Wazee wa Yanga wanamtetea Manji!

Nakubaliana na wewe 100%, huyo pundamilia ana mambo yake kwani tangu jana watu wamemweleza ukweli kuwa bila Mengi and IPPmedia ( Kulikoni & Thisday hat hii hoya hapa hatungekuwa nayo kwani haingekuwepo kabisa, maana swala la mafisadi tumelijua baada ya vyombo vya habari vya IPP kueleza huku vyombo vi ngingine vya mafisadi vilivyonunuliwa vikiwa vinasita kusema, So if you Pundamilia or ngamia you don't understand this, Automatically we will put you into the same group of beneficiaries of Mafisadi!! unless you clear your selfl here at JF.

Mpendanchi na DarkCity,

Hapa jamvini mimi siangalii sura ya mtu wala kusikiliza jina la mtu, ninachozingatia ni hoja yenye nguvu. Kwahiyo mnaponirejea kuwa mimi sielewi mnaniacha hoi kana kwamba kwamba hapa kuna muda maalum wa kujadili hoja na pia ni lazima nielewe hata kama nina mawazo tofauti na wachangiaji wengine. I have my own msimamo na nimeulezea na kutoa sababu ni kwani nini nina msimamo huo. Mimi wakati wote huu wa majadiliano nina heshimu hoja zote za wale ambao ni tofauti na mimi kwani ndiyo zinazonisaidia pia kunifanya nione tofauti hizo.
Inapotoka hoja, basi nitaiangalia kama nina hoja mbadala nitaijibu kama sina nitanyamaza, na hii ndiyo ninafanya wakati wote hapa jamvini.
Please msinichukie au kuniona mtu mbaya ati kwa sababu tu siungi mkono hoja zenu au mkaniona ninatetea mafisadi, la hasha, rejea postings zangu hapo juu nimeeleza msimamo wangu ni upi. Kutofautiana nanti haina maana nina mtetea mtu au watu, hiyo si kazi yangu na wala si kazi ya JF.
Na mara nyingi kama ninaona hakuna haja ya kujibu huwa ninakuwa msomaji tu, nina vigezo ambavyo ninavitumia kuangalia nijibu thread/posting ya mtu. Postings zingine zinakuwa chini ya kiwango kwa hiyo sihitaji kuzijibu nina kula kobis
 
- Ukisoma article ya Raia Mwema, utaikuta hii habari jinsi Makamba alipeleka hoja ya kutaka Mengi na viongozi wanaomfuasi wathibitiwe na CCM kwa kukigawa chama, ndio chanzo cha Mengi kujibu mapigo kwa kuwataja waliomtuma Makamba, kule CC.


I'll get a copy of this Newspaper then nitafanya ka-research nijue kwa undani.

- Depending na how much evidence you have against unaowatuhumu, ndio maana tuna vyama vya siasa ambako unaweza kwenda kupeleka usahidi wako na wakakusaidia kukupa platform ya kuongelea, this is politics vyombo vya dola haviwezi kunyamazisha sauti ya mwananchi yoyote wa kawaida kama ana ukweli, lakini lazima upitie kwenye ngazi zote zinazohusika, kwanza majukwaa ya siasa, then kwenye sheria otherwise inakuwa ni waste of our time yaani wananchi.


Hapa ndipo ambapo ninaona kuwa bado msimamo wangu una nguvu. Under normal circumstances kila jambo ni lazima lifuate sheria halali za nchi. Wote tunajua kuwa Mengi si mwanasiasa kama alivyo Slaa na wengine, yeye ni kama mimi na wewe. Sasa endapo mimi niingepnda aple maelezo halafu nikawataja kwa majina wa watu ni wahalifu, je unadhani ningeishia wapi? (Turejee kesi ya Mtikila na Magabacholi)

- Sasa ni zamu ya mafisadi kumpeleka Mengi kwenye sheria, ili atoe ushahidi wake ambao ninaamini kwa 100% kwamba anao, yaani this should not even be an ishu, lakini Mengi hawezi kuanza kwenda kwenye majukwa na kuanza kutoa ushahidi ili ufanye nini? Ushahidi hutolewa mahakamani, na ni seriakali ndio yenye dhamana ya kumfungulia mwananchi au kiongozi mashitaka, sio Mengi,


Kuhusu watuhumiwa wa Mengi kwenda mahakamani, litakaloongelewa mahakamani halitakuwa shauri la ufisadi zaidi kuwakashifu. Na endepo Mengi atasema kuwa mimi sikuwajashifu ninao ushahidi dhidi yao, unadhani mahakama itasema haya ulete tuanze kesi? it is obvious ataambiwa apeleke kwenye prosecution department jambo ambalo angeliweza kulifanya sasa kwa manufaa ya watanzania wote.

- Sasa kwa maoni yangu hawa wazee wa Yanga wangekua na hoja kama wangeishinikiza serikali, kupata ushahidi kutoka kwa Mengi na kumfungulia mashitaka Manji,

I think this is a powerful argument inabeba nguvu ya hoja zangu kwa maana kama tumemshinikiza Mengi atoe ushahidi na amekataa, basi tuibane serikali ifanye hivyo kwa niaba ya wananchi.

lakini sio kumlaani Mengi kwa kuwasema mafisadi hadharani na kudai ushahidi hivi hawa mazee wa Yanga kweli wanaweza hata kuuchambua ushahidi wa kisheria hawa?


Wazee wa Yanga ninavyowafahamu ni wazee wenye misimamo mikali kwani kaka wangekuwa ni legelege basi ile klabu isingekuwepo leo hii, nina wasifu kwa maana wana hekima na busara. Ninakumbuka kuwa hawa wazee walishaendesha kesi nyingi tu kwenye mahakama zetu, pale walipohitaji utaalam wa sheria walitumia wakili. Tusiwadharau tukatae hoja zao tu pale inapobidi.

This is a none ishu mkuu, hawa wazee wasubiri mechi ya Yanga na Simba, lakini haya ya siasa na sheria wawaaachie wanaohusika tu!

Thanxs!

FMES!

Nina mafua ngoja nikalale kidogo

Stay blessed
 
hiyo babu noma mi mwenyewe leo nimepata mafua na jana nilikula huyo mdudu sijui ndo yenyewe yaani presha inapanda na kushuka pua zimeziba.

Andika wosia baba vile vingine twaweza kurithi kutoka kwako marehemu mtarajiwa hahahahaha
 
Andika wosia baba vile vingine twaweza kurithi kutoka kwako marehemu mtarajiwa hahahahaha

Mkuu nimekuachia shemeji yako...lakini kule mahala usimguse ukimgusa tu yatakayo kukuta shauri yako...alafu lile banda la nyuma lile utamleta ile nyumba ndogo ya Sinza naye akaa pale.
 
Mkuu nimekuachia shemeji yako...lakini kule mahala usimguse ukimgusa tu yatakayo kukuta shauri yako...alafu lile banda la nyuma lile utamleta ile nyumba ndogo ya Sinza naye akaa pale.

Mazee na iwe hivyo!
 

1.
I think this is a powerful argument inabeba nguvu ya hoja zangu kwa maana kama tumemshinikiza Mengi atoe ushahidi na amekataa, basi tuibane serikali ifanye hivyo kwa niaba ya wananchi.


-
Ninaamini kwamba sheria ziko wazi kwamba hata serikali haiwezi kumlazimisha Mengi kutoa ushahidi kwa njia zisizokuwa za kisheria, wanachoweza kufanya ni kusubiri mafisadi wakimpeleka Mengi kwenye sheria kwanza na wao kufuatilia ushahidi na ku-take it from there, lakini sio burden ya Mengi kuwapa wananchi au serikali, ushahidi kwa sababu anajibu tuhuma za waliomtuma Makamba CC.

2.
Wazee wa Yanga ninavyowafahamu ni wazee wenye misimamo mikali kwani kaka wangekuwa ni legelege basi ile klabu isingekuwepo leo hii, nina wasifu kwa maana wana hekima na busara. Ninakumbuka kuwa hawa wazee walishaendesha kesi nyingi tu kwenye mahakama zetu, pale walipohitaji utaalam wa sheria walitumia wakili. Tusiwadharau tukatae hoja zao tu pale inapobidi.

- Hoja ingekua valid kama Yanga wangekua wamewahi kua mabingwa wa angalau Africa hata mara moja, hawa wazee wametumwia tu na Manji kujaribu kuficha ufisadi wake, cha muhimu hapa ni Manji kuwahi kwenye sheria haraka sana, ili akapewe ushahidi wa ufisadi wake.

Sasa again with all due respect, Mengi hana sababu yoyote kisheria kutoa ushahidi wake kwenye majukwaa ya siasa, ikibidi anatakwia kuutoa kwenye sheria tena wka kuhsinikizwa na madai ya Manji, hawa wazee hawana hoja kabisaa wanatumwia tu na Manji.

Respect.

FMES!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom