Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Dodoma mpauko
IMG_20220121_171826.jpg
 
Pole sana, hii ndio sababu sipendi kuendesha usiku. Kingine mtu akiwa anaendesha na mbele kuna lori au gari lolote anachochea tu ili alipite bila kujua kuwa unapoikaribia ile gari na mwendo wako mkubwa mbele inaweza kutokea gari ingine ushindwe kupita utaingia nyuma ya lori au porini.
Ni kweli kabisa watu wa malori ni watu wanajitoa sana kwenye majanga. Sisi wa magari madogo tunajiona tuna haraka zetu bila kujua kilomita chache mbele unaweza kuwa wewe unaehitaji msaada.
 
Nilikua natoka Dom - Arusha.
Kufika makuyumi huwa Kuna kizuizi usiku kwajili ya magari makubwa kukaguliwa, gari ndogo zina pita.

Baada ya kizuizi kuna mizani hivyo magari makubwa yakitoka kukaguliwa huingia mizani alafu yanaendelea mbele uelekeo wa Arusha.

Kumbe kuna gari kubwa moja walipita pale kwenye kizuizi kimagumashi Kwa kutoa ela ya kiwi kwasababu gari Lao bovu sanaa.

Ghafla nikalikuta halina taa hata moja, halina reflector na linatoa Moshi mwingi Sana wakati huo chombo imesha kubali gear na upande wapili kuna chombo ingine iko mafuta Sana.

Option niliyo Kua Nazo za haraka ni kuigonga Kwa nyuma Ile gari mbovu, kuigonga Uso Kwa uso Ile gari ilyo Kua inatoka Arusha au kulimwaga porini.

Mind you hapo barabara iko juu porini ni chini na kuna wanyama.

Basi nikalitupa huko porini likapinduka mara mbili lakini kabla nilisha hangaika na brakes gari ikawa ina sota Tu it was too late.

Alipo kuja mkuu wa kituo pale makuyumi aliwasema Sana wale police kwanini alishindwa kuifwata Ile gari kubwa kumbe washa Kula Chao.

Msaada mkubwa ulitoka Kwa maderava wa magari makubwa. Hawa WA gari ndo walikua wanapita shwaaaa shwaaaaaaa shwaaaaa

Ilikua hivyo.

Pole sana, hii ndio sababu sipendi kuendesha usiku. Kingine mtu akiwa anaendesha na mbele kuna lori au gari lolote anachochea tu ili alipite bila kujua kuwa unapoikaribia ile gari na mwendo wako mkubwa mbele inaweza kutokea gari ingine ushindwe kupita utaingia nyuma ya lori au porini.
Ni kweli kabisa watu wa malori ni watu wanajitoa sana kwenye majanga. Sisi wa magari madogo tunajiona tuna haraka zetu bila kujua kilomita chache mbele unaweza kuwa wewe unaehitaji msaada.
Ni nadra sana kupata msaada ukiwa highway kutoka kwa madereva wa magari madogo , Hawa jamaa wa magari makubwa(malori) huwa na msaada sana aisee....big up kwao.
 
Akiwa naye hatofika hiyo akijitahidi sana ataenda 100 au kama sio peke yake basi awe na wana hapo sawa huku nyuma wana wanapiga vitu vyao utasikia kamua kamua baba bado sijaonaaaaaa
Kuna siku nimepanda IT pale Mbezi inaenda Zambia ilikuwa X5, dreva yupo na jamaa yake dogodogo inaonekana huwa wanaenda Pamoja na kurudi Pamoja. Baada ya kutoka TRA misugu...jamaa alikuwa anaikamua gari mpaka Mimi mzoefu wa kusafiri night nkaanza kuwaza mwanangu ataishije nikipata ajali daaah. Ilikuwa dogo akimpa tu signal ya "clear" dreva anazitafuta 160+. Kona za Iyovi nadhani tulikuwa kwenye 140+. Tumetoka saa mbili usiku pale TRA, sita tupo Iringa hapo wanawahi saa kumi na moja wawe Tunduma Kuna jamaa anaisubiri gari aende nayo kanisani. Nilishuka Puma Iringa natetemeka miguu.
 
Back
Top Bottom