Watu wote mliojiua nikawasema vibaya naomba mnisamehe sana

Watu wote mliojiua nikawasema vibaya naomba mnisamehe sana

Mpaka sasa mleta mada unahisi huwezi pata msaada. Yaani unaulizwa tatizo nini husemi. Ushaamua kabisa kuwa hakuna msaada tena, sasa kwanza funguka kisha watu wenye ubinadamu wakusaidie kadri ya inavowezekana.
 
1. Kuna mikataba /maagano yoyote uliingia pasipo kujua mwisho wake na sasa huoni pa kutokea zaidi ya kujiua?

2. Kuna watu/ viumbe wa aina yoyote ile wanakuzonga wakihitaji uwatumikie na huoni namna ya kuepukana nao zaidi ya kujiua?

3. Uliwahi kushiriki umwagaji damu kwa namna yoyote ile na kwa sasa damu hiyo inakuandama hivyo umeshindwa kabisa kuikwepa?

Ninafikiri shida yako ipo kwenye kundi moja kati ya hayo niliyotaja. Hizo ni miongoni mwa changamoto ambazo ni ngumu sana kuziweka wazi!

Usiogope! Zinatatulika..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna fungu moja hujalitaja na hili hutupelekesha sana mara liingiapo katika njia ya mhusika.
Kuwa na deni kubwa wala huna mwanga ulipaji, hapo ikiambatana na kesi ya Jinai ambayo hujui hata mwanga wake unapatikana wapi!!
 
Acha kujipa matumaini yasio na msingi,huyo Mungu alisha msaidia nani?
Mbona wote wanashida?hz faraja zako nizakijinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikijaribu kukufkria ndugu naona kabisa kuwa ww ni mmoja ya watu waliopoteza matumaini. Labda tu nikukumbushe jambo juu ya hii comment yako ili ujue Mungu hafanyiwi dhihaka.

Nadhani kuna historia za baadhi ya watu Duniani waliowai kuongea ujinga kama wako then yaliyowakuta yamebaki historia na funzo kwa wengne, km ujawasikia basi ni hawa

1. Mtengenezaji wa meli ya titanic: mwenzio aliojiwa vp juu ya uimara wa meli akasema hata Mungu mwenyewe hawezi kuizamisha. Nadhani wote tunajua nn kilitokea

2. Mpuuzi mwingine Azuza (mwanamuziki) huyu alikuwa mbrazil, cku yupo jukwaan kwenye show akawasha fegi anavuta then kawasha nyingine kairusha juu anasema hiyo yako Mungu vuta, nadhani pia tunajua kilichomtokea km ujui itafute history yake

3. Bwege mwingine John lennon (the beatles member): yupo front af camera anajigamba "ooh kundi letu maarufu kuliko Jesus... Mara ukristo utapotea duniani", hajachukua days nyingi akafa. Af leo kuna bwege flan(lil wayne) anaimba eti "if i die today remember me like John lennon" sasa cjui kivp akumbukwe maybe huwa wanaimba wakina tayari wapo high kichwani

4. Christine hewt: Huyu mama alikuwa mwandishi, nae cku karopoka "nimesoma vitabu vingi duniani ila cjaona kitabu kibaya km Bible" nae akuchukua round nyng

5. Tancredo: Hiki kilikua moja ya vyuma vilivyowai kushinda urais kwa kishindo huko Brazil, na huo ushindi wake ulikuwa hivyo baada ya maneno yake aliyotoa kuwa "km nikishinda urais kwa kura 500k basi hata Mungu hawezi kunitoa kwenye kiti cha urais", unadhani nn kilifata....


Sasa me nkwambie tu ndugu yangu, usione fahari kutoa comment ya hivyo ukidhani eti unafurahisha watu au kutaka watu wa comment kukutukana no! Na ndo mana kila mtu kapita pemben wala haja deal na ww. Km huwa unasoma vitabu basi tafuta kitabu kinaitwa "CHANGE YOUR THINKING CHANGE YOUR LIFE" ila mwandishi kdg nmemsahau maana nilisoma mda kdg, hicho kitakufunua na kukubadilisha ktk hiyo hali uliyonayo.

#munguakusaidie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una umri gani mkuu! Tatizo kubwa nini?
Pesa ya kula?
Malazi?
Ni kipi kina kusumbua zaidi sema juwe tuanzie wap!
 
Ndugu yangu mateso niliyo nayo ni Makubwa sana

Nimemutumaini Mungu bila msaada nimechoka bora nife tu mimi

Machozi yananitoka mimi nimekuwa ni Mtu shida miaka yote sijapenda kuwa mjinga wa kwenda kwa waganga

Nimemutumania Mungu lakin wapi

Kama Mungu kaweka agano na shetan niingie kwenye kikombe hiki bas nimechoka Mungu atafute mwingine naomba kikombe hiki kiondoke kwangu ila siyo kwa Mapenzi yangu bali kwa mapenzi yake Mungu mwenyewe



Sent using Jamii Forums mobile app
Nitumie namba ya mkeo inbox ili nikusaidie kulea watoto ukijiua.

USHAURI KWA WENGINE:
Ukiwa na changamoto yoyote ya kimaisha iweke wazi hata humu jf kuna watu vichwa wengi sana watakusaidia kuliko kujiua.

Hiyo unayoiita changamoto kubwa wapo watu waliipitia na wakaishinda. Kuwa muwazi...Shida nini?
Huna ajira?
Mkeo anachepuka?
Umefukuzwa kazi?
Umeambukizwa H.I.V? n.k

Sema ili wadau tukushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani tusifanye mchezo huyu mtu naona kadhamilia kwerikweri...
 
Ndugu yangu mateso niliyo nayo ni Makubwa sana

Nimemutumaini Mungu bila msaada nimechoka bora nife tu mimi

Machozi yananitoka mimi nimekuwa ni Mtu shida miaka yote sijapenda kuwa mjinga wa kwenda kwa waganga

Nimemutumania Mungu lakin wapi

Kama Mungu kaweka agano na shetan niingie kwenye kikombe hiki bas nimechoka Mungu atafute mwingine naomba kikombe hiki kiondoke kwangu ila siyo kwa Mapenzi yangu bali kwa mapenzi yake Mungu mwenyewe



Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuelewa sana kaka na ninajua kuna watu humu hawatokuelewa maana hawajawahi fika point uliyofikia. Niamini nimekuelewa

Nilikuwa katika point kama yako last year, nilijihisi nimeshindwa, nilijihisi nimekwisha, nilihisi maisha yangu hayana thamani maana nikiangalia pembeni yangu sikuona uchafu mkubwa niliowahi kutenda hadi niwekewe maisha mitihani kila uchao. Niliangalia walio pembeni yangu na kufanya kila machukizo lakini wanainjoi maisha yao kuliko mimi. Iliniuma

Kitu kilichonila zaidi siku zote ni kujiliuza WHY ME!!!. Ni nini nimemkosea Mungu wangu au kwa nini nastahili yote haya. Kwani toka kuzaliwa kwangu sijawahi kupumzika. Nililia machozi yakaisha, ujasiri wa kujiua sina na nikaomba Mungu anipe kifo na hakikutokea. Sikuwa na maana ya maisha

Kilichofuatia nilifungua uzi jf na ID nyingine. Niliconfess asilimia kama 40 ya vitu vyote. Nilitukanwa, nilidhihakiwa lakini mwisho wa siku nilipata watu baadhi waliosaidia kunivusha.
Wengi walikuja na kuondoka na kuna time nabaki peke yangu bila mtu wa kuongea nae lakini nimejifunza kulia na kupigania nafsi yangu inapowezekana.

Hujashindwa kaka, umefika point ambayo umeshindwa tu kuhimili shida zako ila hiyo point haikai daima. Utaipita kwa ujasiri na utaweza, usife moyo, usijihisi hauna maana ya kuishi. Bado upo hai, bado una chance ya kuendelea.
Please kaka usijikatie tamaa, nilipita ulipopita na bado nipo hai. Usishindwe kaka
 
acha uoga wa maisha.
KUJIUA SIO KITENDO CHA KIUME.
unatakiwa upambane mpaka mwisho.
Wenye matatizo tupo wengi hata mimi nina matatizo makubwa.lakini uwa si semi kwa watu.
Na komaa nayo na KUPAMBANA KIUME.
kwa hyo acha kulia lia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tiba ya kwanza ni wewe kusema wazi kipi kinakusumbua, kupitia hapo utaweza kupata tiba zingine kutokana na tatizo unalopitia.

Hata wanaosali sana lazima wamwambie Mungu ni shida gani inawakabili, then kwa imani wanakaa wakisubiri Mungu amewasikia na atatenda.

Wale wanaoenda kwa wanasaikolojia pia lazima waseme nini shida, kuanzia hapo wanaanza healing process. Bado hujachelewa, sema hapa shida yako iwe KIUCHUMI(hapa haswa ndipo wengi tulipo) au KIJAMII.
 
basi nchi yetu mtu kama huyu yuko suicidal kabisaa..this is crying for help, and nothing is going to be done..*sad**....Mkuu share matatizo yako..labda utapata msaada..inawezekana kuna wanaopitia au waliopitia unayopitia hivyo wanaweza kuwa msaada kwako..please share
 
Back
Top Bottom