TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
22,344
39,995
Yusuf_Manji_Quality_Group.jpg

Yusuf Manji enzi za uhai wake
Mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mdhamini wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki dunia jana Jumamosi Juni 29, 2024 saa 6 usiku katika Jimbo la Florida nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wake, Mehbub Manji akizungumza na Mwananchi Digital muda mfupi uliopita.

Yusuf Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), kampuni inayojihusisha na sekta mbalimbali kama vile magari, ujenzi, vifaa vya kilimo, utalii, huduma za afya, na mali isiyohamishika.

Manji pia alifahamika kwa kujihusisha na shughuli za kijamii na misaada mbalimbali nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga.

Pia Manji alijihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Manispaa ya Temeke. Septemba 6, 2017 alipoteza sifa ya Udiwani kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Atakumbukwa kwa mafanikio makubwa na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.

Pia soma
- Yusuf Manji apoteza sifa ya kuwa Diwani wa Mbagala Kuu kwa kushindwa kuhudhuria vikao
 
Back
Top Bottom