Waziri Bashungwa akabidhi magari matatu ya Zimamoto yaliyotengenezwa Tanzania, asema "Inawezekana majirani waje kununua magari Tanzania"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Nyumbu (1).jpg
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amekabidhi magari matatu ya Zimamoto (Mitambo) kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambayo yenye uwezo wa kubeba maji lita 5,000 na Foam Lita 500 kwa kila gari.

Waziri Bashungwa amekabidhi magari hayo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, Alhamisi ya Machi 30, 2023 baada ya kutengenezwa na Shirika la Nyumbu lililopo Kibaha Mkoani Pwani.

Ikielezwa kuwa shirika hilo lililopo chini ya Jeshi la Wananchi limekamilisha matengenezo ya magari hayo na yapo tayari kuanza kazi.

Nyumbu (5).jpg


Hafla hiyo ya Makabidhiano imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga, Meneja Mkuu wa Shirika hilo Brigedia Jenerali Hashim Komba, Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maafisa na Askari kutoka Jeshi la Wananchi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri Bashungwa amesema “Tutaendelea kushirikiana na Wizara nyingine kuhakikisha tunatimiza majukumu yetu, Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kushirikiana na vyombo vingine kuhakikisha tunaboresha sekta ya viwanda vya ulinzi.

"Pia mchakato huu umeweza kuokoa fedha nyingi ambapo kama mchakato ungefanyika kuagiza magari haya kutoka nje basi gharama yake ingekuwa kubwa zaidi ya iliyotumika.

Nyumbu (11).jpg
“Katika Awamu ya Sita kuna fursa ya uwekezaji katika sekta ya ulinzi, kazi iliyofanyika ni ya kiwango cha juu, ndio maana hata walivyokuja Scania ambao tunatumia nembo yao, walishangaa ubora ambao umetumika kutengeneza vichwa vya magari haya ya Zimamoto.

“Scania walisema kwa ubora huu hawaoni kwa nini Tanzania waendelee kuagiza magari ya Zimamoto wakati wana uwezo wa kutengeneza kwa viwango vya kimataifa na kupitiliza.

“Tunajua katika uvumbuzi wa masuala haya kuna fursa ya kufanya maboresho, inawezekana kuna changamoto zimetokea wakati wa mchakato, hivyo pale ambapo kuna fursa ya kufanya vizuri zaidi, kaeni mezani muangalie wapi kwenye mapungufu ili muone mnavyoweza kuboresha.

Nyumbu (4).jpg
“Mnaweza kutengeneza magari kwa ajili ya vyombo vyetu lakini pia si ndoto kwamba mnaweza kutengeneza hata kwa majirani zetu, sioni kama ni ndoto hilo kutokea kwa Nchi za jirani kuja Tanzania kununua magari hapa TATC Nyumbu.”

Nyumbu (3).jpg
Naye, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza katika hafla hiyo amesema:

“Wakati fulani ilipotokea kuna tukio la uzimaji moto, Jeshi la Zimamoto lilikuwa linakwenda kufedhehesha badala ya kusaidia, lakini kuimarisha nyenzo, ajira, uwezo, mafunzo na vifaa, kutawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi wa juu wakati wa majanga.

“Kinachofanyika ni mwendelezo wa jitihada za Awamu ya 6 katika kuwezesha maboresho ya vyombo vya ulinzi na usalama.

“Napongeza kazi kubwa ya TATC Nyumbu ambao wametoa miaka miwili kwa magari haya yanayokabidhiwa yatakuwa yanafanyiwa ‘service’, natoa wito wahusika msiruke matengenezo pale inapotakiwa.”

Upande wa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Masunga amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kuahidi kuyatunza magari hayo na kuendelea kuwahudumia wananchi katika huduma za Kuzima Moto na Uokoaji.
 
Tusitake kwenda na mambo makubwa bila sababu. Tuanzie kwanza na bajaji; bajaj na bodaboda tuache kutumia hela nyingi za kigeni kuagiza.

Zitengenezwe humu humu nchini. Hayo ndio mapinduzi na sio kujisifu na magari matatu ya zimamoto ambayo hayana impact kwa jamii pana.
 
Back
Top Bottom