Kosa lako, unafikiri waislam hatufundishwi hayo.
kama kuna mambo yamesisitiziwa katika uislam ni kufanya ihsani (neon la Kiswahili hisani)
unaanzia kwa wazazi wako wawili, waislam wenzako, jirani zako (jirani mkristo unapaswa kumtendea mema kuliko muislam wa mbali), hata wanyama.
lakini kama utachunguza jinsi Ramadhani ilivyo, ule ndio mwezi mmoja waislam wengi wanareflect mafundisho ya dini yao. jamii za kiislam zinapaswa ku-behave kama uonavyo wakati wa ramadhani na Eid, pungufu ya hapo ni changamoto za kibinadamu, na kwa kuwa waumini wa kweli si wengi kama sisi wenye majina ya seifu na juma wengi mnadhani kuwa sisi ni wakatili.
Eid zote symbol nambari 1 ni kutoa na kuhakikisha hakuna muislam anaona siku hiyo ni mbaya kwa kuwa amepungukiwa na mali.