Asprin
Platinum Member
- Mar 8, 2008
- 68,321
- 96,551
"Mbwa mzee hafundishwi sheria, nimesema utafanya kama nilivyosema" hapa kisingizio cha maagizo ya mwalimu shuleni nayaweka pembeni
"Utaleta fimbo nikuchape au nikaitafute mwenyewe" ... hapa nilikuwa nawahi kuitafuta nimpelekee
"Hako kadude kako nilikaona kabla hujakaona, sasa wewe kaendekeze nikuzike ukiwa na kilo mbili"
"Kama baba yako anakudekeza leo mwambie akupikie chakula"
Siku ya harusi yangu "Baba yako hajawahi kunyoosha mkono wako kanipiga, kama unamheshimu na kumpenda baba yako utafanya kama alivyofanya baba yako. Usimpige mkeo"... nina miaka 18 ya ndoa sijawahi kumpiga bibi yenu Sky Eclat
Ahsante sana mama yangu Matesha. Umenifikisha hapa nilipo... Nakuombea maisha marefu zaidi ili wajukuu zako wa kike waige hekima na busara zako