WAZIRI wa Nchi, Osi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amewaweka kikaangoni watumishi watano.

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1.jpg


WAZIRI wa Nchi, Osi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amewaweka kikaangoni watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kwa kutosimamia vyema kituo cha afya.

Waliowekwa kikaangoni ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji (DED), wa wilaya hiyo kwa kuwataka waandike barua za kujieleza, kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na kushindwa kwao kusimamia ujenzi wa Kituo cha Afya Mikumi licha ya fedha Sh milioni 400 kutolewa na Serikali Kuu tangu Juni, 2018. Waliowekwa ‘kiti moto’ kutakiwa kuandika barua za kujieleza mbali na DED, Asajile Mwambambale, ni Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO), Mhasibu wa Wilaya, Osa Mipango Miji na Fundi Mchundo wa halmashauri.

Wametakiwa kuziwasilisha osini kwa Katibu Mkuu wa Tamisemi ndani ya kipindi cha saa 24 kuanzia Januari 2, mwaka huu. Aidha, amewapa mwezi mmoja hadi Januari 30, mwaka huu, viongozi wa Wilaya ya Kilosa kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mikumi baada ya kususuasua tangu Juni mwaka jana kutokana na usimamizi mbovu.

Jafo alitoa maagizo hayo katika ziara yake wilayani Kilosa katika Mji Mdogo wa Mikumi na Kidodi ambayo aliifanya juzi ikilenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya, ambavyo wakazi wa maeneo hayo waliahidiwa na Rais John Magufuli, alipofanya ziara mwaka jana mkoani humo.

Alisema vituo hivyo kila kimoja kilipatiwa Sh milioni 400 kwa ajili ya ujenzi, na vilitakiwa kukamilika tangu Novemba mwaka jana, hata hivyo kwa Kituo cha Afya Mikumi ujenzi wake uko hatua ya msingi, wakati cha Kidodi kikiwa kimekamilishwa na kubakia umaliziaji wa maeneo madogo madogo.

Kutokana na hali aliyoikuta, Jafo alichukizwa na namna ya viongozi wa Wilaya ya Kilosa wasivyowajibika kusimamia ujenzi wa Kituo cha Afya Mikumi ambacho kilipatiwa fedha siku moja na vingine nchini Juni 26, 2018, lakini hadi sasa ujenzi wake upo ngazi ya msingi na hakuna usimamizi madhubuti. “Hebu naombeni wote mnipe maelezo ya kwa nini hali hii iko hivi, na kwa nini msichukuliwe hatua za kinidhamu, kuanzia Mkurugenzi, Mhasibu, Mganga wa Wilaya, Osa Mipango Miji na Fundi Mchundo anayesimamia ujenzi huu?” Alihoji.

Alisema katika ziara aliyofanya katika mikoa nane kwenye halmashauri ambazo baadhi zipo mbali na miundombinu yake ya barabara si mizuri, wamekamilisha ujenzi wa vituo vya afya na nyingine zimekia hatua ya linta, tofauti na Kilosa katika Kituo cha Afya Mikumi, ujenzi upo hatua ya msingi, jambo alilosema ni uzembe na halikubaki katika serikali ya awamu ya tano na hasa kwenye wizara anayoiongoza.

Kwa hiyo, baada ya maelekezo hayo, alisema atafanya tena ziara Januari 30, mwaka huu ili kuona utekelezaji na ukamilishaji wa ujenzi wa kituo hicho ambacho Rais alitoa fedha kusaidia wananchi kupata huduma bora za afya. Naye Mhasibu wa Wilaya Kilosa, George Mashauri katika utetezi wake kwa waziri, alidai ujenzi ulichelewa kuanza kutokana na mifumo ya fedha ya halmashauri kuchelewa kufunguka, na hata ilipofunguka watumishi wa Idara ya Fedha walikosea kutuma fedha hiyo kwenye akaunti ya Zahanati ya Mikumi; maelezo ambayo Jafo aliyakataa.

Kwa upande wake, DMO Dk Halima Mangiri alidai ujenzi huo ulianza tangu Juni kwa kazi zile zilizokuwa hazihitaji rasilimali fedha, hata hivyo walipoka Julai mifumo ilikuwa imefungwa na Septemba Idara ya Uhasibu ilipotaka kulipa fedha hizo, walikosea kuzituma, na hivyo kukaa miezi miwili bila kuanza ujenzi huo. Ulianza Oktoba 2018.
 
Back
Top Bottom