NEMC yatoa siku saba kwa kiwanda cha Chanzi limited Arusha kudhibiti uchafuzi wa mazingira wa harufu kali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa siku saba kwa Kampuni ya Chanzi Limited inayojishughulisha na uzalishaji wa funza kwa ajili ya kutengeneza Chakula cha mifugo, kuhakikisha wanazuia harufu kali inayotokana na shughuli zinazofanyika kiwandani hapo.
-1715924339.jpg

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria - NEMC Dkt. Thobias Mwesiga Richard alipozuru eneo la tukio na kubaini ukiukwaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kwa Kampuni hiyo kushindwa kudhibiti mazingira na kusababisha harufu mbaya inayoleta kero kwa wananchi na kuchafua Mazingira.
 
Back
Top Bottom