Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Bashungwa ametoa agizo hilo Januari 29, 2024 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambalo hivi sasa limefikia asilimia 71 na kusisitiza ubora na viwango katika utekelezaji wake.
Aidha, amezipongeza Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi kwa ushirikiano wao walioutoa katika ujenzi huo kuanzia hatua za awali za usanifu hadi sasa ambapo Mkandarasi yupo katika hatua za mwisho za utekelezaji wa jengo hilo.
Bashungwa amemsisitiza Mkandarasi huyo kutekeleza hatua za mwisho za ujenzi vizuri (finishing) ili Ofisi hiyo kuwa ya mfano, sambamba na kuwa na mkakati wa kuwapa maarifa wataalamu wa Sekta ya Ujenzi ili kuwawezesha wataalamu hao kupata ujuzi na kuweza kutekeleza kazi hizo wenyewe.
Upande wake Mtendaji Mkuu wa Vikosi vya Ujenzi, Mhandisi Simeoni Machibya, amemhakikishia Waziri huyo kuwa ujenzi wa jengo hilo utazingatia viwango na ubora ili kufikia malengo ya Serikali.
Mhandisi Machibya ameeleza kuwa asilimia 68 ya vifaa vitakavyofungwa katika jengo hilo vimetoka nchini kupitia makampuni mbalimbali.