Bashungwa aiagiza TANROADS kufanya tathmini ya maeneo yanayoathiriwa na mvua mara kwa mara

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewaelekeza Mameneja wa TANROADS nchi nzima kuhakikisha wanabainisha na kufanya upembuzi yakinifu kwa maeneo yote ambayo yamekuwa yakiathiriwa na mvua mara kwa mara ili Serikali iweze kuyatafutia suluhisho la kudumu kwa pamoja.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Bashungwa, Februari 15, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu Taarifa ya Mbunge wa Rorya, Mheshimiwa Jafari Chege iliyotaka kufahamu kuhusu mpango wa Serikali juu ya suluhisho la Barabara na madaraja yanayoharibika kipindi cha mvua na kusababisha kukatika kwa mawasiliano.

Aidha, Bashungwa amesema maeneo yote ambayo maji yanavuka barabara yatajengwa kwa kuhakikisha maji hayaathiri miundombinu kwa kipindi chote cha mvua zitakaponyesha.

“Tumeanza kuchukua hatua katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mtanana ambapo kila mwaka maji huwa yanavuka barabara, Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo, tumefanya tathmini ya kina na sasa hivi tuna mkandarasi anajenga kilometa Sita na makalvati makubwa, atainua barabara hii hata mvua za Elnino zikinyesha kila mwezi hakutakuwa na athari,” amesema Bashungwa.

Bashungwa ameongeza kuwa Wizara ya Ujenzi imefanya Tathmini ya athari za mvua za Elnino katika mikoa yote na kubainisha kuwa kiasi cha Shilingi Bilioni 200 kinahitajika kurudisha mawasiliano ya miundombinu ya barabara na madaraja iliyoharibika kutokana na mvua za Elnino.

Kadhalika, Bashungwa ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kuendelea kutoa fedha kupitia Mfuko wa dharura ambapo Wizara ya Ujenzi imeomba kiasi cha Shilingi Bilioni 66 kwa hatua za awali za kuendelea na utekelezaji wa zoezi hili.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi.
 

Attachments

  • IMG-20240215-WA0947(2).jpg
    IMG-20240215-WA0947(2).jpg
    346.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom