Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Road trip yangu ilikuwa Dar - Moro, wakati wa Moro - Dar nilirudi na bus.

Nilikuwa na sister, mzigo ulikuwa ni Athlete. I enjoyed the trip.... Crown tamu aisee ile comfortability yake si mchezo, yan sometimes inavutwa mpaka anavuka 140 lakini nafeel kama bado yuko kwa 80. Sis angu akiwa barabarani ni anadrive kama mwanaume, hanaga wasiwasi na traffic kabisa.

Another trip was Dar to Arusha na Kidia one. Ilikuwa Poa kiasi, Shekilango tulitoka 06:00 kufikia saa kumi na dk 29 tulikuwa around Tengeru. Napenda ile view ya Wami, Tanga ile milima, na wapi pale kunakuwaga na mashamba kibao ya katani, Mombo nk
..please weka pic ya sister hapa tumpe credits zake...
 
Duh leo nimetenda dhambi roho imeniuma sana. Nilikuwa na gari sijaizoe. Taa ya mafuta imewaka range inanionesha nina km20 tu. Nikaamua niweke mafuta ya kunifikisha home tu nikaweka 10,000 nilijua itaongeza range hadi km60 hivi. Baada ya kuweka mshale haukusogea wala range haikubadilika. Nikaenda ninapoenda range inashuka.
Kurudi nikapita njia ile ile range iko 14, nikapita pale kituo cha mafuta nikamwambia Yule dada nimeweka mafuta hapa kwako lakini gauge haikupanda wala kuonesha kuna mafuta yameingia, umeniibia! Dada Yule akasema sijakuibia nimekuwekea hela ulionipa nikamwambia haiwezekani kusiwe na mabadiliko kwenye gauge, ikabidi niende kituo kingine nikaweka 10, aisee gauge ikakurupuka ikapanda sana na range ikaja kwenye 110km. Hapo nikajua ni kweli aliweka mafuta nimemsingizia tu. Nimejisikia vibaya sana.
Sasa inabidi umrudie umwambie hata sahmahani, roho itatulia
 
Nipo Arusha..
nina simulizi tamu ya safari yangu jana..
kutoka nilipotoka hadi hapa kwenu
Kwetu wapi tena jamani?

Screenshot_20210113-231613.png

Weka hiyo simulizi...
 
Back
Top Bottom