Wazee wa Madrassa wampiku Mama Samia Suluhu?

Aiseeeeee ...kumtetea kote like!😅
kweli huwa mchungu. Hata wewe na mimi na mwengine yeyote yule, tutapotapoondoka kuelekea ahaera unafikiri tutakuwa na chochote tena duniani? Utakuwa huna chako wala lako.

Huo ndio ukweli wa maisha kwa sote. Ni nini cha ajabu hapo?
 
Nenda sasa ukachote habari na maarifa kutoka kwa Abdul. kwani huwa nakuona unatangaza sana habari za maendeleo.

Sasa una chanzo cha kuitumikia jamii, sio kila siku ungoje kuwatumikia wenye vibahasha tu. Tunataka tuone interview yako na wazee wa Madrasssa. Labda hiyo itakupaisha kwenye awamu hii, maana ulijitahidi sana awamu iliyopita ukaishia kuitwa ma njaa.

Unafikiri ile falsafa yako unayoipenda sana ya Karma ipo kwenye mabatya tu? Hata kwenye mema ipo, ukitenda mema utalipwa mema, ndio karma hiyo. Sasa nenda kafanye mema kuwatumikia hawa wazee wa madrassa uone karma yake.

Wasiliana Mzee Abdul 0625249605. Huyo Mzee ukikutana nae utafurahi tu, ni totally different character you have ever come across with.
I will.
P
 
Hakuna siri, ukweli ni kuwa Tanzania ilikuwa ya vitisho sana awamu iliyotutoka.

Ukienda huku Makonda, ukienda kule Sabaya ukirudi unatumbuliwa hata kama hauna jipu. Mara una kesi za uhujumu uchumi mara una kesi za kutakatisha fedha, ohoooooo.

Ikabidi wengine turudi zetu kwenye kwenye barafu tupoe kidogo.

Mama Samia katutoa hofu. In shaa Allah aishi kama jina lake "msikivu".
Tumpe ushirikiano Rais wetu ili nchi iwe na amani, nchi iwe na matumaini, kila mtu ajione ni binadamu sawa kama mwingine yeyote, japo tunatofautiana kimapato, jinsia zetu, makabila, dini, itikadi, n.k.

Lakini kubwa zaidi tujitafakari na kujiuliza, ilikuwaje mpaka tulifikia kwenye uongozi dhulumati kiasi kile cha awamu ya 5. Tuitumie awamu ya 5 kama shule, na tuone ni namna gani mifumo yetu ijengeke ili kuzuia tawala kama hiyo iliyopita kuweza kutokea tena.

Lakini pamoja na yote, Mungu hawatupi waja wake. Yawezekana wengi kwa maovu na unafiki wetu, Mungu aliamua kutuadhibu kwa kutupatia utawala dhalimu, lakini baadaye machozi, sala na maombi ya wenye haki wachache, viliweza kuifikia huruma ya Mungu. Sasa tuondokane na unafiki, tujenge mifumo imara inayolinda haki, demokrasia na maendeleo ya Taifa.
 
Group lao linaitwaje huko telegram?

1623127319395.png
 
Asante nitakaribia. Saba Saba inaanza, nitakuwa na vipindi vya TV kwanye vituo mbalimbali, nitawatafuta, niwarushe.
P
Ahsante tunashukuru sana kwa faida ya jamii.

Kwa huduma yako hiyo tuna uhakika Allah atakulipa mema yasio na hesabu kwani ameahidi katika Qur'an kuwa kila anaejitahidi kufanya kazi kwa njia za Allah basi atalipwa maradufu. Amiiiin.
 
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye group la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?

Mama Samia Suluhu juzi alipokuwa akiwaapisha Makatibu Tawala alisema "asilimia 46" ya aliowaapisha ni wanawake. Mama alinifurahisha sana sana kuona kuwa hatutupi wanawake wenzake.

Kilichonifurahisha zaidi ni habari iliyotumwa leo kwenye group la whatsapp na telegram kuwa wazee wa madrassatul Abraar ni muda sasa wameanzisha mpango wa kuwawezesha wanawake kabla ya Mama Samia Suluhu. Wanawawezesha kwa kuwwfundisha fani na taaluma mbali mbali za kazi kwa vitendo, hata mtaa wao unaitwa Vitendo.

Ya leo waliotuma ilikuwa ni kina mama waliojifunza ujenzi kuanzia hapo hapo Madrassatul Abraar, msimamizi wao (Mke wa Mzee wa Madrassa) yeye pia kajifunza usimamizi wa ujenzi hapo hapo Madrassa na mteja wa nyumba wanaoijenga ni mwanamke pia.

Mwenye nyumba hiyo pia nampongeza sana kwa kujitolea kuwakabidhi ajengewe nyumba yake kwa roho nyeupe kina mama hao ambao bado wanapata uzoefu wa ujenzi. Chini ntapandisha video clip.

Hongereni sana wazee wa Madrassatul Abraar, Hongera Bi Samira uliejitolea ujengewe bila hofu ili kina mama wenzio wapate uzoefu,

Jioneeni team ya kina mama ikiwa kazini...

Waandishi wa habari mko wapi mambo mema kama haya yanafanywa na wazee wa madrassa hamyatangazi? Hawa Madrassatul Abraar nimepitia hapa JF nimeona wamebuni mpango wa kuwezeshana wanaouita Nyumba kwa Wote ambao wanatamba kuwa haujawahi kutokea duniani, cha kushangaza si wanasiasa si waandishi wa habari wanaokwenda kuona mipango hii ambayo wangewawezesha hawa wazee ingefanywa kitaifa kabisa tena kwa ufanisi mkubwa kabisa.

View attachment 1808538
Miss you Faiza, karibu sana
 
Hakuna siri, ukweli ni kuwa Tanzania ilikuwa ya vitisho sana awamu iliyotutoka.

Ukienda huku Makonda, ukienda kule Sabaya ukirudi unatumbuliwa hata kama hauna jipu. Mara una kesi za uhujumu uchumi mara una kesi za kutakatisha fedha, ohoooooo.

Ikabidi wengine turudi zetu kwenye kwenye barafu tupoe kidogo.

Mama Samia katutoa hofu. In shaa Allah aishi kama jina lake "msikivu".
Awamu iliyotutoka tulikuwa wasomaji na watazamaji, kama mtu alikuwa anatamani malaika ashuke afute mitandao lazima ukae mbali na mitandao
 
Awamu iliyotutoka tulikuwa wasomaji na watazamaji, kama mtu alikuwa anatamani malaika ashuke afute mitandao lazima ukae mbali na mitandao
AlhamduliLllah na mie nimewaambia wanijengee kwa huo mpango wao wa kuanza ujenzi kwa 2,500. Lakini sasa hawatoki nje ya mkoa wa pwani. Nimewaambia waninunulie kiwanja huko huko kwao. Misugusugu.

Misugusugu napafahamu sana, ni kuzuri kuwekeza nyumba, huko kuna viwanda vingi vimejengwa na mara ya mwisho nilivyoenda vilikuwa vinachipua kama uyoga. Na mama kaja naona kama patakuwa Europe huko.
 
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye group la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?

Mama Samia Suluhu juzi alipokuwa akiwaapisha Makatibu Tawala alisema "asilimia 46" ya aliowaapisha ni wanawake. Mama alinifurahisha sana sana kuona kuwa hatutupi wanawake wenzake.

Kilichonifurahisha zaidi ni habari iliyotumwa leo kwenye group la whatsapp na telegram kuwa wazee wa madrassatul Abraar ni muda sasa wameanzisha mpango wa kuwawezesha wanawake kabla ya Mama Samia Suluhu. Wanawawezesha kwa kuwwfundisha fani na taaluma mbali mbali za kazi kwa vitendo, hata mtaa wao unaitwa Vitendo.

Ya leo waliotuma ilikuwa ni kina mama waliojifunza ujenzi kuanzia hapo hapo Madrassatul Abraar, msimamizi wao (Mke wa Mzee wa Madrassa) yeye pia kajifunza usimamizi wa ujenzi hapo hapo Madrassa na mteja wa nyumba wanaoijenga ni mwanamke pia.

Mwenye nyumba hiyo pia nampongeza sana kwa kujitolea kuwakabidhi ajengewe nyumba yake kwa roho nyeupe kina mama hao ambao bado wanapata uzoefu wa ujenzi. Chini ntapandisha video clip.

Hongereni sana wazee wa Madrassatul Abraar, Hongera Bi Samira uliejitolea ujengewe bila hofu ili kina mama wenzio wapate uzoefu,

Jioneeni team ya kina mama ikiwa kazini...

Waandishi wa habari mko wapi mambo mema kama haya yanafanywa na wazee wa madrassa hamyatangazi? Hawa Madrassatul Abraar nimepitia hapa JF nimeona wamebuni mpango wa kuwezeshana wanaouita Nyumba kwa Wote ambao wanatamba kuwa haujawahi kutokea duniani, cha kushangaza si wanasiasa si waandishi wa habari wanaokwenda kuona mipango hii ambayo wangewawezesha hawa wazee ingefanywa kitaifa kabisa tena kwa ufanisi mkubwa kabisa.

View attachment 1808538
Sasa hawa kina mama hawana familia za kuzisimamia wakatulia majumbani ?
 
In shaa Allah tuombe Mungu na mimi ntautuma ujumbe wako kwenye telegram group la Abraar Nyumba kwa Wote, kama hajasoma hapa atauona kwenye group. Au jiunge kwenye hilo group utapata majibu
Mama wa kiislam anayeipenda dini yake, welcome back
 
Back
Top Bottom