Waziri Jafo aonya wanaosafirisha vyuma chakavu bila vibali

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk Selemani Jafo ametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaosafirisha vyuma chakavu nje ya nchi bila kibali kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Dk Jafo amesema wafanyabiashara hao wanachangia kuongezeka kwa bei za vifaa vya ujenzi kama nondo na vyuma kutokana na malighafi hizo kuwa adimu.

Dk Jafo ametoa onyo hilo leo Septemba 22, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwepo wa usafirishaji haramu wa malighafi hizo.

“Ikumbukwe kuwa kupitia usafirishaji wa taka hatarishi nje ya nchi zipo tozo, kodi na ada zinazopaswa kulipwa hivyo usafirishaji wa taka hizo bila kibali husababisha Serikali kukosa mapato yanayopaswa kulipwa kupitia usafirishaji huo, hivyo kitendo cha utoroshaji kinaikosesha Serikali mapato,” amesema.

Aidha Dk Jafo amesema Wizara hiyo haijatoa vibali vya kusafirisha vyuma nje ya nchi kuanzia Machi hadi Septemba 2023, hivyo akalitaka Baraza la Taifa la Usimamaizi wa Mazingira (NEMC) na mamlaka za udhibiti zilizopo kwenye mipaka ya nchi kukagua shehena za mizigo.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom