Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,233
- 12,740
Mtaalamu mmoja alisema kuwa afya ya binadamu ilianza kuzorota pale alipoanza kulima. Huu ni ukweli kabisa. Babu zetu walipokuwa wanaishi kwa kuwinda na kukusanya walikula kila aina ya chakula. Walikula matunda, majani ya miti, nyama, asali, mayai ya ndege, wadudu, mizizi, samaki nk nk. Watu hawa kila kitu walipata kwa kiasi. Hawakujua upungufu wowote mwilini.
Alipoanza kulima akawa analima mazao ya aina fulani tu. Labda mahindi na maharage. Matokeo yake mwaka mzima anakula ugali maharage. Labda abahatike kula kuku mara moja au mbili kwa mwaka. matokeo yake afya yake ikawa duni kabisa. Mtu anashiba vyema lakini afya yake sifuri. Hali hii inaendelea hadi leo huko vijijini. Ndiyo maana mikoa ya nyanda za juu kusini inaongoza kwa uzalishaji wa chakula lakini pia inaongoza kwa utapiamlo.
Wakati wetu huu wa kisasa vyakula aina mbalimbali vinapatikana kirahisi hasa mijini. Lakini hili nalo limeleta matatizo. Inadaiwa kuwa wakati wa kuwinda na kukusanya, nyama, vyakula vya sukari na chumvi vilikuwa vitu adimu sana. Inasemwa ndiyo maana binadamu akajenga tamaa kali ya vyakula vya mafuta, sukari na kiasi chumvi. Hivi leo hii vimekuja kumharibia kabisa afya yake.
Nyama, sukari na chumvi vinapatikana kwa wingi mno. Na kwa vile alishajenga tamaa kali ya viti hivyo sababu vilikuwa adimu kwake, anaanza kuvifakamia kwa fujo. Matokeo yake ni kuporomoka kabisa kwa afya yake. Matunda yamefanyiwa modifications ili yawe na sukari zaidi. Na matunda yenyewe ni ya ina chache sana. Leo mjini ukisema naenda kula matunda tikiti na ndizi ndiyo hasa utavikuta.
Leo tunaona wahadzabe na wasandawe wanaishi maisha primitive sana, lakini kwenye afya wametuacha mbali sana. Tuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwao kuhusu suala la lishe.