Waziri Jafo, hukuona mapema stendi ya daladala ya Manispaa ya Morogoro ilikojengwa, hukuwahoji wataalam wa mipango miji Manispaa?

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
1,722
2,000
Saalam!

Katika Mambo ambayo Waziri Jafo anatakiwa kuwa makini ni juu ya mipango miji.

Nimeenda manispaa ya morogoro nimeona stand ya daladala imehamishiwa mafiga, nilipohoji, jibu ni kwamba kuondoa jam katikati ya mji.

Hawakuzingati Mambo mengi Sana, Sasa kumekuwa na jam mjini kuliko kawaida. Jafo hukuwahoji watendaji wako? Meya huyu hakustahili kabisa kurudi kwenye nafasi ya umeya kwani ndiyo waliojenga stand ya mafiga Jambo ambalo ni Kama hasara tu.

Daladala hazipaki huko zinazunguka tu mjini.

Jafo rudi Moro uone.
 

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,746
2,000
Ni kawaida kwa wafanyakazi wa Serikali. Hujali zaidi mishahara yao, ndugu zake wakiathirika direct na ama kama kuna kiongozi wake muadilifu atajua (Kama atapata taarifa za uzembe). Kwa mantiki hiyo angalia:-

1. Ujenzi wa barabara na kituo cha mwendo kasi Jangwani! Sasa hakitumiki, sijui kinahamishwa lakini kwa gharama za walipa kodi maskini!.

2. Mipango miji kuwa na tabia ya kuwapimia watu maeneo baada ya kuwa wamejenga na kuwa na miji shagla baghala bila mpangilio wala mifumo sahihi ya miundo mbinu ya huduma.

3. serikali kutokujali uvamizi ama ujenzi katika maeneo yasiyoidhinishwa, baada ya ujenzi kukamilika, wanapeleka umeme, maji, soko, barabara na kodi za majengo wanachukua, halafu baadaye huyo mtu anaambiwa, bomoa umejemba eneo la wazi, ama bonde n.k.

4. Mengine naogopa kuyasema kwa kuwa na mimi ninafamiia inayonihitaji.
 

Don Nzoko

JF-Expert Member
Jan 6, 2020
263
500
Mafiga ni karibu na kwake na biashara zake coz mtaa unaofata kwa kaskazini (misufini) ndo nyumban kwa meya labda awe amehama hv karibuni na kwa upande wa magharibi mtaa unaofata ndo biashara zake za mbao na hardware zilipo(77)
 

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
1,722
2,000
Nafuu kidogo,
Hiyo stend ingejengwa Manzese ,pale lilipokuwa soko.
Stand ingejengwa kikundi, jirani na soko,wangetengeneza Akira nyingi kwa wakazi was mji.
Kwa Hali ilivyo sitashanga kusikia amri abiria wakashukie mafiga.
Maana mjini hali mbaya kuhusu usafirishaji
 

All - Rounder

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,775
2,000
Kwa hiyo Waziri Jaffo Kateuliwa kuwa tu Waziri wa Kushughulika na mambo ya Mkoani Morogoro na kwamba Mikoa mingie Kero ameshazitatua?
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,044
2,000
Yaani jamaa sio mtendaji ni brazamen fulani mjanja mjanja, mi kimoyomoyo namwitaga "Bob Sule"!!!
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,356
2,000
Jenga na kubomoa ni tatizo ambalo tunalo kwa muda sasa;

Unakuta mradi unafanyika baada ya muda unakuta hauna tija tena;

Pia unakuta raia wanajenga maeneo ambayo hawapaswi kujenga, mamlaka zipo kimya na tena zinawapelekea huduma kama maji na umeme.

Halafu anakuja mtu anasema Bomoa.

Hayo ni makosa,

Wenye mamlaka wasikae maofisini tu watembee na kuangalia maeneo yao wafahamu yanayoendelea huko kuliko kukaa tu na mafaili halafu wanakurupuka kuja kufanya maamuzi.
 

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
1,722
2,000
Mkuu, nchi hii imezingwa na Mambo wawili
1. Chukua chako mapema, hii haijali Sheria kila anayeingia anachangamka

2 . Siasa, siasa ya nchi hii sijawahi ona au kuisikia popote pale duniani.

Siasa za nchi hii Zina meno, zinatafuta Sheria na taaluma.
Dr wa binaadam hana maana mbele ya katibu was ccm yoyote Ile.

Wataalam wakifanyakazi zao kitaalam, anakuja mwanasiasa hasa was chama tawala anatoa amri nyingine nje ya taaluma iliyoelekeza Nini kifanyike,
Hasa hasa awamu hii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom