Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Salaam ndugu zangu,
Katuni imekuwa ni michezo/ Filamu muhimu sana katika kusaidia malezi na kuwafariji watoto wetu. Baadhi ya katuni maarufu ni kama Tom and Jerry, Moana, Zootopia, Luca, Sing, Rango na nyinginezo.
Ni kweli kwamba filamu nyingi za katuni zimeundwa kwa ajili ya watoto. Lakini kutokana na kukua kwa teknolojia filamu hizi zimevamiwa na zimekuwa si zenye maudhui ya kitoto pekee. Kuna katuni ambazo zina maudhui ya ngono, matumizi ya lugha ya matusi au mafundisho ya mapenzi ya jinsia moja n.k mfano Familyguy na Bad cat.
Hivyo, pamoja na uzuri na mchango wa katuni katika kulea na kutengeneza furaha za watoto wetu, tunapaswa kuangalia rating ya filamu hizo, kusoma maoni na ushauri kutoka kwa wataalamu kisha kuchagua kilicho bora.