hakuna ana
Nadhani hakuna anayeweza kukubishia kwa kuwa ni personal experience.
unaweza ukawa na shida au ni kweli jamii yako inaweza kuwa na shida, hakuna anayeweza kutoa comments sahihi hapa kwa sababu hujaelezea kwa kina umekutana na changamoto zipi.
labda tuchokoze ufunguke na hii iwe kwa faida yetu sote.
- uislam una taratibu zake na unajieleza vema kuliko dini nyingine katika maisha ya kijamii(nitafafanua) na kwa maana hiyo kabla ya kufanya jambo na waislam unapaswa kuhakikisha kuwa jambo hilo lina fatwa za kidin?
- ufafanuzi juu ya taratibu za kiislam. ktk dini yetu mambo mengi ya kijamii yameainishwa katika kitabu chetu kitukufu (Qur-an) na labda kupatiwa ufafanuzi Zaidi ktk hadithi na maamuzi mengine ya Islamic scholars wakubwa lakini basically concepts nyingi za maisha zimeainishwa kabisa katika Qur-an tukufu. masuala kama kuanza biashara kwa mkopo wenye riba, haliwezi kuwa jambo la kiislam, pia katika upatikanaji wa faida, kuna uharamu kuset faida maradufu ya ulichowekeza. vitu kama kuzidisha mizani ( hapa ina maanisha kuharibu kipimo halisi cha bidhaa iwe uzito au ujazo lakini hata kutoa false adverts ktk quality ya malighafi unayouza ni kosa kisheria).
- Kuna biashara zinazompendeza Allah na zipo ambazo ni haramu kujihusisha, mfano uuzwaji wa vilevi aina zote, kuwa na kumbi za starehe, kuwekeza katika jambo lolote lenye uharamu au mashaka juu ya uhalali wake si miongoni mwa biashara wafanayazo waislam.
- NOTE: mimi si mjuzi wa elimu ya dini kwa kiasi kikubwa. sio ninayoyasema hapa yote kuwa ni sahihi 100%, kama wapo wenye uelewa Zaidi watujuze wote.
- sehemu nyingine ni roles zao katika hizo biashara zako. kiashiria cha awali hapa ni kuwa wewe ndiye mwenye ideas na ni biashara yako, ndio maana the same business wanayoishindwa waislam unaihamishia kwa wakristo. kwao hamfanyi biashara bali wewe unataka kufanya kama unawasaidia au labda unataka kuwatumia kutimiza mambo yako. mfano upo wakati watu walitumia taasisi za kiroho kukwepea kodi, wapo walionunua jina la taasisi za kiroho kwa biashara binafsi etc.
- hali ya kiuchumi ya washirika wako wa kiislam huenda iko duni, au elimu yao iko chini au kinyume chake (wewe ukawa chini) katika mazingira kama hayo ni ngumu kujenga trust za kibiashara lkwa kuwa hamuongei lugha moja. lakini pia uwezo wako wa kitaaluma juu ya dini yako unaweza kuwa ni changamoto, labda una mingle na waislam ambao kitaaluma mko tofauti sana (kama ile elimu ya shule tu) kwa hiyo mkiongea jamaa wanakuwa na mashaka juu ya ucha MUNGU WAKO katika biashara, kumbuka wao watakuwa wanatazama dynamics zote za kibiashara kwa kadri ya maamrisho ya dini yao.
swali, nini msingi/dhamira kuu ya post yako?
hoja yako ni nzuri kama sehemu muhimu ya mijadala ya kiimani ambapo kama itachukuliwa vizuri hakutakuwa na haja ya kukashifiana au kuzungumzia vibaya Imani za mwengine. lakini napenda kujua dhamira ya wewe kuleta uzi huu humu JF.