Azolla mkombozi wa wakulima na wafugaji nchini

Clark cian

Senior Member
Jul 3, 2021
153
139
UFUNGUZI
Kutokana na teknolojia ya uchanganyaji wa vyakula kukua kwa kasi na kutuletea vyakula vyenye uwiano sahihi, kwa namna moja ama nyingine baadhi ya wafugaji wamekuwa wakilazimika kutumia gharama nyingi katika upatikanaji wa vyakula hivyo kwa ajili ya mifugo yao;hivyo kusababisha baadhi ya wafugaji wenye vipato vyachini kutoweza kupata vyakula hivyo kwa kiwango stahiki na muda sahihi.
Hali hiyo imechochea afya za mifugo kuzorota kutokana na malisho ya vyakula vyenye uwiano wa virutubisho usio sahihi kwa mifugo yao, pia kupelekea uzalishaji kwa mifugo kuwa mdogo ukilinganisha na kawaida.
Hivyo basi kutokana na mhemko wa kufungua akili za watanzania na kubadilisha mfumo wa maisha uliopo Kwa sasa, pamoja na kupitia tafiti mbalimbali juu ya mimea mbalimbali na virutubisho vilivyopo ndani mwao;ugunduzi wa mmea wenye asili ya gugumaji unaofahamika kwa jina la AZOLLA umekuwa msaada mkubwa kwa wafugaji hasa wenye kipato cha chini kutokana na mmea huo kuwa na uwiano sahihi wa virutubisho muhimu kwenye makuzi na uzalishaji wa mifugo yetu na sio tu mifugo kama vile ngombe ,mbuzi ,kondoo ,kuku, nguruwe pia hata samaki

download.jpg


UTANGULIZI

Mmea wa azolla ni upi?
ni aina ya mmea wa kijani ambao hupendelea zaidi kustawi kwenye mazingiza ya maji.mmea mmoja kati ya mingi wenye uwiano sahihi wa virutubisho muhimu vinavyohitajika na mifugo yetu .
Mmea wenye sifa ya umbo dogo machachari ,rangi ya kijani inayovutia, mizizi mifupi inayoelea ndani ya maji, na mimea ambayo inaweza kuota eneo lolote ilimradi tu liwe na maji yaliyotuama .

View attachment 2671930


Muundo wa kiasili wa mmea wa azolla kikemikali ni upi?
Mmea wa azolla kiasili umeundwa na uwiano tofauti tofauti wa virutubisho ambavyo husaidia katika makuzi na uzalishaji wa wanyama wetu na huo uwiano ni kama ufuatao
Protini ghafi – asilimia 24 -30
mafuta ghafi – asilimia 3.3-3.6
Nitrojeni- asilimia 4-5
Phosphorus- asilimia 0.5-0.9
Kalsium- asilimia 0.4-1
Potasiam- asilimia 2-4.5
Magnesium- asilimia 0.5-0.65
Manganezi- asilimia 0.11-0.16
Madini chuma – asilimia 0.06-0.26
Kabohyadrate tata {starch}- asilimia 6.54
Crude fibre {nyuzi nyuzi ghafi}- asilimia 9.1
Sukari mumunyifu {glucose}- asilimia 3.5
Kutokana na uwiano huo,mmea huu umepewa sifa ya kuwa na uwiano wa virutubisho ulio sahihi hivyo kuwa halali kwa malisho ya wanyama wetu wafugwao ikiwemo Ng’ombe,mbuzi ,kondoo ,sungura,nguruwe,kuku na samaki pia ili kuweza kuboresha afya za mifugo yetu pamoja na kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa mifugo hiyo

FAIDA ZA MMEA HUU WA MAAJABU
Kwenye sekta ya kilimo
Ni chakula kwa wanyama wote wafugwao, kutokana na kuwa na uwiano sahihi wa virutubisho
Pia kwa wakulima ni nzuri kama mbolea ya kijani hivyo kusaidia kwenye makuzi ya mazao nahii ni baada ya kuhifadhi sehemu na kuacha ikaoza ndipo hutunika kama mbolea

Kwenye sekta nishati
Mmea huu wa azolla pia hutumika kwenye upatikanaji wa nishati ya biogass , na hii ni baada ya kuvuna na kujaza ndani ya visima vilivyozibwa pande zote ,hivyo kuruhusu joto na unyevu unyevu kuozesha {decompose} mimea hiyo na kuzalisha gesi mbali mbali aina ya methane ambayo hutumika kama chanzo cha nishati mbadala kwa matumizi ya majumbani kwetu
Kwenye mazingira
Mmea huu hasa maeneo ya jua kali {tropical region} husaidia kupunguza kiasi cha uvukizi [ evaporation] wa maji kwenye vyanzo vya maji hivyo kusaidia katika kutunza na kuendeleza vyanzo vya maji kwenye maeneo hayo hasa wakati wa wote wa kiangazi.
Pia mmea huo hutumika katika kupunguza kiwango kikubwa cha upotevu wa gesi ya oksijeni kikemikali na hata kibaiolojia kwakuwa hutumia kiasi kidogo cha gesi hiyo kwenye makuzi yake binafsi hivyo kufanya mzunguko wa gesi hiyo kwenye mazingira kuwa mkubwa wakati wote hasa usiku.Pia mimea hiyo husaidia katika kuboresha maji taka ni pamoja na kupunguza madini mbalimbali hatarishi yanayopatikana kwenye maji taka mfano nitrojeni na phosphorus .

NB; Mmea huu pia umeajiri watu ,baadhi ya watu wanajiingizia kipato kwa kuuza mbegu pamoja na kuuza mmea huo uliochakataliwa {processed} kama chakula cha mifugo moja kwa moja ,pia watu wanaweza kujipatia kipato kupitia uchimbaji wa visima sahihi kwa ajili ya uzalishaji wa mmea huu.

HASARA ZA MMEA HUU
Kutokana na kuwepo kwa faida ya mmea huu pia mmea huu ni hatari kwenye mazingira yaliyokuwa na uhitaji wa mvua nyingi mfano mazingira ya wakulima nahii ni kwa kupunguza kiasi cha uvukizi wa maji kwenye vyanzo vya maji hivyo kuaribu mzunguko mzima wa upatikanaji wa mvua.

NI KWA NAMNA GANI NAWEZA ZALISHA MWENYEWE HILI NYUMBANI ?
Woow!! ni rahisi sana fuatilia mtiririko chini
haina haja ya tractor ya kuchimba kisima ila ni wewe na jembe la mkono tuuh kwasababu visima hivyo huwa sio vyenye kina ,huwa ni visima vyenye urefu mdogo kwenda chini,hivyo basi pima urefu na upana utakao pendelea kutokana na uzalishaji utakaoutaka

images%20(6).jpg


Width {UPANA}
Length {urefu}
Eneo la kisima ni sawa na uso wa maji

Baada ya hapo anza kuchimba kwa kuzingatia vipimo vyako na hakikisha hauchimbi kwenda chini sana ni kwa kiasi tu kwa makadirio ni kama inchi 5-6 kwenda chini,

v4-460px-Build-a-Koi-Fish-Pond-Step-2-Version-3.jpg.jpg

Source; agroimage

Baada ya hapo chagua kati ya kusakafia na cement au kufunika la ardhi na plastics cover ili kusababisha maji kutuama eneo husika hivyo kukamilisha zoezi zima la uandaaji wa visima mahususi
kwa uzalishaji wa azolla

images%20(3).jpg

Comp3-6.jpg

source; agroimage.com

Baada ya hapo changanya udongo wenye rutuba pamoja na mbolea zitokanazo na wanyama pamoja na maji safi, kisha jaza kisima chako na mchanganyiko huo.kisha hatua ya mwisho ni kuweka miche yako ya azolla na kuiacha kwa ndani ya wiki mbili tu hapo ndipo mda wa mmea huo kuchipua na kutanda ndani ya maji yako na hapo ndo ndipo utaweza kuvuna na kwenda kulisha wanyama wako

download%20(1).jpg

Source fertilizationpond.com



Kuzingatia
Zao la azolla linaweza kustawi katika maeneo yote ya ardhi lakini hasa kwenye maeneo ya maji yenye kiasi cha hydrogen [Ph range] 3.5 hadi 10,na katika kiasi joto cha 18 hadi 26 kizio cha joto.
images%20(2).jpg

Source;google azzolla

HITIMISHO
Katika kukuza mazingira imara na kamilifu uwepo wa Zao la azolla ni muhimu sana sana,pia ningependa kuiomba serikali hasa katika sekta ya mifugo kuweza kutoa elimu Zaidi vijijini ihusuo malisho ya wanyama yaliyosahihi pamoja na usisiizaji wa ulimaji wa zao ili kukidhi viwango vya juu katika uzalishaji kwa mifugo yetu ili kuhimili mahitaji ya watanzania wote milioni sitini.niwatoe shaka wapendwa ,kujitoa na kuanza kulima zao hili Kwa ajili ya mifugo Yako au kujipatia kipato hautojuta kamwe Kwa sababu haitegemei Hali ya hewa kama yalivyo mazao mengine ya chakula nchini,kwahiyo ni wasihi sana ndugu zangu niwakati wa kubadilika na kuanza kuchangamkia fursa haraka

Asante Kwa usomaji ,
Fuatilia zaidi kuhusu Azolla kupitia


 

Attachments

  • Comp3-6.jpg
    Comp3-6.jpg
    107.2 KB · Views: 25
  • images%20(5).jpg
    images%20(5).jpg
    10.1 KB · Views: 19
  • Comp3-6.jpg
    Comp3-6.jpg
    107.2 KB · Views: 19
Mje mlime azola sasa
Wazo zuri na la kutujenga sisi kama wakulima na watanzania Kwa ujumla ,tuanze kujitathmini katika kutafuta njia mbalimbali za kujipatia vyakula vya mifugo wetu na sio kudepend kwenye source moja tuuh ambayo inachukua mda mrefu kutupatia chakula Kwa wingi
 
any amplified thing won't work as amplified...ingia uone mwenyewe..faida na hasara zake..
 
any amplified thing won't work as amplified...ingia uone mwenyewe..faida na hasara zake..
Ni kweli mzee wangu,lakini kwenye kilimo we take risk na isitoshe hapa tunalima hili zao Kwa ajili ya mifugo yetu na halitegemei kabisa Hali ya hewa kama mazao mengine ya chakula so mda wowote na mahali popote unauwezo wa kulima na kujipatia chakula Kwa ajili ya mifugo yako.nikutoe wasiwasi
 
Asanteni sana Kwa inbox zenu ,tupo pamoja katika kuhakikisha tunaenda pamoja
 
Wazo zuri na la kutujenga sisi kama wakulima na watanzania Kwa ujumla ,tuanze kujitathmini katika kutafuta njia mbalimbali za kujipatia vyakula vya mifugo wetu na sio kudepend kwenye source moja tuuh ambayo inachukua mda mrefu kutupatia chakula Kwa wingi
Pia inaongeza rutuba kwenye udongo
 
Mkombozi wapi? Hizo azzola zingekuwa.mkombozi, ungekuta hawa wakina Silvet land wanazalisha kulisha kuku wao. Hakuna kitu hapo, hio ni kwa backyard kwa project kubwa hakuna cha azolla
 
Mkombozi wapi? Hizo azzola zingekuwa.mkombozi, ungekuta hawa wakina Silvet land wanazalisha kulisha kuku wao. Hakuna kitu hapo, hio ni kwa backyard kwa project kubwa hakuna cha azolla
Ni MKOMBOZI mkubwa sana Kwa wale wasio nakipato Cha kuafford kununua concentrates pamoja na mineral supplement hasa Hawa wakulima wadogo,sasa Kwa upande wako huwezi ona MKOMBOZI Kwa kuwa umeenda Kwenye enterprises kubwa Ambapo huko wanauwezo wa kuafford mineral supplements pamoja na concentrates Kwa ajili ya mifugo Yako (Kuku Kwa jinsi ulivyosema),na pia hili ni fundisho yah likiwafikia wanaweza kuunda farmstead planning Kwa ajili ya kilimo hichi Cha azola,
Hata wewe pia unaweza ukaanza kulima broh Kwa ajili ya mifugo Yako kupunguza gharama ya kununua vyakula vyenye bei
 
Mkombozi wapi? Hizo azzola zingekuwa.mkombozi, ungekuta hawa wakina Silvet land wanazalisha kulisha kuku wao. Hakuna kitu hapo, hio ni kwa backyard kwa project kubwa hakuna cha azolla
Nikuweke wazi tuuh,ndo maana tumeiandika hii kuwafungua vichwa watanzania na hata hao wenye kumuliki enterprises
 
Wakuu kwa wale wenye uhitaji wa Azolla , ninazo karibia robo heka,natuma maeneo mbali mbali nchini,njoo in box,kilo sh 7000
 
Back
Top Bottom