Nikiwa Olevel nilianza kutambua ubora wa kwenda chuo kwa ngazi ya Diploma, ila Advance pia ilinivutia kutokana na juhudi niliyokuwa nayo.
Nguvu ya Advance ikwa imeshinda, kufika kule(Advance) nikagundua haikuwa maamuzi sahihi isipokuwa nikutake risk, kwa PCB mziki haukuwa wa kitoto.
Nikaenda chuo(umri unazidi kukatika) huku ndio nikakutana na balaa lenyewe sasa, a lot of ups and downs with heavy depression. Halafu ndio mtoto wa mkulima sasa huko kijijini wanaanza kusema mtoto/ndugu yetu amekaribia kutoboa.[emoji3][emoji3]
Unamaliza chuo unaingia mtaani unakutana na balaa la ukosefu wa ajira, what the hell, hapo hapo unakuta na mwana ambaye hakufaulu primary au aliishia form 4 na tayari kashatoboa, unabaki mdogo kama piriton.
NB: Dunia ya sasa inahitaji sana skills ambayo inaweza kupatikana kwa kuspecialize jambo fulani then ukalipractise, watoto/ndugu zetu wanaomaliza form 4 tuawasaidie kupata hizi skills kuliko na kupoteza muda bila kupata skills halafu waje waanze kuzitafuta pakiwa too late(kama kwenda Advance then Chuo(degree))