Waumini Wamzawadia gari mpya Askofu Mkuu Mstaafu wa KKKT Dkt. Shoo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,127
Askofu Mkuu Mstaafu wa KKKT Dr Shoo amekabidhiwa gari mpya Toyota Landcruiser ya Mwaka 2023 mpya kabisa 0 km iliyonunuliwa kiwandani

Ahadi ya kumnunulia Zawadi ya gari ilitolewa kwenye misa ya shukrani ya Mchungaji Dkt. Kimaro ambapo Wabunge, Mawaziri, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Siasa na Waumini walihudhuria miezi michache iliyopita

Waliohudhuria ibada ya Dr Kimaro ni Pamoja na Waziri wa Fedha Dr Mwigulu Nchemba PhD, mh Halima Mdee, mh Esther Bulaya, mh Sanga, Godbless Lema nk..nk

Na katika makabidhiano ya zawadi ya gari nyumbani kwa askofu Dr Shoo walikuwepo mh Kidiva, mh Sanga, mh Mbowe nk.

Mlale Unono

---
Askofu Mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT anayemaliza muda wake Dr. Fredrick Shoo leo amekabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota Land Cruiser GR Sport ikiwa ni ahadi iliyoanza kufanyiwa kazi baada ya mmoja wa Waumini wa KKKT Noah Kadiva kutoa wazo hilo Kanisani Kondeni Matala Kilimanjaro katika ibada ya shukrani ya Mchungaji Dkt. Eliona Kimaro April 23 2023.

Baada ya wazo hilo ambalo lilipokelewa kwa mwitikio mkubwa iliundwa Kamati ya zaidi ya Watu 60 wakiwemo Wabunge, Wanasiasa, Wafanyabiashara na Waumini wa madhehebu mbalimbali wakiwemo wa KKKT na hatimaye leo Dkt. Shoo amekabidhiwa zawadi hiyo nyumbani kwake Mailisita, Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Noah Kadiva amesema gari hilo Land Cruiser GR SPORT la mwaka 2023 (zero Kilometer) limenunuliwa
 
1695503066990.png
 
Pumbavu.... Unafiki, , upuuzi...

Dini ni kivuli cha unafiki na uzandiki, nadhani huyo mzee wangempongeza tu kwa shukran pekee badala yake fedha za kununulia hilo gari la bei kubwa wangekusanya hizo pesa kusaidia wagonjwa na wahitaji mbalimbali nchini.

Ndio yale yale waumini wanakufa njaa kwa kuyatolea hayo matepeli(wachungaji) na kuaminishwa wataombewa na kubarikiwa na Mungu wakat huo huo hayo matapeli(wachungaji) yakipata shida yanataka kuchangiwa na fedha ked kede.


Ifike mahala watanzania waelewe hilo jambo japo linauma, ukiona humo hata walioshiriki hiyo ibada ni wapigaji+wanafiki watupu.

Note: kuna vichaa watasema nisiwapangie matumizi, hakuna cha kupangiwa wangetaka kumpa zawadi huyo tapeli basi wangetoa nje ya kanisa na kivuli cha dini.
 
Back
Top Bottom