Watumishi 15,578 waliobainika kughushi vyeti na kupata ajira hawastahili kurudishwa kazini wala kulipwa malipo yoyote!

Mwalaye

Senior Member
Jun 17, 2021
171
232
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
===

SERIKALI imesema watumishi 15,578 waliobainika kughushi vyeti na kupata ajira hawastahili kurudishwa kazini wala kulipwa malipo yoyote.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa alisema hayo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Akitoa ufafanuzi wa sintofahamu inayoendelea katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii juu ya watumishi hao, Mchengerwa alisema msimamo wa serikali juu ya watumishi walioghushi vyeti vya elimu ya kidato cha nne na sita na ualimu uko pale pale na hakuna mabadiliko mengine.

Alisema serikali imepata mafanikio makubwa tangu kupatikana kwa Uhuru mwaka 1961 ikiwa ni pamoja na kuongeza watumishi wa umma kutoka watumishi 17,565 mwaka 1961 hadi watumishi 528,290 Oktoba mwaka huu.

Kati yao, watumishi wa sekta ya afya wamefikia 72,961 sawa na asilimia 13.8 na walimu wamefikia 281,729 sawa na asilimia 53.3.
Mchengerwa alisema serikali iliwaondoa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi 15,578 waliobainika kughushi vyeti vya ufaulu mtihani wa kidato cha nne, sita na ualimu kati ya watumishi 535,770 waliohakikiwa.

Iliwaondoa pia katika orodha ya malipo ya mishahara watumishi 5,335 walioajiriwa katika utumishi wa umma kinyume na sifa za miundo ya maendeleo ya utumishi na kubaki na watumishi wenye sifa stahiki.

Alisema katika jitihada hizo, serikali imeokoa jumla ya Sh bilioni 19.8 kwa kuwaondoa katika orodha ya malipo ya mishahara hewa watumishi 19,708.

Mchengerwa alisema serikali kupitia ofisi yake imefanikiwa kuwarejesha kazini na kuendelea kuwalipa mishahara jumla ya watumishi 4,380 walioondolewa katika orodha ya malipo ya mishahara kimakosa wakati wa uhakiki wa vyeti vya elimu na watumishi hewa.
Idadi hiyo inajumuisha watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na watendaji wa mitaa wapatao 3,114.

Alisema pamoja na kuwarudisha watumishi hao kazini, serikali ilitoa msamaha wa kuwarejesha kazini watumishi walioondolewa kazini kwa kukosa sifa za elimu ya kidato cha nne na baadaye wakajiendeleza na kupata sifa tajwa hadi kufikia Desemba mwaka jana.

Mchengerwa alifafanua kuwa msamaha uliotolewa unawahusu watumishi walioajiriwa baada ya Mei 20 mwaka 2004 bila sifa ya elimu ya Kidato cha Nne lakini baadaye wakajipatia sifa za kuajiriwa.

Haukuwahusu watumishi waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi au waliotoa taarifa za uongo katika kumbukumbu zao rasmi za kiutumishi.

Alisema pamoja na hayo, serikali imefanikiwa kulipa madai ya mishahara ya jumla ya Sh bilioni 2.6 kwa watumishi 1,643 waliorejeshwa kazini baada ya kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kimakosa. Uhakiki wa madai yaliyobaki unaendelea na yataendelea kulipwa kwa kadri itakavyobainika.

CREDIT: Habari Leo
 
Inaumiza, inauma sana, imetugharimu sana tuliokutwa au ndugu zetu kukutwa na janga hili lakini ni muhimu kufanya mambo sahihi kadri inavyotakiwa

Mimi binafsi watu wangu wa karibu sana wamepigwa na hili janga na familia zimeyumba na imetugharimu lakini kamwe siwezi kuilaumu serikali na kumtetea mtu aliyenunua au kughushi vyeti. Kamwe!!!!

Kosa ni kosa tuu haijalishi linakufaidisha au kukubeba kwa kiasi gani
 
Roho mbaya za kubaniana mbona kikwete aliwalipa wote hao na kuajiri maelfu ya vijana kuanzia ualimu Hadi udaktari
Unalipwa isiyo haki yako? Ni taifa la wajinga tu ndo hufanya hivyo, taifa lisilofuata misingi ya kisheria.
 
Unalipwa isiyo haki yako? Ni taifa la wajinga tu ndo hufanya hivyo, taifa lisilofuata misingi ya kisheria.
Hao wangekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kujipatia pesa kiudanganyifu na kugushi nyaraka za serikali...
 
Bajeti ya 21\22 ni kama 33t, ya mwaka 22/23 ni kama 39t. Kutakuwa na bonge la ongezeko la mshara. Hakuna atapungukiwa take home ya 50,000 kwa kima cha chini. Mama oyee
 
Kama ni SHERIA, mbona wale wanaovaa nguo zenye nanii hawajaguswa :D :D , tena kule wamejazana.... Kweli ni udanganyifu ila wametafutwa wale WANAOWEZWA tu...
 
Hao wangekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kujipatia pesa kiudanganyifu na kugushi nyaraka za serikali...
Mkuu; ..."wangekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kujipatia pesa kiudanganyifu na kugushi nyaraka za serikali... " Kweli kabisa100% lakini Serikali kwa busara zake iliamua kuachana nao kimya-kimya. Yule aliyekuwa anadhani kaonewa alipewa fursa ya ku-appeal na wapo kweli waliorudishwa kazini.
 
Unalipwa isiyo haki yako? Ni taifa la wajinga tu ndo hufanya hivyo, taifa lisilofuata misingi ya kisheria.
Na ni wajinga tu wanaoona kulipa watu wasio stahili ni vyema na haki.
Forgery is a Crimal case by Law...
Sasa km tunaona ni vyema na haki watu kulipwa wasicho stahili then some how, somewhere in our brains kuna tatzo la msingi kabisa.
#banana republic
 
Back
Top Bottom