Mfungwa Sajini Rhoda Robert aliyemwua mtoto wa Fundikira amefariki dunia akisubiri kunyongwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
Rhoda%20Robert-July5-2014-ee.jpg


Mfungwa aliyemuua mtoto wa Fundikira afariki dunia




  • [*=left]Ni askari wa JKT aliyekuwa akisubiri adhabu ya kunyongwa

    [*=left]Azikwa na Magereza kwa mujibu wa sheria badala ya ndugu

Mfungwa Sajini Rhoda Robert aliyekuwa anasubiri adhabu ya kunyongwa kwa kosa la kumuua mtoto wa kigogo Swetu Fundikira, amefariki dunia wakati akitibiwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma, kufuatia hali yake kubadilika kutokana na kuishiwa damu mwilini.

Rhoda aliyekuwa askari wa kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mbweni na wenzake Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashid, walihukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Zainabu Muruke Novemba 20, 2012.

Hadi mauti yanamkuta, Jaji Muruke aliyesikiliza na kutoa hukumu ya kesi hiyo alikuwa hajasaini hukumu hiyo na kuwafanya wafungwa hao kushindwa kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu hiyo.

Mapema mwaka huu wakili wa wafungwa hao, Kaloli Muruge, aliiambia NIPASHE kuwa aliwasilisha kusudio la kukata rufaa lakini kikwazo ilikuwa ni nakala ya hukumu ambayo jaji alikuwa hajaisaini.

Habari za kuaminika kutoka Gereza la Isanga mkoani Dodoma ambapo mfungwa huyo alikuwa akisubiri kunyongwa, zilisema kuwa Sajenti Rhoda alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo akisumbuliwa na maradhi.

Alisema hali ya mfungwa huyo ilibadilika na kufariki dunia akiwa hospitalini hapo.

"Alizikwa gerezani kwa sababu alikuwa ni mfungwa ambaye kisheria hairuhusiwi kuzikwa uraiani lakini mwishoni mwa wiki ndugu zake waliarifiwa kuhusu kifo chake kabla ya mazishi na walifika na kuonyeshwa kaburi lilipo," kilieleza chanzo chetu cha habari.

NIPASHE ilizungumza na Mkuu wa Gereza la Isanga, Makoti Mwaibale, ambaye alithibitisha kufariki kwa mfungwa huyo. Alisema mfungwa huyo alifariki dunia Juni 20, mwaka huu katika hospitali hiyo akiwa anapatiwa matibabu.

Alisema Rhoda aliumwa na kupelekwa hospitalini Juni 15, mwaka huu ambapo alilazwa huku akiendelea na matibabu kwani ugonjwa uliokuwa unamkabili ulimsababishia kupungua kwa damu.

"Ugonjwa wa mtu ni siri hivyo alikuwa akiongezewa damu na ilipofika Juni 20 majira ya saa 1 asubuhi alifariki dunia," alisema. Mwaibale alisema mfungwa huyo alizikwa siku hiyo katika makaburi ya wafungwa yaliyopo Dodoma.

Alisema mume wa marehemu pamoja na mjomba wake walitaka kuuchukua mwili huo kwa ajili ya mazishi lakini haikuwezekana kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, alisema kwa mfungwa ambaye amehukumiwa kunyongwa hadi kufa akifariki anazikwa na magereza lakini angekuwa ni mahabusu wa kawaida mwili huo ungekabidhiwa kwa ndugu zake.

Alisema ndugu wa marehemu hawakushirikishwa katika mazishi kwa kuwa kuna sheria zinazowaongoza katika jambo hilo.Mwaibale alisema ndugu zake akiwamo mume wake walifika Juni 22, na kuonyeshwa kaburi la mfungwa huyo lilipo.

Hukumu ya askari hao ilisomwa na Jaji Muruke alisema ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa washtakiwa hao ndiyo waliomuua Fundikira, ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka (Jamhuri) ulikuwa ni ushahidi wa mazingira, kwamba Jamhuri imeweza kuthibitisha mashtaka hayo.

Alisema kuwa anakubaliana na mtiririko wa ushahidi wa upande wa mashtaka kama ulivyoelezwa na mashahidi wake sita akiwemo daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu pamoja na askari polisi wawili ambao washtakiwa katika utetezi wao walishindwa kuuvunja.

"Sheria iko wazi ukiondoka na mtu au ukionekana naye kwa mara ya mwisho na baadaye mtu huyo akapatikana na madhara, wewe ndiyo unawajibika kutoa maelezo ya kina kuhusu yaliyompata mtu huyo," alisema Jaji Muruke na kuongeza;

"Kisheria ukitoa maelezo ambayo hayajakidhi haja na yana utata ni faida kwa upande wa mashtaka ambao hutegemea ushahidi wa mazingira. Maelezo ya kina hayajatolewa na washtakiwa wote."

Aliendelea, "Ushahidi wa Jamhuri japokuwa ni wa mazingira, umejengwa thabiti na upande wa utetezi haukuweza kujenga matundu, ama kuuvunja mnyororo huo, kidole kinawaelekea wao."

Jaji Muruke alisisitiza kuwa katika kesi hiyo licha ya kuwa kuna ushahidi wa kimazingira, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka.

Sajini Roda na Koplo Mohamed Rashid wote wa JKT Mbweni na Koplo Ally Ngumbe (37) wa Kikosi cha JWTZ Kunduchi, walimpiga Fundikira, Januari 23 mwaka huu saa 7:30 usiku wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na baadaye kufariki dunia usiku huohuo wa kuamkia Januari 24, mwaka 2010, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Chanzo: Nipashe
 
mbona ni kama alizikwa haraka haraka!. Haraka za nini wakati huyu alikua ni mkristo? Ndugu si ilifaa waonyeshwe mwili na si kaburi?.
 
Kawaida familia huletewa taarifa ya maandishi ya kifo cha mfungwa ambaye ni ndugu yao.Utaonyeshwa kaburi na kupewa nguo na vitu alivyoingia navyo marehemu.
Muhusika ni yule aliyetambulishwa na marehemu wakati wa kuingia magereza.
 
Kuna utata hapa iweje familia ionyeshwe kaburi tarehe 22 na wasionyeshwe mwili tar iyo aliyokufa au kabla hajazikwa mmmh sina hakika na ichi kifo.

Labda wanasheria watujulishe kuhusu ukweli wa suala hili, maana kawaida mfungwa anapofariki ndugu na jamaa huarifiwa ili washiriki kikamilifu maziko yake hata kama yanafanyika katika himaya ya wafungwa, hali kadhalika kama ni mwumini huwa viongozi wa kiimani waitwe kama alikuwa active katika imani yake.

Pamoja na kwamba alikuwa akisubiria adhabu ya kunyongwa, kawaida baada ya adhabu hiyo maiti huonwa na kuagwa na ndugu za marehemu, hii ya kuvukia haraka haraka bila kushirikisha ndugu na jamaa kuna siri nzito inayohitaji kufanyiiwa utafiti wa kutosha kama ndugu wa marehemu wako makini.
 
Huyo alikua mfungwa... Nadhani taratibu za magereza ziko tofauti

Taratibu za magereza ndio kutoruhusu ndugu kuona na kuuaga mwili wa hayati ndugu yao na kutoshirikia maziko yake? Taratibu za magereza zinafanyamaziko kwa siri na sijui kiongozi wa hayari kiroho aliitwa kumwombea dua ya RIP?
 
Sheria ya wafungwa kifungu cha 73:
73.-(1) On the death of any person detained in a prison the officer in-
charge shall cause immediate notice of such death to be given to the
medical officer.
(2) The medical officer, on receipt ofthe notice, shall cause the dead
prisoner to be medically examined in a manner he considers necessary
and shall issue a certificate stating the cause ofthe death and shall
c a u s e such certificate to be delivered to the n e a r e s t coroner.
(3) The coroner shall report to the Commissioner the result ofthe
inquest held.
(4) The Commissioner shall also cause an inquiry to be held as to
any death in any prison from Other than natural c a u s e s , and report
thereon to the Minister.
 
Sheria ya wafungwa kifungu cha 73:
73.-(1) On the death of any person detained in a prison the officer in-
charge shall cause immediate notice of such death to be given to the
medical officer.
(2) The medical officer, on receipt ofthe notice, shall cause the dead
prisoner to be medically examined in a manner he considers necessary
and shall issue a certificate stating the cause ofthe death and shall
c a u s e such certificate to be delivered to the n e a r e s t coroner.
(3) The coroner shall report to the Commissioner the result ofthe
inquest held.
(4) The Commissioner shall also cause an inquiry to be held as to
any death in any prison from Other than natural c a u s e s , and report
thereon to the Minister.

Asante mwanasheria kutufungua akili. Je, jeshi la Magereza lina uhalali wa kuzika bila ndugu kushirikishwa? Katika kesi hii pamoja na ndugu kutoshirikishwa na maziko kufanyka haraka kuna dalili ya vipengere ulivyoainisha hapo juu kutofutwa kwa muda mfupi.
 
mmh!,hii ni ngumu "kumeza".i can smell some fishy busness behind this news.
 
Nina wasi wasi sana na hukumu hii ya Jaji Muruke iliyooegemea ushahidi wa mazingira na sio ushahidi usiokuwa na shaka, pia kwa nini hakutoa copy na kutia saini ile hukumu yake ili watu hawa wakate rufaa kwa wakati muafaka???...sasa ona kafa kabla ya kukata rufaa kwa uzembe wa Jaji Muruke
 
Back
Top Bottom