Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

wakuu mliopo mjini naombeni kujua kuhusiana na hawa wazee ni watu wa aina gani katika kupambqnua mambo
maana naamini sisi huku kwetu kijijini wazee wengi wapo katiki imani ya cuf na chadema kimawazo na wanapenda sana mabadiliko kwa ajili ya taifa la kesho ......
Naomba kufahimisha juu ya hawa wazee...

kundi la wazee wastaafu wa bandari almaarufu wazee wa bandari wana tabia za vijana wa hiphop ila wakitulia pale na kanzu zao hutadhania ni wao wajanjawajanja wanajua mambo mengi hawazeeki wananyumba zao wanaishi kwa kodi kazi yao draft bao na kujadili habari za simba yanga na siasa wakijadili jambo nnje ya hapo utacheka hadi ujikojolee. Walipolipwa hela ya east africa wakajulikana kama wazee wa east africa. Wajanja sana wakati wanadai hela yao ya east africa walilala barabarani wanajuana wote utawasikia huyu mzee mudi aliajiriwa kipindi cha meneja flani mwaka--------------si wajinga kwa siasa za ndani na wanaweza kukushabikia ukishawapa mpunga ukitoka wanakumwaga ila ukiwachanganya vizuri raisi kuamini na kukupigania-----utasikia tamko lao one clear and authoritative statement kama baba mwenye nyumba
 
Nani anasema Dar es salaam kuna wazee,mtu anakusanya wahuni mnasema ni wazee na wanabaki kazi yao ni kushangilia tu kama mazuzu,wazee wenye busara huwa wanahoji na sio wale wahuni ambao huwa wanaongea na mzee wa tezi dume.
 
Nani anasema Dar es salaam kuna wazee,mtu anakusanya wahuni mnasema ni wazee na wanabaki kazi yao ni kushangilia tu kama mazuzu,wazee wenye busara huwa wanahoji na sio wale wahuni ambao huwa wanaongea na mzee wa tezi dume.

Ha! Ha! Haaaa!!!
 
Ndugu yangu Mjengwa,

Kwanza natoa pongezi kwa kuibua mjadala huu.

Mimi binafsi nipo Dar kwa miaka 31 mfululizo lakini jambo ambalo huwa najiuliza ni hivi vigezo vya wazee hawa wa Dar wanavyopatikana na wakawa na tamko dhidi ya wakaazi wote waishio jijini.

Jambo lingine ambalo huwa linanipa shida ni wazee hawa sifa yao kubwa ni kuvaa nguo za kijani kibichi, pia huwa na Mwenyekiti ambaye hukaa meza kuu ingawa huwa hana sauti ya kutaka maswali miongoni mwa washiriki wa mkutano huo, lakini tena wakishahutubiwa hata kama hotuba ina kasoro wenyewe hupiga makofi.

Jambo lingine wakati huu wa maisha magumu utakuta wazee toka charambe wamehudhuria lakini kumbe wanachukuliwa kwenye matawi ya chama na magari na wanarudishwa huko, na jambo la mwisho sijui kama wazee hawa wa mkoa huwa wanajua matatizo yatakayozungumzwa au huwepo ili mradi mtoa hotuba isionekane hakuna anayemsikiliza.

Naungana nawe Mjengwa ili ajuaye vigezo atasaidia siyo wewe na mimi tu, bali ni watu wengi wanahitaji kujua hili.

Kwani kwa nn asilihutubie taifa kupitia vyombo vya habari!? au anataka kupigiwa makofi kwa kuwa anajua anaenda kuonfea pumba
 
Ni kwanini kikwete anaacha kuongea na hawa vijana zaidi ya 300 waliofuzu JKT nakuamua kuandamana kwenda ikulu wakiwa na bendera nyekundu?
Kwanini kikwete hawaoni hawa vijana wenye shauku naye?
 
kundi la wazee wastaafu wa bandari almaarufu wazee wa bandari wana tabia za vijana wa hiphop ila wakitulia pale na kanzu zao hutadhania ni wao wajanjawajanja wanajua mambo mengi hawazeeki wananyumba zao wanaishi kwa kodi kazi yao draft bao na kujadili habari za simba yanga na siasa wakijadili jambo nnje ya hapo utacheka hadi ujikojolee. Walipolipwa hela ya east africa wakajulikana kama wazee wa east africa. Wajanja sana wakati wanadai hela yao ya east africa walilala barabarani wanajuana wote utawasikia huyu mzee mudi aliajiriwa kipindi cha meneja flani mwaka--------------si wajinga kwa siasa za ndani na wanaweza kukushabikia ukishawapa mpunga ukitoka wanakumwaga ila ukiwachanganya vizuri raisi kuamini na kukupigania-----utasikia tamko lao one clear and authoritative statement kama baba mwenye nyumba

Nimecheka sana...hawa ndio wazee Ally Choki aliowaimba ''Wazee wa bandari''
 
Wazee Wapenda Masinia Ya Pilau, Kashata Na Kahawa Wapo Dar, Pia Wazee Mambumbumbu Wapo Dar, Na Ndiyo Maana Akicheka Wao Ni Makofi, Akijamba Ndo Usiseme Vigelegele Kwa Wingi. Halafu WOTE NI VIBARAGHASHIA Sijui Ni Wale Wacheza Bao Na Wanaokunywa Kahawa Nje Ya Majengo Ya Kuabudia Wakisengenya Watu? Hebu Mwenye Kujua Jinsi Wanavyopatikana.
 
Very very weak prof. Lack of courage, lack of confidence, lack of popularity and fear of challenge hivi ndo vinamfanya mkulu achague audience ya namna hii ya tired and retired old men ktk kipindi hiki cha technological revolution huwezi kuwaambia kitu wazee ambao hawakuweza hata kugundua sindano, mkulu anaogopa sana challenge, jiulize kwanin sio waandishi wa hbr? Kwanin sio vijana?,au basis aseme wakazi wa dar? Kwa nyrere may nyakati hizo it was fyn smhow, SAS kuna a lot to be discussed, karne hoi hatukatai wazee Bali wazee wenyewe wanashangaa dunia imekua kijiji for science and technological innovations, in fact wengi wao hawajui kinachoendelea wapo wapo tu ili mradi siku zinasonga mbele, our president plz soma alama za nyakati dunia inakushangaa kuna mambo mengi ya kufanya zaidi ya your world wide physical presentation.
 
Hawa ndio waliowakomboa nyie kutoka kwenye utwana,lazima tuwape heshima,nyerere mwenyewe anajua,na wanauwezo wao kuliko unavyofikiri
 
ni wazee wa bahasha ya kaki, wewe fuatilia baada ya mkutano wao, vibahasha lazima.
 
Sijajua masuala mazito yahusuyo hatima ya nchi yetu kupitia mchakato wa Katiba mpya kuzungumzwa kwa "wazee wa CCM wa Dar es Salaam!" Najua baadhi yenu mtasema kuwa Rais alikuwa anaongea kwa Taifa zima lakini implication iliyoonekana imekaa kichama zaidi kuliko kitaifa!

Hivi nchi hii imebaki ya hawa wazee wa DSM tena wa CCM au namna gani? Si ingekuwa ni vema Rais angeandaa kipindi ambacho watu wengi wangeshiriki tena kwa kuuliza maswali, kuliko kuhutubia hao wazee ambao wengi wao walikuwa wamelala usingizi na kushtuka baadhi yao wakiwa wanapiga makofi!

Hapo mwenyewe natatizwa sana kama kuzungumza sibora aandae kipind kama alivyo fanya awali na kuuliza maswali live kuliko wazee
 
Nchi iko kwenye vifungo vya nguvu za giza hii ndio maana haiendelei zaidi ya wananchi kuwa kondoo wapole kwa viongozi katili wasiowajali.
Huo ndio umuhimu wa wazee hao,"kamati ya ufundi" ya ikulu hiyo.

Nchi hii nembo yake tu ni zindiko,na ndio inatumika kila mahali hadi vyeo vya maafisa wa jeshi,unategemea nini?
 
Nani anasema Dar es salaam kuna wazee,mtu anakusanya wahuni mnasema ni wazee na wanabaki kazi yao ni kushangilia tu kama mazuzu,wazee wenye busara huwa wanahoji na sio wale wahuni ambao huwa wanaongea na mzee wa tezi dume.

Hahaha hahaha hahaha
 
Inasikitisha kuona matusi na kejeli zinazotolewa kuhusu "wazee wa Daresalaam"
Hii ni tradition iliyokuwepo toka kabla ya kupata uhuru.
Wazee hawa ndio waliomtoa mwalimu toka Pugu na kumleta mjini. Walifahamu kipaji na uwezo wake na wakamuamini kuongoza TANU, wakajitolea hali na mali kukiimarisha chama kugombea Uhuru. Wakamstaarabisha Nyerere kutoka kuvaa kaptula, avae suruali na kuwa muungwana....
Wamejitolea mashamba yao kunufaisha wabara na kama nyie mnaowatukana kuhamia Dar na kujiona vijeba!! Kumbukeni, kabla Dar haijavamiwa na waliokarimiwa, ambao nadhani wengi wenu ndio mnaotoa kejeli, lilikuwa ni mashamba ya wazee wa kizaramo.

Muungwana Nyerere aliona ni wajibu kuwaheshimu wazee hawa waliomuwezesha yeye binafsi na chama kuweza kugombea uhuru. Kila mara alikuwa akiwaita kuwapa ama progress report, kuchukua mawazo zaidi, au kuomba misaada yao kuwezesha vita za kugombea uhuru. Na bila choyo walijitolea kwa hali na mali.

Ni aibu nyie mnaowakebehi, kama sio wao, basi ni vizazi vyao!
Bado wapo watoto na wajukuu wa akina Aziz Ally, Abdulwahid Sykes, Sh. Chaurembo, mzee Tambaza na wengine wengi.
Bila wao, leo hii nyie mlio na midomo mirefu michafu wala msingeweza kuwa huru kuwakejeli watu ambao ki-historia waliojitolea kunusuru na kuipa Uhuru nchi hii.
Ni wao ndio wamewawezesha nyie mliokuja na treni na malori kujiona ndio mabwana wa Dar, wakati ukweli ni kuwa bado ni watwana!!
 
Najiuliza sana nakosa majibu kwa nini huyu raisi JK anapenda sana kuongea hao wazee walioko nchini wanasikia tuu.hamna lolote wanachofanya hawa wazee kwa nini raisi hakai na wasomi au vijana iwe maswali na majibu kama nchini za mwenzetu kama ulaya wanavyofanya ndiyo tutatujua kuwa huyu raisi kweli au mwongo.Inaonyesha hawa wazee kwanza hawana akili za kumuuliza raisi kuwa unakuja kukutana na sisi kwa nini hawa wazee wapo kama bendera fuata wakiitwa wanaenda tuu ..mbona utawala wa raisi mkapa au mwinyi hatujawahi kusikia kukutana na wazee miaka zilizopita.JK hawa wazee wanapenda kuongea nao nini?
 
Back
Top Bottom