Watu wote mliojiua nikawasema vibaya naomba mnisamehe sana

Watu wote mliojiua nikawasema vibaya naomba mnisamehe sana

Anahitaji mchongo wa kumpatia mkate na siyo maushauri ya counselling yenu
Unadhani mchongo utakuja na stress alizonazo bila kushauriwa?Yeye amewaza amefika kikomo ndiyo maana anatafuta msaada (ushauri)
 
kama hana tatizo la kiafya basi uchumi utakuwa umeyumba, bila shaka hapa mdau tatizo kubwa ni kuyumba kiuchumi.
wengi tumeyumba kipindi hiki, ila hatukati tamaa na bado tuna sura zimejaa bashasha ila ndani tunamaumivu mengi
 
Mayala B, Always give yourself a second chance, mawazo kama haya huja na kupita but you never know what tommorow will bring, wapo watu wengi wenye matatizo ya kila aina wanavumilia, kumbuka ni wangapi walio karibu yako wanakupenda, kwanini unataka kuwaumiza roho zao kwa hatua unayotaka kuichukua?

Maisha ni fumbo, muhimu ni kutokata tamaa, leo unaweza kujiona hauna maana duniani kwasababu umekosa unachokitaka, but unaweza kukipata kesho ukasahau haya yote unayotaka kufanya leo.

Usipende sana kuwaza jambo moja muda mrefu, tafuta kitu unachopenda kukifanya kama kuangalia/kucheza mpira, movies, and so on huku ukiendelea kuamini siku yako inakuja, amini hakuna aliyezaliwa kuteseka tu hapa duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni lazima ujuwe kuwa kujitoa roho yako ni dhambi,kukata tamaa na maisha ni dhambi,na ukishajiua kaa ukijua kuwa utaenda motoni direct,sasa kama umeamua kwenda jehanamu tunaktakia kila lakheri,maana maisha ni choice kuchagua kuishi au kufa...
 
Mayala B, Shida nn Mkuu?? Inawezekana kabisa kabisa hapo ulipo, humu JF kuna mwingine alikutwa na majanga ya aina yako tena ye alikuzidi ,..lkn kuna njia fulan fulan alizitumia kuweka kujinasua, nahatimae Leo ni MTU miongon kwa kwa watu wenye Amani.


Embu shuka hapa, tatizo nn, ILI upate suluhisho sawa na hitaji lako.



NB...Usithubutu na usije kukaa na jambo moyoni linalokutesa ( unajiua Mdogo mdogo).
 
Usifike huko please, kifo sio suluhu na wale wote waliojiua pia wanatamani wasingejiua, ndio maana ukimuokoa mtu anayetaka kunywa sumu au aliejinyonga ukikata ile kamba huwa anashukuru sana na hatorudia tena... Jipe moyo utashinda
Sio kweli kuna dingi mmoja huku tulimnusuru mara mbili, mara ya tatu akanywa sumu ya kuulia wadudu shambani akadanja!KIFO kikikuita hata usipoitika utakwenda tu!no way
 
Unaishi mkoa gani mkuu? Km ni Dar si vibaya tukawasiliana

Kwa bahati nzuri mleta mada anatambua asili ya uwepo wetu hapa duniani. Umeongea vizuri sana kuhusu uhusiano wetu sisi binadamu na Mungu. Hakuna mtu aliyekuja duniani kwa kubahatisha tu. Kila mtu aliletwa kwa mpango maalumu wa Mwenyezi Mungu. Kumbuka Mungu alitujuwa kabla hata hatujazaliwa (kabla hata ya kutungwa kwa mimba zetu), kama angekuona hauna thamani kwake si angekuangamiza kabla hata ya kukuleta duniani? Binadamu tuna thamani kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu; na ndio maana alituumba kwa mfano wake.

Matatizo na shida za hapa na pale tunazopitia hapa duniani ni miongoni mwa mapito tunayoyakiwa kupitia kwa makusudi maalumu aliyoweka Mungu. Sisi, kama binadamu tulioumbwa kwa mwili tunaona hatukustahili kupitia mapito hayo (kwa kuwa mwili ni dhaifu), lakini binadamu hakamilishwi na mwili pekee, bali hukamilishwa na mwili na roho. Kwa bahati mbaya, tunapokutana na majaribu haya, tunaupa nafasi mwili tu na kusahau kuwa tuna roho pia. Mchimba dhahabu huijaribu dhahabu yake kwa kuichoma kwenye moto kuona uhalisia wake, vivyo hivyo Mungu hutujaribu binadamu kama tupo upande wake kwa majaribu mbalimbali ili kuona kama tunahimili.

Ayubu alikuwa tajiri na mwenye mafanikio makubwa. Alikuwa na mali nyingi na watoto wazuri, alikuwa mcha Mungu. Lakini Mungu alimjaribu kwa kumruhusu shetani kwenda kuharibu kila kitu cha Ayubu isipokuwa roho yake tu. Shetani alianza kuharibu mali zote za Ayubu, akaua watoto wote na mwishowe akaharibu mwili wa Ayubu kwa kumpa madonda mwili mzima. Ayubu alilala chini akijiuguza kwa muda mrefu, lakini kwa muda wote huo hakumwacha Mungu. Na baadaye Mwenyezi Mungu alimponya na kumrudishia utajiri wake maradufu. Kwa hiyo ndugu yangu, hayo ni mapito tu, usikate tamaa, iko siku yatakwisha. Uwe na amani.
 
Jamani mwenzetu anahitaji msaada wetu wa faraja na mawazo...tafadhali tusipuuzie.
Kuna tuliowapuuzia waliugua tukajua matapeli wengine wanashida wakileta humu tunawakejeli leo hii hawapo na zipo threads za kudhibitisha hilo tunabaki kusikitika.
Ndugu Mayala B tafuta mtu humu JF unaeona ana hekima na utakua comfortable kumueleza kinachokusibu. Inawezekana unapoishi huoni wa kumshirikisha ndo maana ukalileta humu.
Elli Rebecca 83 Zero IQ bowlibo nanilii client 3 Maiti Gyole Carlos The Jackal this guy needs us maybe not financially but someone to talk to. Let's reach out to him asijifanye kitu kibaya. Naumia mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu bora nikafungwe jela maisha kuliko maisha haya ninayopitia

Hujui tu ndugu yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
narudia tena alichosema Carlos

Shida nn Mkuu?? Inawezekana kabisa kabisa hapo ulipo, humu JF kuna mwingine alikutwa na majanga ya aina yako tena ye alikuzidi ,..lkn kuna njia fulan fulan alizitumia kuweka kujinasua, nahatimae Leo ni MTU miongon kwa kwa watu wenye Amani.


Embu shuka hapa, tatizo nn, ILI upate suluhisho sawa na hitaji lako.



NB...Usithubutu na usije kukaa na jambo moyoni linalokutesa ( unajiua Mdogo mdogo).
 
Comet,
'Mtu ajaribiwapo asiseme kuwa anajaribiwa na Mungu. Kwani Mungu hawezi kumjaribu mtu na wala Mungu hawezi kujaribiwa na Shetani". Hili andiko lipo ktk kitabu Cha Yakobo nimesahau mstari.
Pia tukumbuke kuwa mtawala wa Dunia hii ni Shetani, tunapaswa kumuomba Mungu kwa bidii ili atuokoe na mateso ya mtawala wa Dunia hii Shetani.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom