BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Akizungumza Bungeni leo, Selemani Saidi Jafo ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira amesema Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kazi nzuri ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele.
Amesema asilimia kubwa ya baa zilizofungiwa zimekiri kufanya makosa na kwenda kinyume na taratibu, ambapo tayari wahusika wamekubali kujirekebisha na zimeshaanza kufunguliwa.
Amesema “Wamekubali utaratibu wa Kiserikali, kwa Dodoma nimepata taarifa imebaki baa moja tu… taasisi yetu ya NEMC imefanya kazi kubwa.”