Road Trip yangu ya Kukumbukwa mwaka 2018

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
4,538
11,869
Naandika article hii baaada ya kupata inspiration kupitia uzi wa rrondo Wazee wa ‘road trip’ mpo?. Mimi ni subscriber wa uzi huu.

Ilikuwa december 2018 nikiwa na jamaa zangu watano wa idara fulani.Katika hao watano mmoja alikuwa dereva.

Gari tuliyotumia ni off-road toyota land cruiser 4.5 v8 dlx 2013. Mimi sio mtaalamu wa magari, watu wa magari mnajua speed yake na namna inavyoweza kuhimili mikimikiki ya safari ndefu.

Trip ilianzia dar mpaka musoma. We stayed at musoma for six days. Then we left for another roadtrip to Bukoba.

Tuliondoka Musoma saa 11 asubuhi. Around saa nne asubuhi tukafika kivuko cha Kigongo-Busisi Mwanza. Tukavuka na kuanza safari ya kuitafuta Geita Town.

Tulifika Geita na kupumzika kwa nusu saa. baada ya mapumziko tukaanza safari ya kuitafuta Chato.

Tulipita Buzirayombo, Itari then Chato. Tulisimama kidogo kwenye makazi ya marehemu Magufuli. Tukapiga story kidogo na jamaa zetu tuliowakuta pale nje kwenye Mgahawa wake. Sina hakika kama ule mgahawa bado unaendelea kutoa huduma au lah.

Wale jamaa zetu wakatukaribisha supu ya samaki Sato. Hatukulaza damu, supu ilikuwa tamu sana. Wale sato walikuwa ndio kwanza wametoka kuvuliwa ziwani, si unajua tena kanda ya ziwa.

Mwaka 2018 Magufuli alikuwa wa moto sana, he was in his prime time kiasi kwamba kama ulikuwa safarini na gari ukatize Chato jirani na makazi yake, unajikuta tu unakatiza kwa heshima na adabu(nimechomekea tu, hili sio jukwaa la siasa).

Basi tukaamsha zetu kuitafuta Nyamirembe, Katemwa, pori la Biharamuro, Nyakabongo, Kyamyorwa, Muleba na hatimaye around saa tatu usiku tukaingia zetu Bukoba town.

Tulikuwa hatuna haraka, mwendo wetu ulikuwa very reasonable kama watalii vile. Tulisimama mara kwa mara njiani kupiga picha na simu zetu.

Kwangu hii ni trip ya kukumbukwa sana, ilijaa matukio mengi ya furaha, utani, vicheko na story za hapa na pale.

Kipande cha kutoka Geita kuitafuta Chato tulichangamka sana, kwasababu tukiwa Geita tulinunua chupa mbili kubwa za Jameson. Mimi na wenzangu wanne ndio tulikuwa tunazinywa.

Dereva wetu ni kijana wa kipemba, ustaadh fulani mjanja mjanja. Yeye na mambo ya ulevi tofauti. Starehe yake kubwa ni watoto wa kike.

Naambatanisha kipande cha video nilicho record siku hiyo. Ila sikumbuki exactly ni aneo lipi. Nadhani ni Nyamirembe au Nyakabongo. Nawaachia assignment wakali wa location.

NB:
Mmoja kati ya jamaa yangu niliyekuwanae kwenye hii road trip ameshatangulia mbele ya haki miezi mitatu iliyopita. I dedicate this thread to him. May his soul continues to rest in peace. We are dust and to dust we shall return.
 

Attachments

  • InShot_20221028_131741025.mp4
    35.6 MB
Kuna kipande cha safari from Dar to Musoma
hahaha....upo sahihi. kwangu mimi roadtrip ya dar> dodoma> singida> shinyanga> mwanza> musoma haina maajabu sana kwasababu nimekuwa napiga route hiyo mara kwa mara.

bukoba huwa siendi mara kwa mara, kwenda bukoba na gari ni kama unafanya adventure. mbali sana. haina tofauti na ile ya kwenda kigoma kwa gari.
 
Hope's u did enjoy your trip na jamaa zako, nchi yetu ipo safi sana ni Eden ya Afrika
 
Hapo ulisema kuna mmoja ametangulia mbele za haki bs roho yangu imejikuta iko down to the Earth.
ndio hivyo ndg yangu. hatupaswi kuendelea kuhuzunika pale tunapoondokewa na wapendwa wetu. badala yake tuendelee kuishi huku tukienzi na ku celebrate kumbukukumbu nzuri walizotuachia.
 
Bila kuitaja katoro, buseresere, bwanga, runazi, gwanseri, visa vya bunda, kiabakari, nakadhalika sijakuelewa bado
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom