Brand Identity
Member
- Dec 11, 2018
- 7
- 5
*MHE LUKUVI: "Nataka Mtaalamu wa Mipango miji aweze pia kufanya upimaji wa Ardhi, na mtaalamu wa upimaji pia aweze kupanga Miji"*
Kutoka Morogoro:
Tarehe 14.01.2019
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi, ameyasema hayo Leo alipotembelea kwa kushtukiza Chuo Cha Ardhi Morogoro.
Amesema Chuo hicho kinatoa kozi za Mipango miji na kozi za upimaji (Survey) ambapo ameagiza kozi hizo ziunganishwe kuwa kozi moja. *"Lazima vijana wote wa hapa wafundishwe kozi zote za kupanga na kupima, mtu mmoja aweze kupanga na kupima"* alisema Lukuvi.
Waziri Lukuvi amesema kulingana na soko la ajira na ukuaji wa teknolojia, Mwanafunzi akiweza kupanga miji na kupima ataweza kujiajiri katika swala zima la urasimishaji, ameongeza kuwa Serikali imeamua kufanya urasimishaji ikiwa Ni pamoja na kuyatambua maeneo ambayo hayajapimwa kwa kutoa lesseni ya Makazi.
*"Nataka Kila mtu mwenye Nyumba, Kiwanja au Shamba mjini apewe lesseni ya Makazi itakayodumu kwa Miaka mitano, ndani ya muda huo awe ameshapata hati.."* aliongeza *"...Tumeshaongea na taasisi za fedha ili wazitambue rasmi lesseni za Makazi kuweza kutumika Kama dhamana kwa watakaotaka kuchukua mkopo..., Haya Ni Mapinduzi"*
Katika Ziara yake alimpongeza Mkuu wa Chuo Cha Ardhi *Dkt Adam Nyaruhuma* na kusema kwamba anamfahamu kwa umahiri wake tangu akiwa yupo Wizarani.
Alipata nafasi ya kukagua mazingira ya Chuo pamoja na kuongea na wanafunzi wa Chuoni hapo.
Hata hivyo swala la kuunganisha kozi linatakiwa kufanyiwa kazi haraka, Waziri amemuagiza Mkuu wa Chuo kukaa na Wataalamu waone namna gani watatoa Cheti kimoja kitakachomwezesha muhitimu kuwa mpimaji (surveyor) na kuwa mtaalamu wa Mipango miji.
#Arimo
#BrandIdentity
Sent using Jamii Forums mobile app