. hii pia iko katika sheria zilizotumika na kuendelea kutumika kuhusu maeneo.

4. TanRoads (iliyoanzishwa 2000s) inadai kuwa road reserves ni mita 120 kutoka katikati ya barabara ambayo nikutokana nasheria ya barabara ya mwaka 1926/27.

5. Marekebisho kadhaa ya sheria ya barabara yameshafanyika tangu tupate uhuru na ndio maana Wizara ya ardhi, manispaa wanatumia sheria mpya na kuhusisha maeneo katika mipango miji.

6. Barabara ya Morogoro,eneo la Ubungo mpaka KImara mjini, TanRoads imetumia upana wa mita 30 na wakati wa kujenga mwendo kasi ikapanua mpaka mita 45 kutoka katikati ya barabara. Maeneo kutoka KIbaha kuelekea Chalinze, Tanroads inatumia sheria ya sasa ya mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande.

7. Bomoabomoa inayozungumziwa leo ni kutoka KImara Mjini/StopOver mpaka Kiluvia na TanRoads wanadai eneo la mita 120 kutoka katikati ya barabara (pande zote mita 120!)

8. Shauri hili lilishapelekwa mahakamani miaka iliyopita na TanRoads ilishindwa kesi. Hata wakati Waziri wa Ujenzi kati ya mwaka 2000 -2015 alipojaribu kung'ang'ania sheria ya mwaka 1927, si mahakama pekee, bali hata sheria za barabara na baraza la Mawaziri liliafiki kuwa ukubwa wa mwisho ni mita 60 kutoka katikati ya barabara kwa pande zote (jumla upana mzima mita 120). Hili linahitaji uchambuzi wa zaidi pamoja na kumbukumbu husika kuthibitisha hivyo.

9. Inasemekana kuwa miaka ya mwisho ya 90, kwenye mpango wa upanuzi wa barabara hii, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (WB/IMF) waliipa Serikali fedha za fidia kwa watakaolazimika kuhama maeneo yatakayo bomolewa kwa kufanya tathmini ya nyumba, majengo na mali zilizoko kwenye eneo litakaloathirika. Mpaka sasa hakuna mkazi ambaye imethibitika alipatiwa kiwanja kipya cha kuhama na kupewa fidia mali yake kubomolewa na hakuna kumbukumbiu kuonyesha malipo haya yalifanyika vipi.

10. Bomoabomoa ya sasa inafanywa na TanRoads mkoa wa Dar. Inasemekana ngazi zote zilizoulizwa(mawaziri Tamisemi, Ardhi, Ujenzi, TanRoads na hata Waziri Mkuu)kila mmoja inarusha mpira kwa mwenzake na vidole vinaelekezwa mamlaka ya juu ya Mkoa na Nchi.

11. Serikali kutokana na kauli inayosemekana ni ya Rais, inasema haitatoa fidia wala kutoa maeneo mapya kwa waathirika(inabidi kuthibitishwa kama ni kweli).

12. Barabara kuu ya kuingia Dar, imebadilishwa katika mipango ya barabara kuu na kuhamia upande wa Daraja la Kigamboni na highway kuu mpya imeshaanza kukwanguliwa miaka kadhaa iliyopita na itapita pembeni ya mji mpaka Ruvu au Chalinze kwenye maeneo ambayo yako wazi na hayana watu na gharama ni nafuu ukizingatia hakutakuwa na haja ya kubomoa au kutoa fidia kwa watu watakaoathirika kwa kiwango cha kutoka Ubungo pale Sam Nujoma na Morogoro road zinapokutana mpaka Ruvu.

13. Inasemekana mpango wa kupanua barabara hii kutoka Ubungo uko hati hati kutokanana kukosekana kwa fedha na kipaumbele kupelekwa maeneo mengine ya nchi yananayohitaji upanuzi wa barabara, fedha na kipaumbele kuwekwa barabara ya kutoka daraja la kigamboni, fly over za Tazara na Ubungo, Daraja jipya kutoka Aga Khan mpaka Coco Beach, Bandari ya Bagamoyo, Reli mpya na miradi mingine ya miundo mbinu nchini. Mradi unasemekana umesimama kwa kati ya miaka mitano hadi saba na hivyo kuweza kutoa fursa njema kwa mipango inayoeleweka kufanyika ikiwa na kuwapa wakazi watakaoathirika maeneo mapya ya kuhamia na fidia.

Kwa kutazamo hayo mambo 13 niliyataja hapo juu, ni wazi kuna ulazima wa jambo hili kufanywa kwa umakini, haki na kuthamini utu na si kufanyiwa upambe na ushabiki wa kisiasa.

Tafakari ni waathirika wangapi na kiasi gani kitatumika kutoa fidia au hata kufanya zoezi la ubomoaji.
 
Mkuu umechambua vizuri sana na zaidi umetoa Elimu nzuri kuhusu hili suala hasa la umbali wa mita kutoka barabarani hadi kwenye nyumba husika.

Nina jamaa zangu wanaishi Kimara Stop Over ni waathirika wa hili jambo. Ingawa kwa kufuata viwango vya umbali wa mita 60 walikuwa wasiguswe na hii bomoa bomoa. Ila sasa kwa mita 120 wanaguswa na hii bomoa bomoa.

Kwa karibu wiki mbili zilizopita wamekuwa wakifatilia kwenye Mamlaka mbali mbali na imekuwa ivyo ivyo kama unavyosema kila mtu anamtupia mpira mwenzake.

Lakini baadae imekuja kuonekana hili suala limeamriwa na Mkulu mwenyewe. Alivyotaka kubomoa kipindi kile alipokuwa Waziri awamu ya Mkapa alizuiwa na hata wakati wa JK akazuiwa tena kwenye kikao cha cabinet.

Hilo linaonekana lilimuuma sana ndio maana this time kasema lazima wabomolewe tena wale wote wanao kuwa kwenye 120m.

Kinachoshangaza na kinachoumiza zaidi hii barabara haipo kwenye mpango wa kupanuliwa hivi sasa. Haipo kwenye bajeti yoyote ile na wala hakuna funds za kutoka kwa donor yoyote yule ambae zimepatikana.

Nimesikia Waziri Mbarawa bungeni amesema upanuzi wa Kimara-Kibaha labda after 4 to 5yrs. Kwa ufupi hakuna fedha wala donor alijitokeza kuufadhili huu mradi.

Jana wananchi wa hili eneo ndio walikuwa wanakutana na Advocate (nimemsahau jina) ambae ndio wamempa hili shauri akalifungue mahakamani toka wiki iliyopita.

Sijui kwanini wananchi hawa wanatendewa hivi na serikali yao.
 
Ila tu niseme kwamba kuna roho za uharibifu zimetajwa mpaka kwenye misahafu, hili ni pepo baya sana.

...daima halitengenezi bali linaharibu na likitengeneza kitu hakitakosa kuwa na walakini mkubwa....

Hiyo ndio roho ya uharibifu ilivyo
Tunahitaji kuwa na barabara pana eneo husika Lakini hekima na utu vitawale watu walipwe fidia waondoke kwa amani ubabe hautatufikisha popote
 
Mkuu umechambua vizuri sana na zaidi umetoa Elimu nzuri kuhusu hili suala hasa la umbali wa mita kutoka barabarani hadi kwenye nyumba husika.

Nina jamaa zangu wanaishi Kimara Stop Over ni waathirika wa hili jambo. Ingawa kwa kufuata viwango vya umbali wa mita 60 walikuwa wasiguswe na hii bomoa bomoa. Ila sasa kwa mita 120 wanaguswa na hii bomoa bomoa.

Kwa karibu wiki mbili zilizopita wamekuwa wakifatilia kwenye Mamlaka mbali mbali na imekuwa ivyo ivyo kama unavyosema kila mtu anamtupia mpira mwenzake.

Lakini baadae imekuja kuonekana hili suala limeamriwa na Mkulu mwenyewe. Alivyotaka kubomoa kipindi kile alipokuwa Waziri awamu ya Mkapa alizuiwa na hata wakati wa JK akazuiwa tena kwenye kikao cha cabinet.

Hilo linaonekana lilimuuma sana ndio maana this time kasema lazima wabomolewe tena wale wote wanao kuwa kwenye 120m.

Kinachoshangaza na kinachoumiza zaidi hii barabara haipo kwenye mpango wa kupanuliwa hivi sasa. Haipo kwenye bajeti yoyote ile na wala hakuna funds za kutoka kwa donor yoyote yule ambae zimepatikana.

Nimesikia Waziri Mbarawa bungeni amesema upanuzi wa Kimara-Kibaha labda after 4 to 5yrs. Kwa ufupi hakuna fedha wala donor alijitokeza kuufadhili huu mradi.

Jana wananchi wa hili eneo ndio walikuwa wanakutana na Advocate (nimemsahau jina) ambae ndio wamempa hili shauri akalifungue mahakamani toka wiki iliyopita.

Sijui kwanini wananchi hawa wanatendewa hivi na serikali yao.

Ukitazama sana, nia nzuri na ya manufaa makubwa ya mbeleni inaingia madoa na kuzaa chuki kutokana na namna inavyotekelezwa.

Kuna watu wamekaa maeneo hayo miaka 40 sasa, leo unakuja wahamisha kibabe bila kuwapa sehemu mpya au kuwapa haki stahiki ya kufidia wahamie mahali kupya.

Basi wafanyiwe thamani ya mali zao na Serikali iwape nyumba za NHC zilizokamilika kama fidia ya kuhamishwa na kubomolewa nyumba!
 
Tuna miradi ilishafanyiwa upembuzi yakinifu makini kabisa... Tungetekeleza hiyo kwanza tukaachana na hii mipya iliyokosa umakini na kukurupuka kwingi
 
Tuna miradi ilishafanyiwa upembuzi yakinifu makini kabisa... Tungetekeleza hiyo kwanza tukaachana na hii mipya iliyokosa umakini na kukurupuka kwingi
Je zile ring roads Dar zimeshakamilika au hata kuanza kufanyiwa kazi kwa kuangalia mahitaji na uhandisi na mfumo wa kisasa?
 
Lakini nakumbuka wote waliojenga barabara ya Morogoro road walilipwa miaka mingi iliyopita fidia yao.

Hao wanaodai sasa wamejenga baada ya malipo kufanyika na ramani ipo mamlaka husika kwa ushahidi.

Uwezekano wa kulipwa fidia unaweza kuwa mdogo sana kwa wenye nyumba unless otherwise
 
Katika sakata hili ili kila upande upate haki yake nadhani tusije kujaribu kuingiza siasa.

Msuguano utakuwa mkali sana kuhusu uhalali kwa mamlaka kutekeleza agizo hilo
Mbona mnaiogopa siasa?
 
Back
Top Bottom