Waziri Jafo, hukuona mapema stendi ya daladala ya Manispaa ya Morogoro ilikojengwa, hukuwahoji wataalam wa mipango miji Manispaa?

Usiwe mbishi, kubali kukosolewa. Kuwa na udhaifu wa uelewa wa jambo fulani, siyo dhambi. Nakuhakikishia hutaenda jehanamu kwa kukubali mapungufu yako na kisha ukatulizana na kuanza kuyafanyia kazi ya kuyaondoa. Katika mada iliyomezani, kubali kuelekezwa, siku si nyingi utakuwa shujaa.
Nitatetea Kila Jambo ninaloliona ni sahihi.
Suala la uelewa Kila mtu analo japo tunatofautiana viwango.
Hao unaowaona wanauelewa, wanapinga hoja au wanapinga kwakuwa Waziri amehusishwa?
Tuanzie hapo

Maana tumeona mfano Lukuvi amekuwa akitatua migogoro mingi ya ardhi nchi nzima, kwani huko watu wa ardhi mkoa, wilaya na mabaraza ya ardhi hayapo?

Kusema huko Kuna ded, DC madiwani hiyo ni akili timamu?
Tumeona hao wanaosema wapo,wamekosea, niambie nani wakumwendea baada ya ngazi hizo kuboronga?

Saidia palipo na ukweli mkuu,!!

Tumesoma mabandiko mengi humu, wakiambiwa mawaziri hata mkuu wa nchi kuwa njoo au nenda mkoa, wilaya au idara Fulani kuna uozo, je huko hakuna viongozi?
 
Kuna wakati huwa nashindwa kuelewa tofauti ya tabia za kijamii na elimu za kitaalam. Mambo kama haya nayaona sana kwenye local governments kana kwamba kwao kuitwa local governments maana yake ni local mindsets.

Kuna maamuzi mengi sana yanafanyika kwenye halmashauri zetu ambayo ukiyapima katika mizani ya kitaaluma yanagoma ila yanaendana na hulka za viongozi wa hizo halmashauri. Tabia za kujengaleza vi-miundo mbinu vya muda imekuwa ni best practice yenye madhara makubwa sana katika maendeleo ya taifa.

Angalia barabara nyingi zinatumia fedha nyingi kukaraabatiwa kila mwaka baada ya mvua na ni kila mwaka kiasi kwamba mvua zinaponyesha tu, shida zinakuwa pale pale. Hakuna long term plans za kuwa na miundombinu inayoona mbali.

Angalia road reserves zinazowekwa, utadhani wapangaji hawajui kwamba watu bado wanabeba ujauizito na maendeleo yapo yanayohitaji barabara pana zaidi muda mfupi ujao.

Hili linaincubate matumizi ya resources kwa ku compensate watu kila wakati fedha ambazo zingetumika kwa maslahi mapana ya maendeleo.
Na kwa kushindwa kuwalipa wahanga wa upanuzi wa barabaara kwa kutokuwa na road reserves za kutosha, kunaleta maumivu kwa watu na kuwafanya kuwe na mwanya mpana kati ya SErikali ya wao kitu ambacho si sawa katika ustawi wa taifa. Serikali tulivu inahitaji kufanya juhudi za makusudi za kujenga mitazamo ya kuaminiwa, kupendwa, kuheshimika na wananch wake kwa kuwapenda na kuwatendea vyema.
Inawezekana kwa sasa Serikali ikawa inahtaji nguvu tu za wananchi lakini kuna siku itafika itahitaji mioyo na akili zao. Hivyo ni vyema kama hli wangeliona na kuhakikisha wanajenga ustawi katika mioyo na akili za wananchi.

Back to the point, mtindo wa kufanya kazi kwa tabia za kifamilia badala ya misingi ya kitaalamu, ndiko kunakosumbua na ambako mimi naona kunaweza kuwa kuna asisiwa na:-

1). Outdated qualifications za watu kuingia katika vyombo vya maamuzi kama madiwani na mabaraza yake.

2), Kukosa mfumo unaowalazimisha watumishi na viongozi kufanya kazi za viwango ambao unalazimisha hatua za kisheria zichukuliwe kwa kufanya vinginevyo. Hii ni kwa ngazi zote na idara zote za ofisi za uma. Ni mwanza Oyeee!, maadamu kuankucha na bora liende.

3). Kuwekeza nguvu zote za maamumuzi katiak siasa na wanasiasa na kutoa uzito pungufu katika utaalamu na watalaam.

4). Kushuka kwa elimu yetu na hivyo kuzalisha watu wasiokuwa na uwezo wala uelewa mpana .

5). Uwepo hafifu wa vyombo ya kupokea na kufanyia kazi mawazo mbadala yanayotoka kwenye vyombo mbadala wa mihimili rasmi.

What next? Who, how and when exactly? Tunahitaji kumshauri mehshimiwa Rais wetu aongeze jicho la tatu ili anapomaliza muda wake maruwe ruwe haya yawe historia.

Kuna mambo mengi ya kipuuz ambayo yalifanywa na watumishi wa umma kwa gharama ya walipakodi na yameharibika au wakaja kuvunja tena
Mifano iko mingi ila mm nakuja na mmja sehemu niliko walijenga kipande cha barabara kwa gravel wakati baada ya mwaka hakijaharibika wanakuja kuweka lami yaani pesa imepotea
 
Huyu jamaa sio mtendaji makini ni mtoa kauli za ukali tu ila suala la utendaji wenye tija ni zero kabisa mkuu.
Lkn mkuru si alisema alijifikiria Sana kumrudisha katika nafasi hiyo hivyo huko probation.Hapo ndo tutakupojua umuhimu wa mawazo kinzani.wengine wanadhani vyama mbadala ni ugpnvi siyo.nchi haiwezi kwenda mbele bila mnyukano kinzani ndani ya serikali.kwa Sasa tutashuhudia madudu mengi tu ndani ya serikali.Hiki ni kipindi kuzuri kea whistleblowers kuibua madudu mengi ndani ya serikali na watalaumiana wao kwa wao.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Jenga na kubomoa ni tatizo ambalo tunalo kwa muda sasa;

Unakuta mradi unafanyika baada ya muda unakuta hauna tija tena;

Pia unakuta raia wanajenga maeneo ambayo hawapaswi kujenga, mamlaka zipo kimya na tena zinawapelekea huduma kama maji na umeme.

Halafu anakuja mtu anasema Bomoa.

Hayo ni makosa,

Wenye mamlaka wasikae maofisini tu watembee na kuangalia maeneo yao wafahamu yanayoendelea huko kuliko kukaa tu na mafaili halafu wanakurupuka kuja kufanya maamuzi.
Mzee kigoma stendi ya daladala iko ujiji na hakuna abiria wa kupanda Wala kushukuka imebaki Kama pambo tu.wazee wa ujiji wakawavuta wakavutika bila kuchambua bongo zao ukiiona hiyo stendi huwezi amina.stendi nzuri lkn haina daladala Wala abiria watu wanajipandia bajaji haooo stendi imebaki sehemu ya utalii wa ujini.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Sheria gani, mbona mmeshindwa kuwaweka watu maeneo ya kufanyia biashara hususan sokoni.
Sasa ivi kila mji mboga zinauzwa Kila mtaa Tena barabarani .
Unazungumzia Sheria au siasa?
kinachofanya watu wauze mitaani ni ile sheria ya kuruhusu machinga, yani kama mnataka watu wakae masokoni sio mitaani mbona ni jambo dogo tu, inapigwa sheria marufuku kuuza mitaani. ila sasa ndio manispaa wanashindwa kutoa amri hiyo kwasababu ya ruhusa ya umachinga
 
Hebu tujaribu kuielezea root ya kihonda mjini, alafu uniambie Kuna mtu atashukia stand mafiga?
Maana watu wanasafari ya mjini, hata Kama gari ipitie Barbara ya iringa abiria wa katikati kabla ya mjini watashukia wapi?

Hao watakao shukia stand wachukue usafiri mwingine uwafikishe mjini.
Huoni ni kuwatesa gharama?

Hebu angali akili ndogo za watendaji,
Wameweka na sehemu za kuuzia biashara, kule watamuuzia nani?
mji hufuata usafiri, ndani ya miaka miwili tu, wafanyabiashara watagundua biashara zinatoka zaidi mafiga kuliko mjini kwa zamani ni suala la muda, halafu gari si zinafik masika, abiria wa mjini watashuka hapo
 
Huu mtindo wa kupeleka stand nje ya mji, ni upotevu wa pesa na rasilimali za taifa, maan ni hasara tyuuuh.
tatizo mji unakuwa haukui kama stendi zinabaki kati ya mji. trust me, ndani ya miaka miwili mafiga itakuwa mjini, wakazi wa kule wote watafungua fremu pengine na vijighorofa vitaanza kujengwa. pale kati ya mji ni mji wa wahindi ule miaka na miaka panabaki eneo lao walilosha jiwekeza
 
Nitatetea Kila Jambo ninaloliona ni sahihi.
Suala la uelewa Kila mtu analo japo tunatofautiana viwango.
Hao unaowaona wanauelewa, wanapinga hoja au wanapinga kwakuwa Waziri amehusishwa?
Tuanzie hapo

Maana tumeona mfano Lukuvi amekuwa akitatua migogoro mingi ya ardhi nchi nzima, kwani huko watu wa ardhi mkoa, wilaya na mabaraza ya ardhi hayapo?

Kusema huko Kuna ded, DC madiwani hiyo ni akili timamu?
Tumeona hao wanaosema wapo,wamekosea, niambie nani wakumwendea baada ya ngazi hizo kuboronga?

Saidia palipo na ukweli mkuu,!!

Tumesoma mabandiko mengi humu, wakiambiwa mawaziri hata mkuu wa nchi kuwa njoo au nenda mkoa, wilaya au idara Fulani kuna uozo, je huko hakuna viongozi?
Huelewi Muundo wa mambo ya ardhi unampa waziri mamlaka ya moja kwa moja hapo hakuna cha DED wala mkuu wa mkoa tofauti na Tamisemi
 
Mkuu, nchi hii imezingwa na Mambo wawili
1. Chukua chako mapema, hii haijali Sheria kila anayeingia anachangamka

2 . Siasa, siasa ya nchi hii sijawahi ona au kuisikia popote pale duniani.

Siasa za nchi hii Zina meno, zinatafuta Sheria na taaluma.
Dr wa binaadam hana maana mbele ya katibu was ccm yoyote Ile.

Wataalam wakifanyakazi zao kitaalam, anakuja mwanasiasa hasa was chama tawala anatoa amri nyingine nje ya taaluma iliyoelekeza Nini kifanyike,
Hasa hasa awamu hii
True si ajabu mwanasiasa anatoa ushauri kuhusu corona kuliko mtaalamu
 
tatizo mji unakuwa haukui kama stendi zinabaki kati ya mji. trust me, ndani ya miaka miwili mafiga itakuwa mjini, wakazi wa kule wote watafungua fremu pengine na vijighorofa vitaanza kujengwa. pale kati ya mji ni mji wa wahindi ule miaka na miaka panabaki eneo lao walilosha jiwekeza
Unaifahamu jiografia ya manispaa ya morogoro?
Hicho kiwanja cha stand kimetolewa na sua.
Maeneo yote toka stand mpaka mindu yanamilikiwa na sua
Hayo maghorofa yatajengwa wapi?

Mnapojenga muwe mnatafiti vitu vingi.
 
hiiii! si mitaa yote ya misufini, mafiga, uwanja wa taifa yote sasa imekuwa centre, wakazi wenye nyumba mitaa hiyo lazima watumie fursa kuendeleza nyumba zao kibiashara zaidi.
na kuhusu sua kushika maeneo hayo mengine, ni suala la muda tu kuanza kuachia maeneo hayo, maana hata wameshaachia sehemu kubwa tu ya ardhi yao, unavyoona shule za sua sekondari, pia eneo walilojenga kitngo chao cha kilimo biashara na hosteli zao yote yalikuwa mapori ya chuo ila wamegeuza matumizi kuwa ya makazi na shughuli nyengine hata hapo ndani ya miaka michache watabwaga manyanga wataachia eneo manispaa wapangie matumizi mengine
 
Hiyo mkuu ni kufikirika,
Mipango ipo ya muda mfupi na muda mrefu
Hebu fikiria Sasa stand kuiweka mafiga tusubiri sua iachie maeneo,ni mwaka gani?

Yaelekea unaishi morogoro.
Nikuombe nenda kaangalie kikundi au nyumba ya bar ya kambarage,pana eneo kubwa japo linatuwamisha maji,lakini serika isingeshindwa kulijaza kifusi na kulitengenezea miundombinu ya maji nakuyaelekeza mto kikundi.
 
mafiga ni pazuri zaidi, tena pako karibu na barabara kubwa
 
Back
Top Bottom