Dhamira (theme) ya mepenzi ya jinsia Moja inapenyezwa kwenye baadhi ya filamu za watoto. Wazazi tuwe makini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,803
4,467
Habari wanajamvi,

Filamu za watoto imekuwa miongoni mwa sehemu muhimu sana ya kulea watoto wetu. Filamu hizi zinajumuisha katuni, TV Shows, Filamu za watu halisi na nyinginezo zilizotengenezwa kumlenga mtoto.

Sote tunajua kuwa filamu na wahusika wa filamu wamekuwa na Athari kubwa kwenye tabia na mienendo ya watoto wetu. Ni kawaida kabisa kwa watoto kujiita majina ya Wahusika walio kwenye filamu na hata kuiga matendo au tabia za wahusika hao. Filamu hizi zimekuwa zinaacha mafunzo makubwa kwa watoto kwa sababu ya kuvuta umakini wao wakati wa kuzifatilia.

Kama ni mfatiliaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari utakubali kuwa kuna vuguvugu na wimbi kubwa la kuwatetea wapenzi wa jinsia moja kutoka maeneombalimbali duniani na hasa kutoka nchi zilizoendelea.

Tayari wenzetu wa jamii/ nchi hizo wanachukulia jambo hili ni kawaida kiasi ambacho wanaliingiza kwenye filamu na katika Mitaala yao ya elimu toka shule za awali mpaka elimu ya juu.

Nimebaini kwamba baadhi ya filamu za watoto za kimagharibu (katuni/ animations) zinazotoka hivi karibuni zimekuwa na maudhui yanayochochea mahusiano ya jinsia moja na kuonesha jambo hilo kawaida kwa watoto. Kuna scenes zinaonesha aidha mtoto wa kiume anavutiwa na mwanaume mwenzie au anambusu (kiss) kama ishara ya kuonesha mapenzi (Tazama movie ya Strange World).

Nchi za wenzetu wakitaka jambo lao wanalisimamia na kutumia mbinu nyingi sana kulieneza. Nilichoona hapa ni kwamba hawa wenzetu wanapenyeza maudui ya namna hii ili kutengeneza kizazi ambacho baadaye kione kuwa na mahusiano au kumtamani mtu wa jinsia yako ni kawaida kabisa.

Kwa kusema hayo, naomba nitumie nafas hii kuwasihi Wazazi na walezi kukagua maudhui ya filamu za watoto kabla ya kuwaachia kuangalia wakiwa wenyewe.

Salaam
 
Back
Top Bottom