Waziri Bashe aipaka matope Tanzania Kimataifa

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Kauli ya Waziri Kilimo Hussein Bashe kuilazimisha na kuishinikiza Benki Kuu ya Tanzania kuacha kusimamia sheria zilizopo na kufanya upendeleo kwa Benki ya Ushirika katika mfumo wa utoaji wa mikopo.

1. Benki Kuu ya Tanzania imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Benki Kuu ambapo benki hiyo ili kutimiza majukumu yake kikamilifu imepewa kinga ya kutoingiliwa na chombo chochote (Autonomous Power), Benki Kuu haiingiliwi katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria, kiutawala na malengo iliyojiwekea.

2. Waziri wa Kilimo Hussein Bashe hana mamlaka na nguvu kisheria kuiagiza na kulazimisha Central Bank, agizo la Waziri huyu halina msingi wowote wa kisheria, kitendo cha Waziri kuishinikiza Benki Kuu ni uvunjaji wa sheria na amevuka mipaka yake ya uongozi, inasikitisha sana kwa kiongozi wa ngazi ya juu aliyeaminiwa na nchi kuvunja sheria na kushindwa kujua mipaka ya majukumu yake ya kazi.

3. Benki Kuu ya Tanzania imechukua hatua gani kutokana na kauli ya Waziri Bashe ambayo imedhalilisha na kubeza mamlaka ya BOT, kama kauli hizi zitaachwa kama zilivyo itajengeka dhana kwamba kumbe Benki Kuu ya Tanzania inafanya maamuzi kwa mashinikizo ya wanasiasa na sio kutokana na vigezo, utafiti na hali ya uchumi nchini hali ambayo itaichafua nchi yetu kitaifa na kimataifa.

4. Taasisi za Fedha za Kimataifa WB na IMF zinazohusika na kutoa kanuni na miongozo ya uendeshaji na usimamizi wa sekta ya fedha duniani zinaweza kuiadhibu Tanzania kwa kukiuka kanuni na miongozo ya usimamizi wa Benki Kuu.

5. Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikifanya mabadiliko mengi ya kisera na kimfumo bila shinikizo kutoka chombo au mtu yoyote kwa kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi na matokeo ya tafiti mbalimbali, BOT imejipatia umaarufu mkubwa kimataifa na kupewa tuzo mbalimbali kutoka taasisi zinazoaminika duniani. Iweje leo inaenda kulazimishwa na kushinikizwa kutoa upendeleo katika mfumo wa utoaji wa mkopo wa benki ya ushirika pekee?

6. Waziri Bashe anazikaripia benki na kuzishinikiza ziache kusimamia sheria na masharti ya utoaji wa mikopo yaliyowekwa na BOT na badala yake zitoe mikopo kiholela. Taasisi zetu za fedha zinafanya kazi nzuri sana ya utoaji wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi tulitegemea pongezi kwa mabenki kutoka kwa Waziri badala ya kutoa lawama na dhihaka.

7. Kauli za Waziri Bashe zimejaa utata na uvunjaji wa sheria za nchi, kaingilia mamlaka zingine ambazo ni nje ya mamlaka aliyopewa, kulazimisha na kushinikiza badala ya kushauri kwa vigezo na taarifa za utafiti ni mambo ya kusikitisha ambayo hayatarajiwi yafanywe na kiongozi mkubwa wa ngazi yake.

cc:
 
Nimesoma huu uzi kwa makini sana kama Mchumi nimeona wazi Bashe hana uwezo wa hiyo nafasi hiyona wabunge inabidi muwe makini sana kwa mipango anayoileta kwenu namuona ni mtu wa kujivuna tu kwa kiingereza na kuwadharau wenzake bungeni kwamba hawajasoma Form Six lakini ukiangalia kwa ujumla ni kweli Bashe anaipaka matope nchi yetu kimataifa tunaweza kufutiwa misaada kwa kuingilia utendaji kazi wa Benki Kuu ya Tanzania
 
Serikali yetu imeshindwa kupokea tenda ya brash(sisal product)tani laki tano per year kutoka kwa mchina leo unakuja kutupigia porojo hapa,
Mngechukua tenda alafu ninyi kama serikali mngekua mnakusanya kutoka kwa wazalishaji wadogo wadogo, wakati huohuo mnatengeneza mazingira ya kuwawezesha kwa kuwapatia pembejeo.

Mashamba makubwa sana ya mkonge yapo mfano Tanga na mengine mengi tu ambayo per year huwezi kosa tani laki tatu mpaka nne kama yakiwekewa usimamizi.ila sisi wapekuzi tunajua sababu kwanini viwanda vingi pia vya mkonge vinakufa ama kufungwa na kubaki magofu yasiyo na faida, hii ni kwasababu mwenyewe dhamana ya kusimamia na yeye anayo tenda binafsi ya kusaply sisal product(brash) huko kwa wachina je unadhan atakubali serikali ichukue ulaji wake?j8bu ni hapana.

Akili zakuambiwa changanya na zako, povu ruksaaaa.
 
Back
Top Bottom