Wazanzibari wapanga kufanya mandamano 1/4/2011 kisa wamechoshwa na Muungano

Status
Not open for further replies.
Toka lini Zanzibar aliwahi kujiendesha yenyewe?, toka utawala wa Sultan, mwingereza then Tanganyika (12 january 1964 mpaka 26 April 1964 this was a period where Zanzibar was de jure independent). lete data ambazo inaonyesha Zanzaibar inaweza simama. You just go away mnatuletea ghasia, we have nothing to loose zaidi ya hao wanasiasa wanautaka muungano ili walinde maslahi yao

Kijana nimesema kuwa huelewi kitu na nikisema sasa itakuwa natowa kejeli lakini waulize wazee wako sabuni za Lux walikuwa wakitumia vipi?
 
Bora wapewe uhuru wao wanaotaka watuachie tanganyika yetu! Wakirudi tena unakuwa mkoa cyo nchi tena. Nchi ina wabunge wengi maraisi wa2 lakini watu hata mil 2 hawafiki wachache kuliko jimbo moja la bongo.
Ukubwa wa puwa si wingi wa makamasi. Kwa udogo wake huohuo Zanzibar ipo na Mzanzibari anajihisi huru kujisema hivyo . Tofauti na wenzetu, hamko tayari kuitwa kwa jina lenu halisi, pengine halisound vizuri sasa.
 
Vunjeni muungano nani anautaka bana tuachieni Tanganyika yetu tupete mnatuzingua tu. Teh teh teh next morning sultani in the house.
 
Kijana nimesema kuwa huelewi kitu na nikisema sasa itakuwa natowa kejeli lakini waulize wazee wako sabuni za Lux walikuwa wakitumia vipi?

Inaonekana huna adabu wala mimi si kijana kwako, hili jukwaa hatufahamiani,mambo ya kuitana vijana hapa wala si mahari pake. Jenga hoja toka lini Zanzabar ilishawahi kisimama kama sovereign state?. Harafu mbona hampendi kuzungumzia historia yenu toka enzi za Utumwa, ili tujue nyie wanaharakati kweli..?? au hamjui nyie mliletwa hapo kama watumwa fikilieni wakati mwingine mjue hata mlikotoka, au mnafikiri nyie asili yenu ni Zanzibar. Hebu na wewe kamuulize mzazi wako ulifikaje Zanzibar atakupa jibu
 
Sauti:Kongomano la katiba – 05 March 2011 | MZALENDO.NET
Wananchi, wazalendo, wapenda amani, maendeleo na utaifa wa nchi yetu ya Zanzibar.
Kufuatia mjadala wa Katiba Mpya unavyoendelea, mengi yamefichuliwa dhidi ya muungano wetu uliodumu kwa miaka 47. Pamoja na nia njema wakati wa kuasisiwa muungano wanchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, kiukweli sasa hivi hali haiku hivyo.
Tumeshuhudia wanansheria wetu, mara kwa mara, wamekuwa wakitoa dosari zao zinazoonyesha kupotea kwa nia njema iliyokusudiwa. Miongozi mwao ni pamoja na kutamka bayana kuwa muungano huu kisheria haipo tena, kilichobaki ni kinadharia tu.
Hivyo basi, ni wakati wetu sote kwa pamoja kuungana katika kudai haki yetu kama raia watiifu kwa taifa letu pamoja na kudai haki za nchi yetu iliyopoteza haki zake kwa kufanya maandamano ya amani.
Madhumuni ya maandamano.
- Kudai muungano ujadiliwe upya na pande zote.
- Kuunga mkono matamko yanayotolewa na wanasheria wetu kwenye mjadala wa katiba.
- Kutoa muamsho kwa jamii na wananchi juu ya kutetea haki za nchi na taifa letu – Zanzibar.
Petition itakuwa na ujumbe ambao ni open letter itakayo beba ujumbe mmoja wa madai yetu kwa sehemu zote zitakazofanyika maandamano.
Siku ya Maandamano.
Maandamano yamepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 1/04/2011. Ijumaa ni siku ya mwisho wa wiki, itakuwa muafaka kwa Wazanzbibar wengi kuweza kushiriki. Vilevile itakuwa ni wiki nne kabla kufanyika sherehe za Muungano hapo 26/04/2011. Wale walioko makazini tunaomba waombe likizo zao mapema ili waweze kushiriki.
Eneo la Maandamano.
Maandamano yatafanyika ulimwengu mzima.
Kitovu cha maandamano haya kitakuwa ni ndani ya Zanzibar, ambapo Petition ya madai yetu itawasilishwa kwa Waziri wa Sheria na Katiba na Mwanasheria Mkuu wa SMZ.
Kwa wale walioko Tanzania Bara, wao watawasilisha Petition yao kwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa nchi nyengine dunia, Wazanzibar na Watanzania kwa jumla, watafanya maandamano kwa kila nchi yenye ubalozi wa Tanzania. Petition zitawasilishwa kwa mabalozi wa nchi husika ili kuziwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambae wakati huohuo anakuwa Rais wa Shughuli za Serikali ya Tanganyika pamoja na Rais wa Zanzibar.
Yanayohitajika
Tunaomba ushirikiano kutoka kwa Wazanzibar wote ulimwenguni kufanikisha shughuli hii. Tunahitaji mawakala wa kusimamia kutoka kila nchi husika. Hii itasaidia kufikisha ujumbe kule tunakokusudia.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nami kupitia email yangu ashakh@mzalendo.net
NOTE: Msisitizo unatiliwa kuwa haya ni maandamano ya amani, kwa lengo la kudai haki zetu.

Sawa bana. Yetu macho. Lakini nakwambia haya maandamano utaishia kufanya wewe, mke wako na utitiri wenu uani kwenu.
 
Kwanza Mtumwa ni mzee wako wa upande wowote. Wewe mwenyew huijuwi Historia la usingewaita watu watumwa. Watumwa walitoka Tabora, Kigoma Mwanza na kwengineko Tanganyika na Wazanzibari walikuwa madalali. Naona uelewa wako wa suala hli ni mdogo sana kijana. Waliofanya Mapinduzi wengi wao walikuwa hao unaowasema wewe na kwa taarifa yako Zanzibar ilikuwa na Washirazi, Watumbatu na machotara ambao hawakuwahi hata siku moja kuwa watumwa. Nenda darasani ukajifunze ili unapoamuwa kutukana matusi hayo yasikurudie mwenyewe1
Wewe hujui Historia staki kuanza kukufundisha hapa ila ujue tu kwamba watumwa wengi walitoka DRC kupitia Kigoma, Tabora mpaka Bagamoyo. Kasome kazi alizofanya Tipputippu ndani ya DRC, wala si waha wa Kigoma walikamatwa kwa wingi kwani Historia inaonyesha wazi waha wakuwahi huwa na strong empire zilizoshughulika na biashara ya utumwa. Dalali wa Biashara ya utumwa Zanzibar alikuwa Sultan na wala si hao watumbatu unaowasema, hao wote walikuwa watumwa. Ni wazi kwamba baada ya kutokomezwa kwa utumwa watumwa waliokuwa wakivuna minazi na karafuu walibaki Zanzibar ndio nyie mnaosumbua sasa na damu yenu ya DRC.
 
Zanzibar si nchi.Unguja na Pemba ni Viwilaya wala si Mikoa.Bora mjitenge na Tanganyika mnatufilisi
 
Toka lini Zanzibar aliwahi kujiendesha yenyewe?, toka utawala wa Sultan, mwingereza then Tanganyika (12 january 1964 mpaka 26 April 1964 this was a period where Zanzibar was de jure independent). lete data ambazo inaonyesha Zanzaibar inaweza simama. You just go away mnatuletea ghasia, we have nothing to loose zaidi ya hao wanasiasa wanautaka muungano ili walinde maslahi yao

zanzibar ni kama mkasi, haukati mbele bila kushikwa nyuma. Kama wanataka iwe somalia mpya, ok. Sie tumewasitiri tu, chizi akikataa nguo unamfanyaje?
 
Naona sasa Tanzania kumekucha. Hizi zote ni harakati nzuri ambapo hutokea pale jamii yoyote inapokuwa na kuhitaji kupata nafasi ya kusonga mbele zaidi. Hivyo ni wakati mwafaka kwa Wazanzibar pia kutafuta mahali pa kupumulia kama wanaona kuwa haki haitendeki/haipatikani sehemu fulani fulani hivi. Kwa kiasi fulani muungano huu umekuwa ukiwanufaisha kiasi fulani wakubwa/wadosi wa zanzibar (mfano wabunge n.k) lakini hapohapo ukionekana kama kuwanyima fursa katika uso wa Dunia, kwani ukishatoka Tanzania, Zanzibar ni sawa na mkoa mwingine wowote ule wa Tanzania (HILI TUSIBISHE). Hivyo jinsi sisi na CDM wanapopingana na kupanda kwa hali ya maisha, si vibaya nao wakafikiri jinsi ya kuondoka kwenye nira za Watanganyika kwa kuwa wanaona muungano haujakidhi haja yao.
 
Kila April 1 ni siku ya wajinga! Imekaaje hii? Siamini kama wazanzibari wanaweza kuandamana siku ya wajinga! Unatuhakikishia vipi?
 
Jamani..................... Naomba kuuliza?? Muungano ukifa na Urais wa JK unakoma??? Au?? Can't wait ...........................!!! Go ZNZ go...... PIPOS............... POWER!!!!!!
 
abdulahsaf, kwa definition iliyotolewa na TEDNWA na sisiem , maandamano kama haya yanaweza kuangusha serikali iliyoko madarakani. wakati wa kampeni umeisha watu wapeleke hoja bungeni na halmashauri za miji ili wawakilishi wao wazijadili kwa lengo la " kudumisha utawala uliopo madarakani" . Pamoja na hayo ninaunga mkono wtu kutoa mawazo yao, kama watawala hawana hoja kiasi hicho basi watafute njia nyingine ya kutekeleza wajibu wao badala ya kuanza kukumbatia mawazo mgando.
 
Nitashukuru sana kama wazanzibar kama watajitenga,ili na sisi tuigenge nchi yetu upya!!wananiboa sana,siupendi muungano!hawa jamaa wanabembelezwa sana na CCM!Waondoke wao na CUF yao!!
 
Mataarisho yapoo na yanaendelea,haya sio maandamano ya siasa na ya wananchi wote kwa ujumla zanzibar,,,,,mungu akipenda yatakuwa ya amani,,,yatafanyika kila pembe ya dunia,siku ni nzuri sana wala sio mbaya kabisaa muda muafaka, Pia kuna hati za muungano feki tutaziorezesha kila Office ya UNITED Nation,,,,,tutazisambaza kila kona ya dunia.. tunaomba ushikiano wenu....mi pia naunga mkono,

......na mimi pia, coz mkiipata ZANZIBAR yenu na sisi tutapata TANGANYIKA yetu:hand:
 
Ngekewa,

Kasome historia ya Mirambo. Huyu Mzee alikuwa hadi na Urafiki na Waarabu. Aliwachapa na kuwapa kibano cha nguvu hadi wakawa wakipita Tabora basi wanalipa kodi.

Tatizo la Zanzibar ni kuwa kila mtu mweusi au mwenye asili ya BARA basi mnamwita Mnyamwezi. Wale watu, wengi wao si Wanyamwezi. Wengi walikuwa wametoka maeneo mbali na Unyamwezi.

Kama Wanzanzibar wanataka kujitenga, si waombe tu WAJITENGE? Kwani nani hataki wajitenge? Sisi tunacholaani ni hii tabia ya KULIALIA kwa mambo mengine na kusubiri BARA wachukie na wawafukuze kwenye MUUNGANO. Mngeliungana na kuja na kauri moja kuwa HATUTAKI TENA MUUNGANO. Tungeliachana kwa amani.

Hali ilivyo sasa na hasa ukiangalia ushiriki wa CUF huku bara, kunazidi kuongeza uhasama wa Wabara kwa watu wa visiwani. Itapelekea kuwa siku tunavunja Muungano, basi hatupendani kama Rwanda na Uganda. TOKENI ZENU na muende salama.
 
Kwanza Mtumwa ni mzee wako wa upande wowote. Wewe mwenyew huijuwi Historia la usingewaita watu watumwa. Watumwa walitoka Tabora, Kigoma Mwanza na kwengineko Tanganyika na Wazanzibari walikuwa madalali. Naona uelewa wako wa suala hli ni mdogo sana kijana. Waliofanya Mapinduzi wengi wao walikuwa hao unaowasema wewe na kwa taarifa yako Zanzibar ilikuwa na Washirazi, Watumbatu na machotara ambao hawakuwahi hata siku moja kuwa watumwa. Nenda darasani ukajifunze ili unapoamuwa kutukana matusi hayo yasikurudie mwenyewe1

Huko central Africa ndiko mlikotolewa na Tiputipu kama hamjui! (soma attachment)
 

Attachments

  • New Microsoft Word Document.docx
    59.5 KB · Views: 132
Inaonekana huna adabu wala mimi si kijana kwako, hili jukwaa hatufahamiani,mambo ya kuitana vijana hapa wala si mahari pake. Jenga hoja toka lini Zanzabar ilishawahi kisimama kama sovereign state?. Harafu mbona hampendi kuzungumzia historia yenu toka enzi za Utumwa, ili tujue nyie wanaharakati kweli..?? au hamjui nyie mliletwa hapo kama watumwa fikilieni wakati mwingine mjue hata mlikotoka, au mnafikiri nyie asili yenu ni Zanzibar. Hebu na wewe kamuulize mzazi wako ulifikaje Zanzibar atakupa jibu

Mkuu niafafanulie signature yako...imeniacha hoi kidogo
 
Bravo Zanzibarians niko nyuma yenu! Afadhali our motherland Tanganyika irudi, mmetunyonya vya kutosha!
 
Sioni sababun ya huu muungano fake. Tupate Tanganyika yetu na wao wote Wapemba na Waunguja warudi kwao kutoka Tanganyika yetu. Kundi kubwa la Wabunge kutoka huko hadi Dodoma kupiga porojo na kula mabilioni ya hela zetu. Watu si zaidi ya 1m lakini kelele za utaifa haziwaishi. Tanganyika haipotezi kitu wakiondoka. Katika hilo JK nitampa tano bora.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom