WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira wahukumiwa kifo!

Yaani bado kusubiri hadi ikifika maana wanaweza kata rufaa wakitaka, then raisi anaweza wasamehe etc si unajua nchi yetu hii
Msamaha wa raisi hawezi kutoa msamaha kwa makosa ya mauaji ,ujambazi wa kutumia silaha na kesi za uhujumu uchumi!sheria za nchi zinakataza!
 
Katika kesi hii inasemekana kulikuwa na kihoja cha aina yake; Inabidi mfumo wetu wa sheria uangalie upya suala zima la kuwatumia wazee wa baraza kama hawa, ambao hali zao tu zinaonyesha wako katika mazingira rahisi mno ya kuhongwa na kupindisha ukweli.

Na ikiwa hakimu mwishowe hazingatii ushauri wao, kuna haja gani ya kuwa na wazee wa baraza?

Jana katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam wazee wa baraza katika kesi ya Swetu Fundikira waliushangaza umma uliohudhuria kesi hiyo (nafikiri hata na ndugu wa washtakiwa hawakutegemea kile walichosikia) baada ya wote watatu kudai kuwa washtakiwa waachiwe huru kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa wao walimuua Swetu Fundikira. Aliyetoa kali kabisa ni Mzee Raha Saidi aliyedai polisi wamewabambikia kesi washtakiwa ki ujanja ujanja. Mzee mwingine Ali Kampea alidai kifo cha marehemu ni ajali tu kwani alianguka ndipo akaumia kichwani na kupeleka kifo chake. Bibi Johari yeye alidai kuwa yeye haoni kama washtakiwa walikuwa na nia mbaya na hatimaye kumuua Swetu Fundikira bali washtakiwa ni watu wazuri na nia yao ilikuwa ni kumpeleka polisi tu na si vinginevyo hivyo yeye anaona hawana hatia.
SAM_3574.JPG


Kuna bahasha mezani hapo kwa wazee! Halafu hawa si kamati ya ufundi ya Mahakama. Kwa hiyo siyo rahisi kuondolewa mkuu
 
Je, Hawa wazee wanaelewa kiingereza fasaha kwani ndio lugha ya mahakama ingawa mimi sio muumini wa kutumia lugha ya kikoloni kama haikufungi na bila sababu za msingi.
 
Jamani jamani, hivi ni lini Tanzania tutakuwa serious japo kidogo tu kwa mambo nyeti?
Yaani hao wazee ukiwaangalia tu sura zao, ukaja kwenye majina yao..... naomba nisitie neno.
..Mzee Raha Said
..Bibi Johari
..Ali Kampea...
Aisee..mie simo...
 
Hapa panahitaji uchunguzi mpana:
  • Wazee wa CHADEMA
  • Wazee wa kanisa
  • Baraza la Walei
  • Wazee wa Moshi
Mkuu hawa huwezi kuwaona kwenye public kwani wanafanya kazi ndani ya taasisi zao tu, lakini wale wengine wanaotokea ktk public ndio ninaohoji, kwa nini wavae vile?
 
Du na mimi natamani ningekuwa mtoto wa kiongozi au hata mtoto mpigania uhuru plus na akili yangu nakuapia nisingekuwa hapa nilipo, lakini Mungu ni mwema huwezi kujua kwa nini Mungu akanifanya hivi nilivo.So back to the topic nasema na ntasema kweli kwamba kwanza angekuwa alieuawa ni mlalahao wa Tandika ama mlalahoi wa Buguruni kwa Mnyamani kesi hii ingesikilizwa miaka 12 ama watuhumiwa kwa kuwa walikuwa ni watumishi wa serikali wangekuwa wameshatolewa zamani maana wangekuwa waliua bila kukusudia sasa kwa kuwa ni mtoto wa Fundikira ni haki bin haki
 
Mimi nadhani kwenye utaratibu wa wazee wa baraza kama ipo haja basi utumike utaratibu wa daftari la wapiga kura. Yaani inakuwa zamu ya mtu kuwa mzee wa baraza kwa kipindi cha mwaka mmmoja, kama hapatikani basi mtu anayefuata hadi wa mwisho. Mtu ikiwa zamu yake kama huna rekodi ya uhalifu au kitu kingine cha kukufanya uwe mzee wa baraza katika kesi basi unachaguliwa. Unaweza kugawa daftari kwa jinsia lakini si kwa namna nyingine yeyote. Kisha unawapa semina ya muda mfupi wanakuwa wanasikiliza. Ndio utaratibu unaotumika Marekani kuteua jury, tena inasomwa hadharani na unajua nani ni jury. Unasikiliza kesi moja tu sio zote kwa mwaka katika mahakama husika. Kama huu utaratibu haufai basi na tufute wazee wa baraza hawana tija naona hapo hata kuandika ni shida sijui nadhani ni mazoea na nadhani wameambiwa wewe kila kitu kataa
 
kumbe inawezekana ktk mahakama zetu sasa tunaomba wafanye hivyo hivyo kwenye kesi za UFISADI
 
watanzania kwa kusahau tuko juu sana mbona kesi zipo nyingi sana hajiulizi hata kwa nini kesi imeendeshwa haraka sana na kutolewa hukumu tena kali sana ya kifo. ccm kwa kufoji mko juu sana maana hata hili nikwakuwa anauhusiano na Fundikira angekuwa aliyeuwawa ni mtoto wa kabwera ingeyeyushwa tu na mwisho wake anapewa miaka 2 au hata kulipa hela ya nyanya. Angalieni kesi ya Chenge aliua alilipa nini? kuweni makini na viini macho
 
Msamaha wa raisi hawezi kutoa msamaha kwa makosa ya mauaji ,ujambazi wa kutumia silaha na kesi za uhujumu uchumi!sheria za nchi zinakataza!

aliyekuambia rais hawezi toa msamaha kwa makosa ya mauaji ni nani -waliomuua kombe hujui kuwa wako uraiani sasa na walitoka kwa msamaha wa rais
 
Hivi hukumu ya Kifo Tanzania ipo? na katika historia ya nchi hii ni wangapi waliohukumiwaga kifo??

Mkuu Ndallo wako wengi sana labda suala ni utekelezwaji wa hukumu yenyewe. Kuna wengi ambao hukumu zao hazikutekelezwa na kuachwa wakiwa magerezani tu wakisubiri utekelezaji hadi wakajifia wenyewe. Kuna wengine ambao hukumu zao zilibadilishwa na kuwa vifungo vya maisha.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom