A
Anonymous
Guest
Sisi watumishi ajira mpya kutoka maeneo tofauti tumeshirikiana kuandika andiko hili kuhusu malipo ya fedha za kujikimu ambayo yamekuwa kizungumkuti kwetu, lengo ni mamlaka zipate kujua kinachoendelea na tuweze kusaidiwa.
SIKONGE, TABORA
Tunaomba Wanahabari mtusaidie kupaza sauti kuhusu hili jambo, sisi ajira mpya katika Wilaya ya Sikonge, Kada ya Ualimu Msingi, tangu mwezi wa sita hela ya kujikimu hatujaipata.
Mpaka leo (Septemba 27, 2023) bado hatujalipwa ili hali hela hiyo unatakiwa kulipwa kabla ya kuanza kazi na huu mwezi wa tatu tangu tumeanza kazi.
Malipo haya tunatakiwa kulipwa zile wiki mbili za mwanzo unapopewa muda wa kujiandaa kabla ya kuanza kazi rasmi, kuna gharama flani ya kuanzia maisha.
Tumejaribu kufuatilia tunaambiwa fedha zimeshafika lakini ukiulizia unaambiwa tuwape muda, Mkurugenzi yeye tulimbana wiki iliyopita akasema fedha zimeshafika kwa idara, tuwaulize huko.
ROMBO, KILIMANJARO
Upande mwingine Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro pia tuna changamoto ya kutolipwa fedha za kujikimu.
Sisi Walimu tuliajiriwa Juni 2023 lakini mpaka leo hatujapata malipo hayo, tumeshadai muda mrefu lakini tunabaki njia panda, tupo na wenzetu Madaktari, Wauguzi wa kike pamoja na sisi Walimu.
Mwaka jana na mwaka juzi wenzetu walipata changamoto kama hiyohiyo, ilifikia hatua hadi wakaandamana ndio wakapata haki yao.
Safari hii (2023) hali inaendelea vilevile, tulitakiwa kupata ndani ya wiki mbili za kwanza lakini mpaka leo, Halmashauri za wenzetu huku Kilimanjaro tumesikia wameshapata lakini sisi tu ndio bado na tunasikia hela zimeshatoka TAMISEMI.
Kama zimetoka TAMISEMI, kwa nini hawatupi malipo yetu? Ukiuliza kwa Mkurugenzi (Godwin Chacha) hatoi ushirikiano mzuri, kila wiki tunaenda ofisini kwake lakini hakuna kinachopatika cha maana.
Pia soma
= Waziri Mchengerwa aagiza Fedha za Kujikimu za Ajira Mpya zilipwe kabla 30 Oktoba, 2023
= Waziri Mchengerwa njoo Halmashari ya Ngara Watumishi Wapya hatujalipwa Fedha za Kujikimu