Sheria iboreshwe kudhibiti uchafuzi wa mazingira

Daz911

JF-Expert Member
Aug 1, 2018
730
1,208
U hali gani mwana JF.

Napenda kuliongelea suala la uchafuzi wa mazingira kama kero. Serikali ya Jamuhuri ilipendekeza siku ya Jumamosi kama siku ya kufanya usafi, aidha iliweka sheria nzuri ilipelekea viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki kufungwa. Kwa hili serikali ilijitahidi japo kumekuwa na uchakataji mpya wa mifuko plastiki ambayo yamebadilishwa tu rangi.

Napendekeza Elimu ya utunzaji wa mazingira iwekwe katika mitaala ya kufundishia mashuleni. Sawia na uzalendo hii itasadia jamii kuwa na mwamko mpya kwa miaka ya baadaye. Hakuna kazi ngumu kama kumfundisha mtu mzima, hasahasa katika mazingira ya kiafrika ambapo watu wengi wamezoea kuishi kimazoea. Watu wanajiendea bila mipangilio. Unamenya pipi unadondosha ganda chini, vocha unakwangua unajidondoshea tu chini, mwingine anakula mahindi gunzi analipiga danadana analiacha hapo, chupa za Nyagi, dompo, Hanson choic, zinatupwa ovyo mtaani, wenye baa huwa wanazikusanya kimtindo, mwisho siku anaenda kuzitupa porini usiku, Wamama wanazitupa nepi za watoto jalalani huku zikigombaniwa na mbwa, maji machafu yanamwagwa chini kuondoa vumbi.

Mzikii sauti kubwa na makanisa yenye mikesha karibu na makazi nayo ni uchafuzi mkubwa tu wa mazingira na ni kero,(waweke sound proo kila mtu ajipigie kelele mwenyewe). Kiufupi kila mtu anaishi anavyotaka, mwisho wa siku madhara yanakuwa makubwa.

Uhuru ambao hauna maaana umezidi Tanzania, ni jambo la kawaida sana kwa Mtanzania kutupa taka anapojisikia. Watanzania wengi wana desturi akinunua bidhaa, ataendelea kufurahia kula huku atadondosha kile kifungashio sehemu yeyote anayojisikia. Bila hatua kuchukuliwa tunakoenda ni hatari sana, taka zimezagaa mitaani, takeaway zinatupwa kila sehemu. Watu wamejisahau kiasi cha kwamba wote wanaishi maisha ya aina moja, sio vijijini sio mijini mitaani mingi ni michafu.

Kama nchi tuweke sheria kali kwa yeyote atakayetupa taka hovyo, Ikiwezekana kuwepo na mgambo kwenye majiji, kwa sehemu za vijijini maafisa watendaji wapewe mwongozo. Wachukuliwe hatua kali watendaji endapo hawatawajibika.

Yawekwe mapipa ya kuwekea taka sehemu kadha za miji na mitaa, ili kurahisisha watu kuweka taka sehemu moja. Na Kwa watakao kaidi wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwemo faini au kifungo, kutegemeana na sheria zitakazowekwa. Pipa viwanda viweke namna rafiki ya ku-recycle taka na bidhaa zao.

Na mwisho itolewa elimu kwa jamii, njia za kisasa za utunzaji wa mazingira. (mitaa mingi hauwezi hata kupiga picha hadi utafute location 😁)

Endapo hili likifanikiwa, watu watastaarabika kwa kiasi chake na umasikini utapungua kwa kiasi chake.

Mimi naannza leo, wewe je?
 
Sheria gani wakati sasa hivi umeanzishwa mtindo wa ukusanyaji taka wa kijinga! Taka zinawekwa kwenye viroba kisha viroba hivyo kurundikwa kando ya barabara kusubiri gari la taka lipite lichukue taka hizo. Linaweza lisipite siku tatu na kusababisha uvundo mitaani na kuwa kero
 
U hali gani mwana JF.

Napenda kuliongelea suala la uchafuzi wa mazingira kama kero. Serikali ya Jamuhuri ilipendekeza siku ya Jumamosi kama siku ya kufanya usafi, aidha iliweka sheria nzuri ilipelekea viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki kufungwa. Kwa hili serikali ilijitahidi japo kumekuwa na uchakataji mpya wa mifuko plastiki ambayo yamebadilishwa tu rangi.

Napendekeza Elimu ya utunzaji wa mazingira iwekwe katika mitaala ya kufundishia mashuleni. Sawia na uzalendo hii itasadia jamii kuwa na mwamko mpya kwa miaka ya baadaye. Hakuna kazi ngumu kama kumfundisha mtu mzima, hasahasa katika mazingira ya kiafrika ambapo watu wengi wamezoea kuishi kimazoea. Watu wanajiendea bila mipangilio. Unamenya pipi unadondosha ganda chini, vocha unakwangua unajidondoshea tu chini, mwingine anakula mahindi gunzi analipiga danadana analiacha hapo, chupa za Nyagi, dompo, Hanson choic, zinatupwa ovyo mtaani, wenye baa huwa wanazikusanya kimtindo, mwisho siku anaenda kuzitupa porini usiku, Wamama wanazitupa nepi za watoto jalalani huku zikigombaniwa na mbwa, maji machafu yanamwagwa chini kuondoa vumbi.

Mzikii sauti kubwa na makanisa yenye mikesha karibu na makazi nayo ni uchafuzi mkubwa tu wa mazingira na ni kero,(waweke sound proo kila mtu ajipigie kelele mwenyewe). Kiufupi kila mtu anaishi anavyotaka, mwisho wa siku madhara yanakuwa makubwa.

Uhuru ambao hauna maaana umezidi Tanzania, ni jambo la kawaida sana kwa Mtanzania kutupa taka anapojisikia. Watanzania wengi wana desturi akinunua bidhaa, ataendelea kufurahia kula huku atadondosha kile kifungashio sehemu yeyote anayojisikia. Bila hatua kuchukuliwa tunakoenda ni hatari sana, taka zimezagaa mitaani, takeaway zinatupwa kila sehemu. Watu wamejisahau kiasi cha kwamba wote wanaishi maisha ya aina moja, sio vijijini sio mijini mitaani mingi ni michafu.

Kama nchi tuweke sheria kali kwa yeyote atakayetupa taka hovyo, Ikiwezekana kuwepo na mgambo kwenye majiji, kwa sehemu za vijijini maafisa watendaji wapewe mwongozo. Wachukuliwe hatua kali watendaji endapo hawatawajibika.

Yawekwe mapipa ya kuwekea taka sehemu kadha za miji na mitaa, ili kurahisisha watu kuweka taka sehemu moja. Na Kwa watakao kaidi wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwemo faini au kifungo, kutegemeana na sheria zitakazowekwa. Pipa viwanda viweke namna rafiki ya ku-recycle taka na bidhaa zao.

Na mwisho itolewa elimu kwa jamii, njia za kisasa za utunzaji wa mazingira. (mitaa mingi hauwezi hata kupiga picha hadi utafute location 😁)

Endapo hili likifanikiwa, watu watastaarabika kwa kiasi chake na umasikini utapungua kwa kiasi chake.

Mimi naannza leo, wewe je?
Hebu siku moja jaribu kuweka pipa la taka nje ya nyumba unayoishi, utapata jibu.
 
naamanisha ninaweka pipa za kutosha, mwanzoni watu wakishazoea baadaye hata haitahitajika nguvu kubwa
 
Miaka ya zamani kila nyumba ilikuwa na pipa za lita 40 na vituo vys mabasi kulikuwa na vipipa vidogo kwa ajili ya tikiti. Watengeneza majiko na koroboi wakayaiba kama waibavyo alama za barabarani hivi sasa.
 
Back
Top Bottom