SoC04 Wazazi na Malezi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Razorblade

Senior Member
Aug 30, 2019
168
403
Kumekuwa na changamoto kubwa sana ya mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu ya kitanzania na sababu kubwa ya changamoto hii ni wazazi kutoa malezi duni kwa watoto.

Malalamiko yamekuwa mengi sana kuhusu mmomonyoko huu wa maadili kwa miaka ya hivi karibuni lakini inasahaulika kwamba msingi mkuu wa maadili unaanzia kwa wazazi au walezi.

Changamoto hii ya mmomonyoko wa maadili kwenye taifa letu imekuwa ikihusisha zaidi vijana lakini athari hizi huanza kuonekana mapema kabla ya umri wa belehe.

Wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa sana kukua kwa changamoto hii kwa sababu wazazi walio wengi hivi sasa wamepuuza jukumu la malezi wakiamini kuwa malazi, mavazi na chakula ndiyo malezi pekee kwa mtoto na kuacha jukumu kubwa la malezi kuwa chini ya walimu pamoja na viongozi wa dini na kusahau kwamba mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi mwenyewe.

Elimu duni ya kijinsia na kujitambua inayotolewa na wazazi ina mchango mdogo sana katika ukuaji wa mtoto hasa katika kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii imechukua nafasi kubwa sana kwenye jamii yetu lakini bado wazazi hawaonyeshi kulizingatia hili na inafahamika wazi kwa namna gani mitandao hii ilivyo na muingiliano wa watu wengi na wenye tabia tofautitofauti kutoka kwenye mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Balehe ni sehemu ya ukuaji ya mtoto na ndiyo kipindi ambacho wazazi wanapaswa kuwa karibu zaidi na watoto ili kuweza kutoa nasaha pamoja na elimu ya kijinsia, elimu ambayo itatoa muongozo wa jinsi gani mtoto huyo anaweza kuishi katika jamii bila kuleta athari mbaya kimaadili.

Kwa watoto wa kike imekuwa kawaida wanapofikia umri wa belehe kupelekwa kwa ndugu wengine kama shangazi kwa lengo la kupewa elimu ya ukuaji, si vibaya kufanya hivyo lakini hakuna elimu kubwa hasa anayopatiwa binti huyo zaidi ya kuelekezwa namna ya kujistiri pale anapokuwa katika siku za hedhi.

Kwa watoto wa kiume pia kwa maana anafikia umri wa balehe lakini mzazi wa kiume hajali, mtoto anakosa elimu kutoka kwa mzazi inapelekea kufata hadithi za vijiweni ambazo zimefanya vijana wengi wa kiume kuwa na uraibu wa kusisimua sehemu zao za siri.

Vijana wanapitia changamoto nyingi sana hasa vishawishi lakini kutokana na wazazi kutokuwa karibu nao zaidi watoto kushindwa kuwasilisha changamoto zao na kuweza kupatiwa muongozo kutoka kwa wazazi basi huamua kuwasilisha changamoto hizo kwa watu baki ambapo kwa kiasi kikubwa hushindikana kupata utatuzi sahihi wa changamoto hizo.

Matukio ya uhalifu, uasherati pamoja na matumizi ya maadawa ya kulevya wahanga wakubwa ni vijana, vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa lolote duniani lakini nguvu kazi hiyo inazidi kupungua na kupelekea maendeleo ya kusuasua katika nchi yetu.

Mzazi ni wajibu wako kufatilia mienendo ya mtoto wako na kuhakikisha watu gani ambao anakutana nao na katika mazingira gani ambayo hupendelea zaidi kuwepo kwa nyakati tofauti, kufanya hivi kutasaidia kumlinda na kumjenga mtoto katika maadili mazuri.

Taifa linategemea wazazi katika malezi, wazazi hawanabudi kutenga muda maalumu baada ya kipindi fulani kwa ajili ya kukaa na watoto wao ili kuwapa nasaha na kutoa muongozo wa namna gani wanaweza kuishi katika jamii.

Wazazi wanapaswa kuwa karibu zaidi na watu wanaopatikana katika maeneo ambayo watoto wao hutumia muda mwingi zaidi kuwepo ikiwemo walimu shuleni na wahusika wanaopatikana katika maeneo yanayotolewa elimu za dini.

Wahenga walisema “Asiyefunzwa na ***** hufunzwa na ulimwengu”, watanzani kwa ujumla badala ya kuacha jukumu la malezi kwa wazazi wa watoto husika pekee hatunabudi kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha tunatoa elimu kwa vijana ili kuweza kulinda maadili katika jamii.

Walimu pamoja na viongozi wa dini nafasi yenu ni kubwa sana baada ya wazazi, hivyo basi kwa kushirikiana na wazazi mnapaswa kuwa mstari wa mbele katika kulinda vijana na maadili ya kitanzania kwa kutoa elimu stahiki kwa vijana kabla na baada ya balehe.

Wito kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii pamoja na taasisi mbalimbali kushirikiana kwa pamoja kulinda maadili ya kitanzania kwa kutoa elimu kwa wazazi juu ya namna nzuri ya malezi kwa watoto, teknolojia inakua basi ikue sambamba na kuimarisha maadili katika jamii yetu.

Vijana hakikisheni kuwa mnafata mafundisho sahihi ya wazazi, walezi, viongozi wa dini pamoja na watu wanaowazunguka, kujiepusha na matukio ya uhakifu, uasherati pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya, kwa kufanya hivi kutapelekea kuimarika kwa maadili.

Tanzania ni nchi inayohitaji nguvu kazi ya vijana kwa wingi ili kurahisisha kukua kimaendeleo, hivyo basi wazazi na walezi ni wajibu wenu kutekeleza swala zima la malezi vile inavyotakiwa.

Ahsante!
 
Wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa sana kukua kwa changamoto hii kwa sababu wazazi walio wengi hivi sasa wamepuuza jukumu la malezi wakiamini kuwa malazi, mavazi na chakula ndiyo malezi pekee kwa mtoto na kuacha jukumu kubwa la malezi kuwa chini ya walimu pamoja na viongozi wa dini na kusahau kwamba mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi mwenyewe.
Tuchane laivu, makavu🏃

Vijana hakikisheni kuwa mnafata mafundisho sahihi ya wazazi, walezi, viongozi wa dini pamoja na watu wanaowazunguka, kujiepusha na matukio ya uhakifu, uasherati pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya, kwa kufanya hivi kutapelekea kuimarika kwa maadili.

Tanzania ni nchi inayohitaji nguvu kazi ya vijana kwa wingi ili kurahisisha kukua kimaendeleo, hivyo basi wazazi na walezi ni wajibu wenu kutekeleza swala zima la malezi vile inavyotakiwa
Sawa mkuu, kila mmoja atimize majukumu yake katika familia
 
suala la maadili tushazama shimoni yaani hata sijui tuanzie wapi mbaya zaidi hiki kizazi cha vijana wanaosujudia ulevi na ngono, mabinti wadangaji na singo mazaz ndio hawa wazazi wa youth generation ijayo. It sad to they that the worst is yet to come.
 
suala la maadili tushazama shimoni yaani hata sijui tuanzie wapi mbaya zaidi hiki kizazi cha vijana wanaosujudia ulevi na ngono, mabinti wadangaji na singo mazaz ndio hawa wazazi wa youth generation ijayo. It sad to they that the worst is yet to come.
Usasa na ujuaji mwingi, wazazi wengi hivi sasa hawataki hata umkanye mtoto wake anapokosea.
 
Back
Top Bottom