Wazee wa Yanga wanamtetea Manji! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wa Yanga wanamtetea Manji!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dark City, Apr 30, 2009.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wazee wa Yanga waliongea na vyombo vya habari jana na kumshambulia Mengi kuwa aache kumkashifu mfadhili wao bwana Yusuph Manji. Walisema mambo mengi sana ila kubwa ni kuwa Mengi aachane na Manji kwa kile ambacho wanajaribu kuonesha kuwa Mengi anamwonea wivu. Kwamba amwache kabisa mfadhili wa Yanga. Je, wanaelewa kinachoendelea au wanajali vijisenti wanavyoimbiwa na baadaye kupewa kupitia mlango wa nyuma kwa kivuli cha ufadhili? Je wanauchukia ufisadi au kwao nchi kuibiwa si neno ili mradi wamepewa pilau na biriani?
   
 2. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Achana na hao wazee tuwapuuze tuu kwani kwa sasa wanakula faida tu. Hawajui what is happenin. Jana niliwaona nikasikia kichefuchefu!
   
 3. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nami pia niliwaona. Kwa kweli ni wa kuhurumiwa. Hawajui watendalo. Kama Mengi angekuwa ndio mfadhili wa Yanga, wangeandamana kumuunga mkono. Njaa mbaya jamani!
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hawa wazee wanaiaibisha Yanga klabu yenye historia ya ukombozi Tanzania.
  Kukosa pesa ni kitu kimoja lakini kukosa akili ni kite kingine kabisa, umaskini wao utaishia kuwapigia deki wahindi kwa ajili ya mlo wa jioni.
   
 5. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukiwanyima wananchi wako elimu , watakuwa watumwa wa kila kitu.Elimu ya darasa la saba haitoshi na ndio chimbuko la umasikini wetu na mawazo ya kipuuzi na kipumbavu kama ya hawa wazee.

  natamani mabomu ya mbagala yangetua vichwani mwa mafisadi.
   
 6. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa ni watumwa wa gredi ya chini wanaohongwa allowance, kahawa na kashata.

  Wapo wale watumwa wa gredi ya juu wanaohongwa magari, nyumba, trip za majuu, nk. Hawa wanamadigrii, maPhD na wanashikilia ofisi za juu serikalini. Wakistaafu wengi wao wataishia kuwa kama hawa hawa watumwa wa gredi ya chini.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wote hapo juu naona mmekaa Kisimba simba ngoja tuwasubili wana jangwani wenyewe tuone msimamo wao na wao wanasema kuhusu hili...
   
 8. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #8
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Waacheni jamani, angalau wakati tunasubiri hatima yao kupitia kwa YAN GA tunarejeshewa hela zetu kiaina kwa kuinua michezo. GT yupo? au bado amelala?
   
 9. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wazee wengine bana! Wao ndio wenye mali, wameibiwa mali yao, mwizi anarudi kuwaambia ok nitawasaidia kuifadhili timu yenu........doing that kwa mali ile ile aliyoiba! wangejua, kama asingewaibia mali yao, wazee wale maskini wa Mungu wangeweza kuwa na uhakika wa kutunzwa na serikali mpaka Mungu atakapo waita, watoto wao wangekuwa na uhakika wa kwenda shule, uhakika wa matibabu bora, uhakika wa ajira..........!

  Ama kweli ....Kosa mali pata akili!
   
 10. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Mimi ni mwana Yanga, lakini natanguliza utaifa mbele, hao wazee ni watumwa waacheni na utumwa wao, itachukua mda kuwaelimisha nini kinaendelea katika nchi hii, hivyo waacheni wafu wawazike wafu wao
   
 11. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Achana na hao wazee kwanza hawajui wanenalo plus elimu ndiyo hiyo ya kukimbia umande, unategemea comments gani? Umaskini ndiyo unaowaponza lakini wawe makini manji hana mchezo waulize waislam kajifanya rafiki kiwanja kimeenda sasa Yanga wasipokaa vizuri vitega uchumu vyao vitaondoka.... Hafadhari uwe maskini na heshimu kuliko kuwa na hela kwa kujidhalilisha...
   
 12. D

  Dina JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hii naona ndio suala la kubeba njaa kwenye mfuko wa nailoni (transparent)! Hawajui hata wanachotetea ni nini! Kumbukumbu kubwa iko tu pale wanapoitwa Quality plaza kwa mazungumzo na bahasha, baada ya hapo watatetea kila uozo regardless....ovyo....
   
 13. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  utumwa wa hela na njaa.....
   
 14. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo jamaa akiiba 100bn za walipa kodi akawapa 100mn Yanga ndo unaridhika? Mi nadhani huu ni utumwa wa kiakili.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu kama ungesikiliza chanel 10 hawa wazee wameongea maswala ya busara wanasema kama Mengi anaushahidi kuhusu Mfadhili wetu Manji kuwa ni fisadi papa basi afuate utaratibu wa kufikisha malalamiko yake yaani aende polisi au TAKUKURU au ampleke mahakamani wanadai Mengi yeye si hakimu wa kukaa na kumnyoshea mtu kidole wewe fisadi papa wewe fisadi dagaa.
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Si bora ya huyu anaye saidia kuna watu hapa hata msaada hawatoi hata chembe lakini ni makupe...huyu Manji binafsi naona kama Mengi.Mengi anasaidia kwa janja flani lakini naye alituulia NBC mkumbuke alihujumu...anajisafisha kwa njia yake pia.
   
 17. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu Fidel
  Mimi nadhani sehemu kubwa ya wachangiaji wanapofikia kujadili hoja fulani hawaangalii substance ya hoja zilizofikishwa kwao.

  Kama watasoma au kusikiliza kwa kwa makini hawa wazee wanaowaponda hapa ni kwamba waliamua kutoa taarifa yao hiyo baada ya kutafakari kuwa utaratibu na sheria hazikungatiwa na Mengi wakati anafanya press conference yake. Kwa maana ya kuwa hakutowa ushahidi na vielelezo juu ya tuhuma zake. Na kikubwa kabisa ambacho wazee wale wa Yanga (ambao wengine wanawaita hawakusoma) wameonesha busara yao hata ya kuonesha nini Mengi angefanya, yaani kufikisha ushahidi na vielelezo vyake katika vyombo husika. Sasa kwa wale ambao wanataka kuwa hukumu hawa wazee kwa kueleza misimamo yao kama klabu wanakosea kwani klabu ya Yanga ina mahusiano na Manji kama mfadhili wao.
  Nadhani ni vema tukaagalia uzito wa hoja ya wazee na sio kuwakashifu kwa maneno ya kejeli, hatujengi na hatuwatendei haki.
   
 18. J

  Jafar JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Much expected.
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu hawa wazee watu wangewasikiliza maoni yao wangeungana kabisa na matakwa ya hawa wazee wao wanadai Mengi hakufuata kanuni na taratibu za sheria kumshambulia Manji walisisitiza kama anaushahidi wa kumtia hatiani Manji apeleke mahala uhusika ili wamshughurikie. Alafu kumbukeni Mengi na hawa wazee ni tofauti kabisa
   
 20. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Siwezi kukubaliana na wewe hata siku mmoja kwa hoja yako hii, Wale wazee kama siyo njaa zao na elimu duni hawangeweza kwenda kwenye vyombo vya habari kumtetea Manji. Kuna maswali mengi hapa:-
  1. Nani kawatuma kwenda huko
  2.Kwa nini awatume
  3. Nani kalipia gharama za conference?
  4. Je wanachama wamekaa na kukubaliana pesa zao zikatumike kwenye conerence? au manji kalipia gharama?
  5. Kwa nini alipie?
  6. Kwa nini wanamtetee na asijitetee mwenyewe?

  Mengi alichofanya ni sahihii kabisa kikatiba, ana haki na wajibu wa kutoa mawazo yake , Hivyo mwenye kuona mawazo yake yanamwumiza naye ana wajibu wa kulalamika kwenye vyombo husika. Hivyo siyo Mengi ndiye aende kulalamika mahakamani hapani, Manji ndiye aende.

  Hapa tutapoteza muda wetu sana kujadili kitu ambacho jibu lake linajulikana Umasikini wa wazee wa yanga, na Ukosefu wa Elimu hata ya kufikiri tu. Ndiyo maana hao wazee hushinda mabarazani wakijadiri mambo ya ovyo abdala ya kutafuta pesa, Pita pale Yanga sasa hivi utakuta wamelala kwenye mikeka tangu subuhi hadi jioni!!!!! What next kama siyo omba omba!!!!!
   
Loading...