Kesho kutakuwa na mgomo wa madereva wa daladala Manispaa ya Morogoro, jiandaeni

Spanishboy

Senior Member
Apr 24, 2011
118
65
Habari zilizotufikia punde zinaeleza kuwa kesho kutakuwa na mgomo wa madereva wa daladala kwenye Manispaa ya Morogoro. Mgomo huo utazihusisha daladala za maeneo yote ya manispaa ya Morogoro jambo ambalo litapelekea kuwepo kwa shida kubwa ya usafiri mjini hapa.

Sababu za kufanya mgomo huo ni kupinga vitendo vya kukamatwa na kutozwa faini kubwa vinavyofanya mara kwa mara na askari wa usalama barabarani.

Kamanda anasema mgomo hauwezi kupindua sheria na kwamba hauwatishi askari kuendelea kusimamia sheria hizo ambazo mara nyingi zimekuwa zikikiukwa na madereva wa daladala mkoani humo na kuanza kulalamika pale wanapokamatwa na kupigwa faini.

Soma zaidi hapa safarimoja: Breaking News: Kesho kutakuwa na mgomo wa madereva wa daladala Manispaa ya Morogoro, jiandaeni

 
Back
Top Bottom