WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira wahukumiwa kifo!

Hii kesi imechukua Miaka miwili tu tangu kuanza kusikilizwa mpaka hukumu.
Kumbe inawezekana kusikiliza kesi kwa muda mfupi ee?
Manake wapo wanaosota Mahabusu zaidi ya miaka kumi kwa kesi za mauaji kama hizi.
What's up Tanzania?
 
Msamaha wa raisi hawezi kutoa msamaha kwa makosa ya mauaji ,ujambazi wa kutumia silaha na kesi za uhujumu uchumi!sheria za nchi zinakataza!

Mkuu Presidaa amepewa uwezo wa kubadilisha hukumu toka kunyongwa hadi maisha.. Au kuwapa msamaha baada ya kutumikia kifungo kwa muda wa miaka kadhaa..
 
Geuzeni hiyo bahasha ili tuone kilichomo!

katika kesi hii inasemekana kulikuwa na kihoja cha aina yake; inabidi mfumo wetu wa sheria uangalie upya suala zima la kuwatumia wazee wa baraza kama hawa, ambao hali zao tu zinaonyesha wako katika mazingira rahisi mno ya kuhongwa na kupindisha ukweli.

Na ikiwa hakimu mwishowe hazingatii ushauri wao, kuna haja gani ya kuwa na wazee wa baraza?

jana katika mahakama kuu kanda ya dar es salaam wazee wa baraza katika kesi ya swetu fundikira waliushangaza umma uliohudhuria kesi hiyo (nafikiri hata na ndugu wa washtakiwa hawakutegemea kile walichosikia) baada ya wote watatu kudai kuwa washtakiwa waachiwe huru kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa wao walimuua swetu fundikira. Aliyetoa kali kabisa ni mzee raha saidi aliyedai polisi wamewabambikia kesi washtakiwa ki ujanja ujanja. Mzee mwingine ali kampea alidai kifo cha marehemu ni ajali tu kwani alianguka ndipo akaumia kichwani na kupeleka kifo chake. bibi johari yeye alidai kuwa yeye haoni kama washtakiwa walikuwa na nia mbaya na hatimaye kumuua swetu fundikira bali washtakiwa ni watu wazuri na nia yao ilikuwa ni kumpeleka polisi tu na si vinginevyo hivyo yeye anaona hawana hatia.
sam_3574.jpg

 
WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT - Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi leo wamehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. HABARI NA PICHA ZAIDI KUWAJIA HIVI PUNDE!

HUYU SWTU FUNDIKIRA ni MZANZIBARI au MTOTO wa Marehemu CHIEF FUNDIKIRA?

MUNGU IBARIKI ZANZIBAR MUNGU IBARIKI SERIKALI YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.AMIN.
 
Mbona kama kuna walakini katika hukumu?wazee wa baraza kupingana na hukumu ya jaji!kuna nini hapo?kwa nini maamuzi yametoka tofauti na maoni ya wazee wa baraza?ina maana gani kuwa na wazee wa baraza?
 



mkuu maneno yako ya busara sana!
Uliwahi kujinasibu hapa kwamba umewahi kupewa makuzi ya kiislam kupitia madras! lakini kwa kushabikia upuuzi huu ninawasiwasi sana kama kweli malezi hayo yalikuwa na manufaa yoyote kwako zaidi ya kukufanya mtumwa wa ujinga na fitina/uzandiki!
 


Uliwahi kujinasibu hapa kwamba umewahi kupewa makuzi ya kiislam kupitia madras! lakini kwa kushabikia upuuzi huu ninawasiwasi sana kama kweli malezi hayo yalikuwa na manufaa yoyote kwako zaidi ya kukufanya mtumwa wa ujinga na fitina/uzandiki!

umeona hao wenzako walivyoandika hapo juu! ulitaka niwagogee like huku wakikashifu iman yangu ...??? si utakuwa ni ujuha huo

mbona wakurupuka

again jibu la mkuu ni la busara na linastahiki kwa comments zenu mlizo mwaga
 
Katika kesi hii inasemekana kulikuwa na kihoja cha aina yake; Inabidi mfumo wetu wa sheria uangalie upya suala zima la kuwatumia wazee wa baraza kama hawa, ambao hali zao tu zinaonyesha wako katika mazingira rahisi mno ya kuhongwa na kupindisha ukweli.

Na ikiwa hakimu mwishowe hazingatii ushauri wao, kuna haja gani ya kuwa na wazee wa baraza?

Jana katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam wazee wa baraza katika kesi ya Swetu Fundikira waliushangaza umma uliohudhuria kesi hiyo (nafikiri hata na ndugu wa washtakiwa hawakutegemea kile walichosikia) baada ya wote watatu kudai kuwa washtakiwa waachiwe huru kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa wao walimuua Swetu Fundikira. Aliyetoa kali kabisa ni Mzee Raha Saidi aliyedai polisi wamewabambikia kesi washtakiwa ki ujanja ujanja. Mzee mwingine Ali Kampea alidai kifo cha marehemu ni ajali tu kwani alianguka ndipo akaumia kichwani na kupeleka kifo chake. Bibi Johari yeye alidai kuwa yeye haoni kama washtakiwa walikuwa na nia mbaya na hatimaye kumuua Swetu Fundikira bali washtakiwa ni watu wazuri na nia yao ilikuwa ni kumpeleka polisi tu na si vinginevyo hivyo yeye anaona hawana hatia.
SAM_3574.JPG

Hivi vikongwe vinatakiwa mahakama ya kadhi sio hapa
 
Hapa suala la udini linaonekana halipo sababu mhanga Swetu Fundkira, na Wazee wa Baraza inavyo onekana (angalau kulingana na majina) wote ni Waumini wa dini ya Kiislamu.

Kwa hiyo basi, hawa Wazee wa Baraza watakuwa na sababu zao za msingi zilizowafanya kufikia uamuzi waliofikia, kwa hiyo msidharau hilo.

Hakuna habari au maelezo yoyote kuonyesha ushahidi wa upande wa mashitaka, ili watu waweze kutathmini ubora na ukweli wa upande wa pili, na vigezo gani walivyotumia Wazee wa Baraza kufikia uamuzi wao.


Hawa Wazee wa Baraza wanaweza kuwa hawajakosea kwenye maamuzi yao, hadi tupatiwe story nzima na ushahidi wa upande wa mashitaka ili tutathmini ukweli upo wapi.
 
Naona wadau mmeamua kuwa street lawyer,nawashauri kabla ya kuamua kwa kutumia mioyo yenu,mtumie akili zenu.Someni hukumu then ndo mjue kama hawa wanajeshi hiyo hukumu ni sawa ama la,na kwa haraka haraka nimeona kuwa hakimu amewahukumu hao wanajeshi kwa ushahidi wa mazingira,swali ni Je sio kesi zote za jinai zinatakiwa kuwa proven beyond reasonable doubts?
 
Hiv hawa masoldier kabla ya kuua walikuwa wanaendaga msikitin kwel,naona hukumu ya jana wamepigilia jez za msikitin wazee wa swala5,.hiv hii nikuurizisha umma wao wacha Mungu au ndo uzaifu ule binadam kujifanya wa Mungu akiwa kwenye mikasa...
 
hanging-noose-mdn.jpg


na Happiness Katabazi na Betty Kangonga


HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa askari wawili wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mmoja wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kumuua kwa kusudia, Swetu Fundikira.
Askari hao MT 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa JKT, Kikosi cha Mbweni, MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ, Kikosi cha Kunduchi na MT 85067 Koplo Mohamed Rashid wa JKT Mbweni.
Washitakiwa hao walidaiwa kumpiga na hatimaye kumuua kwa makusudi Fundira Januari 23, majira ya saa 7:30 usiku wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia usiku wa kuamkia Januari 24 mwaka 2010, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.
Sweti Fundikira ni mtoto wa mdogo wa Mwanasiasa Maarufu nchini, marehemu Chifu Abdallah Fundikira.
Hukumu hiyo ambayo inaweza kukomesha vitendo vya askari kujichukulia sheria mkononi dhidi ya raia, ilitolewa jana na Jaji Zainabu Muruke.
Jaji Muruke alisema baada ya kusikiliza kesi hiyo, ameridhika na ushahidi uliotolewa na mawakili wa upande wa Serikali ambao ulidai kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo la mauji kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Akisoma hukumu hiyo iliyovuta hisia za wengi mahakamani hapo, Jaji Muruke alisema ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonesha washtakiwa hao kuwa ndiyo waliomua marehemu (Fundikira), ushahidi mazingira unaonesha pasipo shaka walihusika na mauaji hayo.
“Sheria ipo wazi na inaanisha kuwa ukiondoka au ukionekana na mtu kwa mara ya mwisho na baadaye mtu huyo uliyeondoka naye akapata madhara au amekutwa amekufa, wewe uliyeondoka naye ndiyo utawajibika kisheria na madhara yaliyompata mtu huyo;
“Japo kuwa ushahidi uliotumiwa na upande wa mashitaka katika kesi hii ni wa mazingira, lakini umeweza kuthibitisha kesi yao, upande wa utetezi nao umeweza kutoa ushahidi wenye matundu mengi na unaokatika katika sana na ambao umeshindwa kuudhoofisha ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri dhidi ya washtakiwa, ’alisema jaji Mruke.
Aidha, alisema Jamhuri imeweza kuthibitisha kosa la mauaji, hivyo mahakama imewaona washtakiwa wote wana hatia ya kumuua Swetu Fundikira.
Hata hivyo, Jaji Muruke kabla ya kutoa adhabu hiyo alimpa nafasi wakili Karoli Muluge pamoja na washtakiwa kusema lolote kabla ya kuwapatia adhabu hiyo.
Wakili Muluge aliiomba Mahakama iwape adhabu ndogo kutokana na mazingira ya kesi hiyo, umri wa washtakiwa kwani bado ni vijana, nguvu kazi ya taifa na familia zao zinawategemea.
Naye mshtakiwa wa kwanza, Sajenti Robert aliiomba Mahakama impunguzie adhabu akidai kuwa mama yake ni mjane na anamtegemea, pia ana watoto wadogo.
Hata hivyo Jaji Muruke alilamuamuru mshtakiwa wa pili, Koplo Ngumbe kukaa chini baada kuanza kujitetea kuwa ametiwa hatiani kimakosa na anamwachia Mungu.
Kwa upande wake mshtakiwa wa tatu, Koplo Rashid aliiomba mahakama imuonee huruma na impunguzie adhabu akidai kuwa bado ni mdogo na hilo ni kosa lake la kwanza.
Akitoa adhabu, Jaji Muruke alisema ni kweli maombi ya mshtakiwa wa kwanza yanatia huruma na kwamba mshtakiwa wa tatu hata kumbukumbu zinaonesha bado ni mdogo, pia hilo ni kosa lake la kwanza, lakini alisema kuna roho iliyopotea.
“Sheria ipo wazi kabisa mshtakiwa yoyote anayepatikana na hatia adhabu yake ni moja tu ambayo ni kunyongwa hadi kufa na hakuna mbadala wa adhabu hiyo…hivyo mahakama hii kwa kauli moja inatamka kuwa washitakiwa wote wa tatu mahakama hii imewahukumu adhabu ya kifo hivyo, mtanyongwa hadi kufa,” alisema Jaji Muruke:
Baada ya kutoa adhabu hiyo Jaji Muruke alitoka katika chumba cha mahakama na ghafla ndugu wa marehemu Fundikira waliangua vilio ndani ya ukumbi wa mahakama, kama vile walikuwa msibani.
Ndugu wawili wa marehemu, Mwasiti Fundikira ambaye ni Dada wa marehemu na Shelina Hamisi (mpwa wa marehemu) walianguka chini na kuzirai kwa muda hali iliyowalazimu watumishi wa mahakama kuwapatia huduma ya kwanza kwa kuwapepea hadi waliporejea katika hali ya kawaida.
Mke wa marehemu, aliyejitambulisha kwa jina la Lucy ambaye aliachwa akiwa mjamzito, alisema hakuamini kama haki ingetendeka kwani mpendwa wao aliuwawa kinyama.
Hata hivyo wakili wa washitakiwa hao, Muluge alisema hakuridhika na hukumu hiyo na kwamba atakata rufaa.

 
Back
Top Bottom