Watu waliokufa kipindi ambacho hata dini ya ukristo na uislam hazijaanzishwa wako wapi kama tunajiaminisha kwa kusema dini humfanya mtu kuona pepo?

Uliwahi kujiuliza! kwannini watu tunatumia lugha tofauti katika kiwasiliana?au je kwanini rangi zetu zumetofautiana?.

Mkuu kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu dini, au ya kuwauliza watu waliojikita sana kwenye dini Kwanza ni kwanini sisi waafrika au watanzania hakutafuta uhuru kutoka kwenye dfini. Kwa kiingereza ningesema freedom from religion, ni kama tumeamua kuwa wafungwa na watumwa wa dini. Thiolojia ambazo wageni walileta kutudhibiti, na tumekubali kabisa kujiweka chini yake.
 
Sasa chukua hii!!rizqi anatoa mungu lakini kupitia wanaadamu wenzetu!
 
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Ukristo/uislam umeanza lini?

Kabla ya hapo watu walimjuaj Mungu?
Tuanzie hapo kwanza
 
NB: Dini hazikuja baadae sana zilikuwepo miaka na miaka ila sema dini za Abrahamic/Mashariki ya kati (Islam/Jewish/Christianity) ndio zimekuja Afrika baaadae sana ila haimaanishi hazikuwepo huko nyuma kipindi tunatambika. Kama na sisi tungeamua kusambaza dini zetu huko ulaya na uarabuni leo hii penginepo ng'wanamalundi angekuwa nabii wao wanamwabudu.[/QUOTE]

Mkuu ww una msimamo gan, waliokufa kipindi hicho, walienda peponi au jehanam?
 
Hivyo, wokovu ni kwa wanadamu wote - wale 'watakaoamini wataokoka' na 'wasioamini wataangamia'.[/QUOTE]

Hakuna kitu kama hicho
 
Nakataa kauli yako ya uongo ya kusema ya kuwa suala la kutokutii kwa Ibilisi ndio kumezaa jambo la moto.

Soma hapa katika surat Insaan aya ya 1-2. Anasema Allah aliye juu :

1. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa.
2. Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru. (al Insaan : 1 - 2 ).
Bado Hujajibu hoja ya mada..... Sawa kauli yangu unaweza usikubaliane nayo sasa basi what is the alternative?? Je nini chanzo cha hukumu ya moto? Na kwanni Mungu aliweka hyo hukumu??

Pia nimejenga hoja kupitia Hyo Sura ya 7... Hivyo basi ungetuelewesha jukwaa zima Je hapo nlipoquote Allah alimaanisha nini?? Aliposema watakaokufuata nao watatupwa Jehannum je hamna role ya Ibilisi mpaka hapo??

Embu funguka mkuu watu wajifunze
 
NB: Dini hazikuja baadae sana zilikuwepo miaka na miaka ila sema dini za Abrahamic/Mashariki ya kati (Islam/Jewish/Christianity) ndio zimekuja Afrika baaadae sana ila haimaanishi hazikuwepo huko nyuma kipindi tunatambika. Kama na sisi tungeamua kusambaza dini zetu huko ulaya na uarabuni leo hii penginepo ng'wanamalundi angekuwa nabii wao wanamwabudu.

Mkuu ww una msimamo gan, waliokufa kipindi hicho, walienda peponi au jehanam?
[/QUOTE]
Mie sio mtaalum wa dini so sina uhakika wa hili suala ndio maana naeleza kwa mujibu wa vitabu vya dini tu kama alivyotaka mtoa mada.

Hivyo jibu ni wameenda JEHANAM.....
 
Bado Hujajibu hoja ya mada..... Sawa kauli yangu unaweza usikubaliane nayo sasa basi what is the alternative?? Je nini chanzo cha hukumu ya moto? Na kwanni Mungu aliweka hyo hukumu??

Nimekupa aya kuonyesha ya kuwa ulicho kisema si sahihi,ya kwamba si sahihi ya kuwa kuasi kwa Ibilisi ndio chanzo cha watu kuwekwa motoni. Maandiko yako wazi na swali lako nimelijibu.

Swali la hapa ni swali lingine si swali la mwanzo kuhusu chanzo cha hukumu ya moto,ni ahadi ya Mola kwa waja wake watakao kwenda kinyume na sheria zake yaani kinyume na amri zake. Yaani huo ni utaratibu wa chaguzi za adhabu kwa waja wake. Hekima ya yeye kuweka moto kama adhabu anaijua yeye na yeye ni mjuzi wa kuadhibu.

Kuhusu kujibu swali la mada husika sijalijibu makusudi kwanza kwa kumpa nafasi ya mtoa mada kukiri juu ya swali lake kama nilivyomuuliza. Na nimemuahidi kumjibu swali lake kwani si swali gumu,ni muda tu.
 
Pia nimejenga hoja kupitia Hyo Sura ya 7... Hivyo basi ungetuelewesha jukwaa zima Je hapo nlipoquote Allah alimaanisha nini?? Aliposema watakaokufuata nao watatupwa Jehannum je hamna role ya Ibilisi mpaka hapo??

Suala la moto kuumbwa lilikuwepo kitambo hata kabla ya viumbe hivi kuwepo. Kuasi kwa Ibilisi ni matokeo na moto upo kwa ajili ya binadamu na majini na Ibilisi ni miongoni mwa majini.

Nimekuanzia aya ya 14 katika sura ya 7 Qur'aan ili upate mtiririko wa jambo jinsi lilivyo. Soma tena aya hizo.

14. Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa.
15. Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula.
16. Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.
17. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani.
18. Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote
19. Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu
20. Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele.
21. Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini.
22. Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri? (al 'Araaf : 14 - 22)
 
Mtu wa mwanzo kuumbwa alikuwa Adam kisha akaumbwa Hawa kutokana na Adam, baada ya kuumbwa walipewa muongozi wa kuishi na muumba wao, waliteleza katika kufuata maagizo hayo lakini waliomba msamaha na walisamehewa.
Maana ya neno Islam maana yake ni amani, kujisalimisha kwa Mola mlezi, watu wanafikiri dini ya uislamu ilianzishwa na Muhammad bin Abdullah (S.A.W.) hapana bali yeye ni mtume wa mwisho wa Allah, uislamu ulikuwepo toka uumbwaji wa dunia, tunaamini kila mtu aliyeamini kuwepo kwa Mungu mmoja asiyezaa wala kuzaliwa na hafanani na kitu chochote ni muislamu.
Mungu alikuwa akiteremsha wajumbe wake kutokana na utashi wake, ikiwa kuna watu ambao hawajafikiwa na ujumbe huo basi hao Mungu hawezi kuwahukumu, kwa kuwa alisema hawezi kuwaadhibu watu mpaka awapelekee mtume.
Ongea point kidogo basi acha kudanganya. Au Quraan inakuambia udanganye? Mwislam wa kwanza alikuwa Muhamad tena according to Quraan yako. Na alieshushiwa hiyo alikuwa Muhamad. Usiongee uongo
 
Ukwl ni huu hapa

kwanza tuamn kwamba ktakua na ufufuo wa ambao ni waadlfu na wasio waadlfu Matendo 24:15

Hapo kwenye wasio waadlfu ni wale ambao hawakuskia Neno imean hawakulpata kama wale wanaoish Polin Imean bush man na kama hao unaowasema hapo ambao hawakuiskia mababu ztu

swal ulza mm
 
(44) Al-Muminoon
Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini.

(15) Al-Israa
Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.

Baada ya aya hizo hapo juu, msingi wa hoja ya mtoa mada upo hapa....

(51) Taa-Haa
Akasema: Nini hali ya karne za kwanza (yaani watu walioishi kabla ya huu ujumbe wa nabii Musa kuwafikia)?

(52) Akasema: Ilimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi katika Kitabu. Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau.

Yaani, kuhusu hatma (peponi/motoni) ya hao watu walokufa kabla ya kujiwa na ujumbe wa mtume /nabii husika ni MwenyeziMungu tu ndiye anayefaham.

~M/Mungu ni Mjuzi~

NB: kwenye ( ) katikati ya aya ya 51 ni yangu ili kuextend ufaham
 
Bado Hujajibu hoja ya mada.....

Hoja ya mada naijibu kwa mtindo huu,ni baada ya kuona mtoa mada anachelewa kujibu swali nililo muuliza.

Katika dini ya kiislamu kuna watu wanaitwa "Ahlul Fitrah" watu hawa hawakufikiwa na ujumbe wapo waliokuwepo baada ya mtume Issa mpaka zama zetu hizi,na kuna watoto walio kufa kabla ya kubaleghe ambao watoto hao si waislamu kwa maana ya kuwa hawakufika muda wa kuandikiwa madhambi.

Mola wetu ni muadilifu sana,hatoi adhabu kwa waja wake bila kuwafikishia ujumbe kama anavyosema Allah aliye juu :

15. Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume. (al Israa : 15)

Na akasema tena katika surat al Mulk aya ya 8 :

8. Inakaribia kupasuka kwa hasira. Kila mara likitupwa kundi humo walinzi wake huwauliza: Kwani hakukujieni mwonyaji? (al Mulk : 8)

Aya hizi zinaonyesha ya kuwa Allah hawaadhibu waja wake mpaka uwafikie ujumbe na malaika wa motoni yaani walinzi,pindi watakapo kuwa wanawaingiza watu motoni watakuwa wanawauliza watu wale kwa kusema :

71. Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri. (az- Zumar : 71)

Sasa wale ambao hawakufikiwa na ujumbe watawekwa siku ya hukumu mbele na watapewa mtihani,watakao faulu wataenda peponi na watakao feli wataenda motoni. Hii ndio hukumu ya watu hao.
 
Suala la moto kuumbwa lilikuwepo kitambo hata kabla ya viumbe hivi kuwepo. Kuasi kwa Ibilisi ni matokeo na moto upo kwa ajili ya binadamu na majini na Ibilisi ni miongoni mwa majini.

Nimekuanzia aya ya 14 katika sura ya 7 Qur'aan ili upate mtiririko wa jambo jinsi lilivyo. Soma tena aya hizo.

14. Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa.
15. Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula.
16. Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.
17. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani.
18. Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote
19. Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu
20. Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele.
21. Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini.
22. Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri? (al 'Araaf : 14 - 22)
Shukrani kwa kujenga hoja hivi na ndio nilichotaka ili wasomaji wote tufaidike....

Sasa basi najikita hapo Verse 18, je alimaanisha nini kusema watakaokufuata watatupwa Jehanam kama yeye ibilisi??

Je ina maana kuna Role ya Ibilisi kufikisha watu motoni??

If No?? Je Ibilisi kupewa ''likizo'' mpaka kiama ambapo kaachwa kudanganya ulimwengu ili wamkosee muumba wao hapo bado hakuna role ya Ibilisi kwenye kudetermine watu kutupwa motoni??

Hapo ndio naomba ufafanuzi mkuu maana naona una undermine role ya ibilisi kusababisha watu kutupwa motoni

Karibu
 
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Kwny uislam mtume wa kwanza ni nabii Adam (a.s) na ndie binadamu wa kwanza, sasa iweje useme wapo binadamu waliokuwepo kabla ya uislam
 
Shukrani kwa kujenga hoja hivi na ndio nilichotaka ili wasomaji wote tufaidike....

Sasa basi najikita hapo Verse 18, je alimaanisha nini kusema watakaokufuata watatupwa Jehanam kama yeye ibilisi??

Je ina maana kuna Role ya Ibilisi kufikisha watu motoni??

If No?? Je Ibilisi kupewa ''likizo'' mpaka kiama ambapo kaachwa kudanganya ulimwengu ili wamkosee muumba wao hapo bado hakuna role ya Ibilisi kwenye kudetermine watu kutupwa motoni??

Hapo ndio naomba ufafanuzi mkuu maana naona una undermine role ya ibilisi kusababisha watu kutupwa motoni

Karibu

Ibilisi ni adui mkubwa kwa wanadamu na sisi tumetahadharishwa nae,kwa sababu ana uwezo wa kushawishi watu kufanya maasi.

Lakini Allaha alishasema ya kuwa wale waja wake walio simama katika msimamo wa dini Ibilisi hatoweza kuwashawishi.
 
zamani kabla ya Dini wewe hukuwepo pia kumbuka tu wao walikuwa na imani zao ambazo walifundishwa kwa wakati huo.Kumbuka tena kila zama na kitabu chake .
sawa mkuu ila vitabu vyote vinaonesha siku ya hukumu ni moja tu na kwa Mungu hakuna kubadilika na Mungu ni yule yule siku zote sasa inakuaje kuwe na mgawanyiko wa imani au je kuna Mungu wa sasa na wa zamani?
 
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Nadhani swali lako limelenga dini zoote japo hujataka kuwa specific unataja dini gani,kwa kuwa mimi ni kristo nitalijibu swali lako kikriso zaidi kwa kutumia maandiko ya kwenye kitabu cha biblia uwe unakiamini au hukiamini ndio muongozo wetu sisi wakristo kwenye hii safari ya kuelekea peponi,kimejaa majibu yoote yanayohusu dini yetu,na pia wenzangu wa dini zingine watakuja kujibu kwa namna watakavyoona inafaa.
Kwa sisi wakristo katika dini yetu kuna makanisa mawili,kuna kanisa la kwanza lililokuwa chini ya sheria,na kanisa la pili ambalo tupo sasa chini ya neema,kwa lugha nyingine ningeweza kuandika kuwa kuna nyumba mbili,nyumba ya kwanza iliyokuwa chini ya sheria na nyumba ya pili iliyo chini ya neema ndiomaana ndani ya biblia imeandikwa utukufu wa kanisa(nyumba) ya mwisho utakuwa mkubwa kuliko utukufu wa kanisa(nyumba) la kwanza (HAGAI 2:9)
1.KANISA(NYUMBA) LA KWANZA
Hii inajumuisha watu woote waliokuwepo tangia kuumbwa kwa dunia hadi siku ile ya pentekosti Roho mtakatifu anawashukia mitume,watu waliokuwa chini ya hili kanisa walikuwa chini ya Neema ya Mungu mwenyewe kama wakiwa na imani kwake.
2.KANISA(NYUMBA) LA PILI
Hii inajumuisha watu woote tangia siku ile ya pentekosti Roho mtakatifu kashuka duniani hadi sasa hivi,kanisa la sasahivi linaitwa kanisa la Neema,tunaokolewa kwa kuisikia INJILI, na sio tena zile sheria za torati na manabii, na injili ni rahisi imeandikwa UTUBU,UBATIZWE UJAZWE ROHO MTAKATIFU ndio injili waliyoagizwa mitume hizo ndio habari njema tulizoambiwa.
Huwa sipendi kujibu maswali kwa juu juu ndio maana nimeanza kuelezea kanisa la kwanza na kanisa la pili la leo,sasa nikirudi kwenye swali lako umeuliza kwanza watu kabla ya hii INJILI (DINI) haijaja walikwenda wapi??,Jibu ni hivi woote walikuwa wanakwenda chini kuzimu(Chini ya nchi),! isipokuwa kuzimu ilikuwa imegawanywa kulikuwa na mpaka kati ya watu waliokuwa wamefanya matendo mema kwa mujibu wa imani zao kwa Mungu na watu waliokuwa wamefanya matendo mabaya ambao hawakumuamini MUNGU
Sehemu walipokuwa wanaenda waliotenda matendo mema palikuwa pamepewa jina la "KIFUANI PA ABRAHAM" kati ya hizi sehemu Mbili kulikuwa pametenganishwa na shimo kubwa wa huku hawezi kwenda kule na wa kule hawezi kuja huku rejea mfano wa Yesu (LUKA 16:19-21),Watakatifu wa kanisa la kwanza walikuwa wanakwenda hapa 'kifuani pa ibrahimu" kama sehemu ya kupumzikia sababu wao walikuwa watakatifu ambao dhambi zao zilikuwa zimesafishwa kwa kafara ya wanyama (kama kondoo na ng'ombe') sasa kafara halisi ya Yesu ilikuwa haijaja bado na kwa kuwa Yesu pekee ndio njia ya kwenda mbinguni iliwapasa hawa watakatifu wa kwanza wasubiri kifuani pa ibrahimu hadi Yesu atakavyokuja!.iliwapasa watu waliokufa kabla ya Yesu kuja nao Wasikie/Wahubiriwe INJILI kusudi siku ya mwisho asiwepo mwanadamu ambaye atasema hakuisikia injili kwa kuwa Mungu ni Mungu wa Haki hukumu zake ni za haki! (1Petro 4:1-6)
Yesu alivyokufa aliwaendea wafu waliokuwa wamekufa kabla ya kuja kwake kwenda kuwahubiria injili na hao waliomkubali siku walifufuliwa na wakawatokea watu wengi! (Mathayo 27:51-53),
kumalizia kwa mujibu ya sisi wakristo na hayo maandiko niliyoyaweka hapo,watu woote siku ya mwisho watahukumiwa kwa INJILI sababu woote waliisikia INJILI waliokuwa wamekufa kabla ya INJILI kuja duniani na ambao tupo kipindi hiki cha INJILI na ndiomaana hadi Yesu anakuja mara ya pili INJILI itakuwa imeshahubiriwa kila kona ya DUNIA kila mtu atakuwa kaisikia INJILI
"TUBU,BATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO, POKEA ROHO MTAKATIFU" utaokolewa
 
Back
Top Bottom