Waziri Jafo, hukuona mapema stendi ya daladala ya Manispaa ya Morogoro ilikojengwa, hukuwahoji wataalam wa mipango miji Manispaa?

Stand ingejengwa kikundi, jirani na soko,wangetengeneza Akira nyingi kwa wakazi was mji.
Kwa Hali ilivyo sitashanga kusikia amri abiria wakashukie mafiga.
Maana mjini hali mbaya kuhusu usafirishaji
Umewaza kitu ambacho watu wengi walikiwaza wakiwemo madereva wa bajaji

Wakati bajaji zinasumbuliwa kwa kukosa parking kila uliyeongea nae alipendekeza kikundi

Lakini cha ajabu huwa ni ngumu sana mwananchi wa kawaida kushauri jambo likakubalika maana wao wanajua nani ana masilahi wapi

Usishangae siku za usoni kuona maghorofa yanaporomoshwa pale kikundi

Kule mafiga wamechemka...ni pembeni sana halafu daladala nyingi hazina route ya kule na abiria hawana wanachofuata kule wala njia inayoelekea kule
 
Manispaa kuna kitu akiko sawa na mipango yao, ata soko tu vikazi vya wafanya biashara ni vichache kulinganisha na vikazi vilivyokuwepo zaman na mbaya zaid viongoz wamejilimbikizia vikazi wanawapangisha wafanya biashara elfu 60 au 70...

Matokeo yake kuna kundi kubwa bado wanauzia mitaani kusababisha watu wasifike sokon sasa na walio sokon awauzi nao wanakimbia kurud mitaani wauze inabaki ni mbio za mgambo na wao.
 
Wanachojali wao ni kuyajaza matumbo yao na ukiwashauri wanakwambia kuwa wewe ni mpinga maendeleo
 
Mafiga ni karibu na kwake na biashara zake coz mtaa unaofata kwa kaskazini (misufini) ndo nyumban kwa meya labda awe amehama hv karibuni na kwa upande wa magharibi mtaa unaofata ndo biashara zake za mbao na hardware zilipo(77)
Hawa makada wa ccm wanajali maslahi yao tuuu
 
Mkuu, nchi hii imezingwa na Mambo wawili
1. Chukua chako mapema, hii haijali Sheria kila anayeingia anachangamka

2 . Siasa, siasa ya nchi hii sijawahi ona au kuisikia popote pale duniani.

Siasa za nchi hii Zina meno, zinatafuta Sheria na taaluma.
Dr wa binaadam hana maana mbele ya katibu was ccm yoyote Ile.

Wataalam wakifanyakazi zao kitaalam, anakuja mwanasiasa hasa was chama tawala anatoa amri nyingine nje ya taaluma iliyoelekeza Nini kifanyike,
Hasa hasa awamu hii
Ccm hoyeeeeeee
 
Jafo maneno mengi lakini hamna kitu. Anaweza kuwa waziri wa kwanza kutumbuliwa awamu hii, na wizara yake ina mambo mengi sana. Simbachawene aliiweza ile wizara.
 
Hawa makada wa ccm wanajali maslahi yao tuuu
Kuna siku nilikutana na kada wa ccm anaitwa somebody Mnola, akaanza kujitapa kuwa nimechua vikazi vikazi soko kuu na viosk stand ya daladala.

Nilimuuliza kwa sifa zipi maana wewe siyo mfanyabiashara wa sokoni?
Majibu ni Kama ifuatavyo

Mimi ni kada wa ccm ndugu, nawezaje kuzikosa hizi fulsa?
Hakuna kada wa ccm atakayehitaji kitu ktk nchi hii akakikosa.

Upatikanaji wa meya morogoro kura zilipigwa siku nne, Kila zikihesabiwa wagombea wanafunga sawa.
Taarifa zinasema wagombea wote walikuwa was chama kimoja na wote walitoa rushwa kwa wajumbe walewale.

Taarifa zilizidi kusema
1. Alitoa2m, kwa wajumbe wote
2. 3m kwa wajumbe wote
3. 5m pia kwa wajumbe wote.
Hivyo kila mjumbe alikumbatia 10m mfuko wa nyuma(matakoni wanaita)

Kwa uingiaji huu madarakani tutegemee kupata huduma Bora na usimamizi mzuri was kazi za serikali?
 
Waziri wa Tanzania nzima mnampa lawama za Morogoro?

Na mikoa mingine wamlaumu nani??


Stendi za kila mkoa ni kazi ya waziri??
 
Mkuu inasikitisha sana na hawa wana CCM wanazidi kuitafuna Tanzania yetu
 
Waziri wa Tanzania nzima mnampa lawama za Morogoro?

Na mikoa mingine wamlaumu nani??


Stendi za kila mkoa ni kazi ya waziri??
Kila mkoa utatoa kero zake na wengine tutachangia kadiri iwezekanavyo.
Uwajibikaji wake ni wa nchi nzima hivyo hizi zinamuhusu
 
Back
Top Bottom