Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LordJustice1, Nov 19, 2011.

 1. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sijajua masuala mazito yahusuyo hatima ya nchi yetu kupitia mchakato wa Katiba mpya kuzungumzwa kwa "wazee wa CCM wa Dar es Salaam!" Najua baadhi yenu mtasema kuwa Rais alikuwa anaongea kwa Taifa zima lakini implication iliyoonekana imekaa kichama zaidi kuliko kitaifa!

  Hivi nchi hii imebaki ya hawa wazee wa DSM tena wa CCM au namna gani? Si ingekuwa ni vema Rais angeandaa kipindi ambacho watu wengi wangeshiriki tena kwa kuuliza maswali, kuliko kuhutubia hao wazee ambao wengi wao walikuwa wamelala usingizi na kushtuka baadhi yao wakiwa wanapiga makofi!
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu tutaendelea kuona mengi mengi eti wanachama wa CCM ndio wazee wa Dar na TV station zote zikaonyesha LIVE, kumbe mkulu anajiabisha....
   
 3. m

  maggid Verified User

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  TANGU ‘Enzi za Mwalimu’, kukiwa na jambo kubwa kitaifa, basi, Mwalimu aliliongea kupitia kwa “ Wazee Wa Dar Es Salaam”. Na mahali haswa wanapokutana ‘Wazee wa Jiji’ kumsikiliza ‘ Mkuu Wa Kaya’ ni pale Upanga kwenye Ukumbi wa Diamond.

  Jambo hilo lililoasisiwa na Mwalimu sasa limekuwa ni utamaduni wa kisiasa. Mathalan, ni pale Upanga Diamond Jubilee ndipo Mwalimu alipotangaza vita dhidi ya Idi Amin kupitia Wazee Wa Dar Es Salaam.

  Nilipokuwa mtoto pale Ilala, nilitamani sana nikue nije kuwa mtu mzima, kisha niwe mmoja wa ‘ Wazee wa Dar Es Salaam’ ! Ndoto yangu hiyo imefutika! Naam, nimepoteza sifa ya kuwa ‘ Mzee wa Dar Es Salaam’!

  Ndio, sifa ya kwanza ya kuwa ‘Mzee wa Dar Es Salaam’ ni lazima uwe na zaidi ya miaka 50, uwe mkazi wa Dar Es Salaam kwa miaka isiyopungua 20 mfululizo! Hilo halijaandikwa popote lakini ‘Wazee’ wenyewe wa jiji wanauzingatia utaratibu huo.

  Siku za karibuni kuna “Kijana wa Dar es Salaam” kaninong’oneza kuwa wako mbioni kuwashawishi wazee wa jiji waongeze sifa za kuwa mzee wa Darisalama. Kwamba ili uwe Mzee wa Dar Es Salaam ni sharti, ama uwe umezaliwa na kukulia Dar, au umezaliwa nje ya Dar lakini ujana wako wote umeishi Dar. Hivyo basi, unapoteza sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam kama umekuja Dar ukubwani! Marekebisho hayo ya taratibu na sifa yakifanyika, huenda hata mie nitakuwa na sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam.

  Na Wazee wa Dar Es Salaam wana Mwenyekiti wao. Kwa kawaida siku ya ‘shughuli’ ya wazee, huvalia kanzu, kibagharashea na kizibau. Ndiye huyu ambaye huwa wa kwanza kumpokea ‘Mkuu wa Kaya’ anapoingia ukumbini kuwahutubia wazee.

  Ni kwa namna gani basi Mwenyekiti wa Wazee wa Dar Es Salaam anachaguliwa?

  Jibu: Hilo ni swali la kizushi na usithubutu kuliuliza mbele ya ‘Wazee wa Dar es Salaam’- watakutoa mbio kwa bakora! Lakini lililo dhahiri ni kuwa, Wazee Wa Dar Es Salaam hawajawahi kuwa na Mwenyekiti mwanamke. Hata Bi. Titi Mohammed hakupata kufikiriwa. Heshima ya kumpa barabara kuitwa kwa jina lake ilitosha, na amshukuru Julius, wanasema Wazee ‘orijino’ wa Dar Es Salaam.

  Ndio, Mkuu yeyote wa Kaya katika nchi hii atashauriwa aongee mbele ya Wazee wa Dar Es Salaam kama ana kubwa analotaka liwafike wananchi. Ni mara moja katika miaka ya karibuni nimemsikia Rais wa nchi akilihutubia taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dodoma.

  Inasemekana jambo hilo liliwashtua baadhi ya Wazee wa wa Dar Es Salaam. Na kuna siku nilitembea kwa miguu mitaa ya Kariakoo Kusini; Livingstone, Mahiwa, Swahili na mingineyo. Hatimaye nikafika kwenye kijiwe cha chai na kahawa pale Mtaa wa Lumumba. Nilianzisha mjadala juu ya Wazee wa Dar Es Salaam. Na hapo nikayasikia manung’uniko.

  Ndio, baadhi ya Wazee wa Dar Es Salaam wanaamini kuwa Ilala ndio Dar Es Salaam. Na kwamba ni Wazee wa Ilala ndio waliompokea Julius Nyerere alipoingia mjini. Wanahoji; Iweje Wazee wa ‘mashambani’ Kinondoni na Temeke nao waitwe Wazee Wa Dar Es Salaam? Swali linabaki; Wazee Wa Dar Es Salaam ni akina nani?

  Maggid Mjengwa,
  Iringa,
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Watakuwa wale wanao kaa kwenye vijiwe vya kahawa.
  Na wale wanao kaa makao makuu ya Simba msimbazi na Jangwani wanakunywa kahawa wengine wanacheza draft au bao
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbona umejijibu wewe mwenyewe ndani ya thread yako?
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hapa.....i reserve my comment
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Lazima uwe mwana CCM pia na uwe na vipaji hivi
  1. Kuvaa barghashia
  2. Kupiga miayo
  3. Kunung'unikanung'unika
  4. Kupiga matonge vizuri
  5. KUPIGA VIGELEGELE NA MAKOFI
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Akina Majuto hawaalikwi.
   
 9. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Mjengwa,

  Kwanza natoa pongezi kwa kuibua mjadala huu.

  Mimi binafsi nipo Dar kwa miaka 31 mfululizo lakini jambo ambalo huwa najiuliza ni hivi vigezo vya wazee hawa wa Dar wanavyopatikana na wakawa na tamko dhidi ya wakaazi wote waishio jijini.

  Jambo lingine ambalo huwa linanipa shida ni wazee hawa sifa yao kubwa ni kuvaa nguo za kijani kibichi, pia huwa na Mwenyekiti ambaye hukaa meza kuu ingawa huwa hana sauti ya kutaka maswali miongoni mwa washiriki wa mkutano huo, lakini tena wakishahutubiwa hata kama hotuba ina kasoro wenyewe hupiga makofi.

  Jambo lingine wakati huu wa maisha magumu utakuta wazee toka charambe wamehudhuria lakini kumbe wanachukuliwa kwenye matawi ya chama na magari na wanarudishwa huko, na jambo la mwisho sijui kama wazee hawa wa mkoa huwa wanajua matatizo yatakayozungumzwa au huwepo ili mradi mtoa hotuba isionekane hakuna anayemsikiliza.

  Naungana nawe Mjengwa ili ajuaye vigezo atasaidia siyo wewe na mimi tu, bali ni watu wengi wanahitaji kujua hili.
   
 10. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Wazee wa daresalaam!
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Huu mfumo wa kutafuta huruma kupitia wazee umepitwa na wakati....nchi imeshikwa na vijana kwasasa,na wazee hawana chao tena ukitaka kufanikiwa ongea na vijana na sio wazee tena..lakini pia mfumo wa kuongea na wazee wa DSM sijui kimsingi sio wazee wa DSM ila ni wazee wa CCM wa DSM ni wa kushangaza,hivi wazee wa mtwara,Lindi,Kigoma,Rukwa nk watapata lini fursa ya kuongea na raisi? Utashangaa wazee watakao kuja leo watakuwa wamavaa vinguo vya CCM na njaa njaa zao.I hate these people wanaojihita wazee wa DSM..
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Ni wazee waliochoka kimaisha,hawana mbele wala nyuma,sijawahi ona mzee mwenye maisha mazuri kaenda kumsikiliza jeikei.
   
 13. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo hakuna wazee wa dsm, kuna wazee wa ccm
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Wacheza bao wa Ilala, na Lazima ujue kushangilia hata upumbavu!
   
 15. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Alafu kwanini maongezi na hao wazee lazima yafanyike IJUMAA.
   
 16. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ni forum ya kupiga majungu na propaganda ili kuwapaka matope madaktari.
  Wengi wa hao wazee wa Dar ni wale ambao hawawezi kuuliza why and how?
  Watahubiriwa na kujazwa ujinga, then it will be broadcasted live on TVs.
  The same propaganda was used by President Mwinyi in 1990 during the UDSM's saga.
  However, report ya Judge Mloso (sikumbuki vizuri jina la judge), ikaja tofauti kabisa na propaganda za Mwinyi.

  Ma Dr. Jiandaeni, Hizo propaganda zitawapa zitawapaka matope na kuwatia hasira!
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wanapasha kwa gahawa na ugolo sasa hivi wakiingia ukumbini JK akikohoa au kupiga chafya utaona wanashangilia
   
 18. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  gogovivu
   
 19. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwanza hawa wazee kwa sasa wamepoteza sifa hawastahili tena kuitwa wazee wa dar es salaam bali wazee wa sisiem....miaka ya karibuni mathalani mwaka uliopita nimeshuhudia kama mara mbili hivi mkuu wa kaya akiongea na wazee wa dar es salaam. Kinachonisikitisha ni kuwa kikao cha kwanza mkuu wa kaya aliongea nao kama wazee wa sisiem wa dar es salaam,cha pili akaongea nao kama wa dar es salaam. Kinachosikitisha ni kuwa marazote alizoongea nao ni kama vile alikuwa akiponda upinzani sasa kwa minajili hii nazani ni bora wakaitwa wazee wa chama !!!!!
   
 20. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu umeniwahi,na wengi ya wazee hao ni kutoka Ilala na Temeke,na hasa wa Ilala wao ndio uwa wanajiita wenye jiji,elimu hawana,maisha ya kueleweka hawana,wao ni vijiweni na story za kale tu na story za Simba,Pan na Young,wazee waliostaarabika wako mbali kabisa na hao wazee!
   
Loading...