Kwa failed system kama ya CCM ni kwamba Serikali haiendesheki na si hujuma

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,198
Wengi wanaweza wasinielewe. Ila kwa wenye kuelewa mambo na walioiona CCM ktk historia, watakubaliana nami. Na hata wale wasioweka linganisha data nyingi sana kwa mara moja, wanaweza hata kuangalia quality ya wana ccm na kuona kuna shida zaidi ya watu,hata wale wanaopigiwa upatu. Bila nguvu za ziada hawawezi hata linda au kutetea value yoyote ya ccm.bila nguvu nyingi hawawezi simama ktk jukwaa huru la fikra.

Hakuna kiongozi wa ccm atakuja asianze sifiwa sana mwanzo, muda mfupi baadae. Kilio Cha hujuma toka ndani kisianze, kisipoanza cha hujuma basi watendaji wake wataambiwa ndio hawana sifa, baadae wanarudi tena ktk hujuma. Hii ni pattern inayojirudia. Ni pattern hihi inayoweza onekana kwa watu wasio na utaratibu wa maisha, au wanaomini mifumo, imani, na mila zilizoshindwa ktk dunia ya wakat huo.

Ni CCM hi hi imejengwa ktk ujamaa unaominisha watu unaoaminisha watu kwamba kushindwa kwao kunatokana na watu fulani wanaitwa mabeberu na si mipango na uendeshaji mbovu wa maisha yao.

Sitegemei popote katika maisha haya utawala huu mpya utakapoona mambo hayaendei wakimbilie ktk hoja kwamba anahujumiwa. Itakuwa ni kipindi km taifa kujiuliza km tunahitaji tena ccm ili tutoke ktk hii vicious cycle.

Tutakaposikia hii kilio cha kuhujumiwa basi wajue sisi wananchi ndio tuna kila sababu ya kuhujumiwa na tutahitaji nasi kulia hicho kilio na kudai fidia ya hizo hujuma.bado hatujalia, kwa vile tunaamini kulalama sio tiba, ila kuwakumbusha kwamba shida ni mfumo uliopitwa na wakati unaoshikiliwa na uwepo na chama kilichopitwa na wakati.

Ccm na hii nchi ni kama mdudu au binadamu aliyeingiwa ktk jiji na akitafuta njia ya kutoka huku akitembea kwa miguu,huku mitaa mingi ikizunguka hapo hapo na mingine haichomozi. Wapinzani ni km watu waliopo ktk jiji hilo hilo huku wakiwa na gari na chopa pamoja na google map. Ukiwa na chopa unaona mitaa na unaweza mwongoza mtembea kwa miguu mitaa ipi inachomoza. Ccm ni mtembea kwa miguu mpuuzi anayebishana na mwenye kujua njia huku akiwa hana njia ya kutoka. Mwishowe anaishia kurudi palepale

Magufuli akitaka fanikiwa hana haja ya kupoteza muda na kazi ngumu yenye tija ndogo kwa kujenga nyumba juu ya msingi wa mchanga mtupu CCM.

Anachoweza fanya cha kukumbukwa ni kuibomoa kabisa CCM. Mengine yatajiendesha yenyewe. Nchi nyingi zenye mifumo mizuri hujiendesha zenyewe. Ccm imetengeneza nchi hata ikiwa na uongozi haiendi sana. Ccm ni kikwazo kikubwa sana.

Ujamaa ni km mganga anayetambika wengine wapate pesa, huku yeye akipewa kidogo zaidi. Kwa misemo ya CCM mganga hajigangi. AS If mganga hawezi kunywa dawa anayompa mtu. Hamjawahi sikia watu wote waliojifunza vitu kwetu wamekwenda pata tuzo? SABABU Ni nini? Ni kwamba mchawi hastahili chochote ktk hii, mchawi ni km mtumwa anayeshikia vitu watu hadi wenyewe(warithi) waje chukua. Mwishowe hujisifu kwamba wao ndio watoa risiki, wao ndio watoto wa mjini, wao ndio master planners.

Kwa aliyewahi sikia huu usemi.."ULE Mradi ulikuwa mzuri sana hadi zilipoingia siasa" kwa lugha nyingine hawakusema tuu "ilikuwa nzuri hadi ilipoingia CCM". Walipogusa tuu ikanajisika.

Ujamaa si kitu halisia. Wajamaa kila ktk maonyesho yao ni uongo na kinaishia kuwa maonyesho tuu na si kwa matumizi. NI Kujionyesha tuu kuwa nao wapo au zaidi ila si vitu halisi. Kwa miaka yote tz ktk maonyesho utaona sample nyingi .

HATA Kilimo siku zote ni nursery.Hata kelele za kilimo kwanza ni maonyesho tuu.. WANAOFANYA Serious ni wale waliokuja ktk maonyesho. Dunia nzima kuna nchi zilijifunza kilimo kwanza na sasa wanakata mbuga. Wanachoweza ni kukwamisha wazawa kwa vile ndio size yao, ndio namna ya kuendesha huu mfumo ulioumbwa na wivu ndani yake, mfumo wenye ghiliba na kuchukia mafanikio. Waliofanikiwa kuharamishwa.

Kwa bahati mbaya sana watu hawajaona . Ila nadhani watz wacha mungu wangekuwa wamefunguka kidogo "wangefanya maombi ya kumshukuru mungu kwamba tupo salama hadi sasa". Mpaka sasa ujamaa na jiko lake CCM wameshafikisha watz ktk stage ya mbali sana kugeuzwa magaidi. Watz walipewa adui, wakapewa sababu za kuchukia, wakapewa moyo na nia ya kupigana, wakapewa kinga wasipate kuamka akili(wakaambia kila anayeamsha ni kibaraka asiyetakia nchi mema, kuwa anayewaamsha anataka madaraka). KISHA Wakapoozwa kusubiri amri ya uongozi mkuu..

PROPAGANDA Machines zote kuanzia vyuoni, mabalozi, na waandishi wote kazi ni moja kuwageuza magaidi na kuwakinga na wokovu. Ukiwasikiliza watz ktk mijadala unaweza tapika jinsi wanavyoongea km misukule bila aibu. Hata Walioona mwanga hawakuweza ona vyema kwani tayari matongotongo na ukungu yalishaganda sana machoni. Mara nyingine wakingalia vitu wanakuwa na wasiwasi km ni chenyewe.

Magufuli pole sana, hiyo ndio CCM na watu wake na uwezo wao. Makosa mengine si hujuma ndivyo akili zao zinawatuma kwamba wanafanya best thing around for the party. Ni makada walioapa kufia chama na mwenyekiti wake.

Soon utakuwa mwenyekiti utapewa utiifu wa kutisha. Hata yule mama shem wako kwa wajina alikuwa anatimiza wajibu wake kwa chama. Kutetea chama ili hayo mambo ya wezi wa mishahara kwa watumishi hewa mkamalize sirini km munge la siri.

Ndio akili za kijamaa, na bahati mbaya sana wajamaa huwa issue zao zinajigonga pabaya sana kiasi cha kuwafanya wasiamini km treni zao ni km nyumba ya babel na hakuna mkono wa mtu. Ujamaa ni shetani ndio maana wanajipa uungu kwamba binadamu(mwananchi ana mapungufu sana bila kuongozwa na kusaidiwa fikiri atatumbukia shimoni).

Wajamaa kwa vile miungu, chama ni dini, ikulu ni mbingu na mwenyekiti ndio mwenye fikra pekee sahihi. Basi huwasaidia wananchi kuchagua habari takatifu ili yule mwovu asiyewazidi. Basi Nape malaika mlinzi kaamua kuwasaidia wananchi wasisikie akina Kitwanga na akina Lema waovu wakubwa wanaoleta vitu vya kutwanga. Na kumvuta mungu(aka mwenyekiti sharubu).

Imagine Cuba leo ndio inapata internet na tv kwa wananchi wake. Pamoja na elimu na uwezo wa watu wake.Leo Cuba km gereji kubwa ya kukusanyia magari ya kizamani. WANGEKUWA Si wajamaa leo wangekuwa wapi?

Sidhani km Marekani ndio waliwanyima Cuba kuwa na internet zaidi ya Mungu Castro mlezi wa kila raia, mungu wao na baba yao wa kulinda hadi na fikra mpya.

Huo ndio ujamaa km ugaidi ulivyoacha nchi za watu na mateso makubwa bado wanaamini wengine ndio wanawahujumu km vile wengine ndio waliwalisha hizo itikadi za kuwazungusha ktk matatizo bila kutoka.

In fact kilio chochote cha utawala huu kuhusu kuhujumiwa ni ushahidi tosha kwamba shida si kiongozi ni CCM(mfumo usio na mpangilio wenye maana). MAGUFULI Alijibainisha km CCM na serikali akaiita yake. Watz wakaamini km ni yeye basi nchi itakwenda. Sasa hata yeye anaona CCM ndio shida. Wapinzani walikuwa sahihi.

Its funny majibu speaker wa bunge anahukumu kesi ambayo yeye mwenyewe ni mtuhumiwa, badala ya kujibu tuhuma anadhibu mlalamikaji kwa kulalamika. Huo ndio ujamaa "The sum of all stupidity"

Leo Mkapa hajui kwanini mchakato wa katiba kakwama. Leo magufuli hajui sasa udini sijui udhehebu uliomwingiza ndio kikwazo kwake, sasa hivi udini umewekwa on guard kulinda old guards. Huu ndio wendawazimu wa ujamaa. Hawana project endelevu. Yenyewe ndani kwa ndani ina mifumo ya kujibomoa au kubomoa project zao wenyewe. Tazama radio za Ccm, sukita, na TBC.

Hayo ni maono ya kifikra na nawasilisha rasmi.
 
Viongozi wetu wakivurunda hawataki kukubali pale wanapovurunda ni mabingwa wa kulalama kua wanahujumiwa na watu au mfumo hawataki kuwajibika.
 
Unaweza ukawa na chembe chembe ndogo sana za hoja, lakini kwa hivi vyama vya Kichagga , Ccm bado inahitajika sana. CCM ni chama kizuri sana kilikuwa kinaharibiwa na Mafisdi na wale walioamini CCM ni wao na wao ndiyo CCM. Magufuli anarudisha hadi ya CCM, itachukua muda sana Upinzani huu wenye mrengo wa Ukabila, Udini na Ukanda kuiondoa CCM madarakani. Siyo mtazamo wangu, ni mtazamo wa Watanzania walio wengi. Ndivyo wasemavyo makazini, vijiweni, kwenye mikusanyiko ya starehe n.k.
 
Mwaka jana ulikuwa ni wakati muafaka sana kwa upinzani kusimama na kuwaeleza wananchi ni suluhisho lipi mbadala walilonalo, ili CCM iweze kuonekana imepitwa na wakati. Bahati mbaya sana kwa upinzani wakashindwa kuja na mawazo mbadala, wakashindwa kujenga hoja kwa vitendo ili wananchi wengi waweze kusema huu ni muda muafaka wa kuondokana na CCM.

JPM kupiga pushup jukwaani ulikuwa ni ujumbe mzito sana wa kisiasa, alionyesha watu kwamba mimi ninafanya hivi sasa mwambieni yule wa upande wa pili afanya kama nilivyofanya. Siku zote mpiga kura hutakiwa kuiona nuru ya matumaini kwa mgombea wa urais. Kati ya JPM na EL ni JPM aliyekuwa na nuru, aliyekuwa amebeba matumaini kwa maana halisi ya neno hilo. Ndio maana mwaka 2008 Barack Obama akaja na kauli mbiu ya Change, na alifanana na hayo mabadiliko.

Uchaguzi wa mwaka jana na matokeo yake ni somo tosha kabisa kwa upinzani, ni lazima wajipange ili waweze kupata mgombea mwenye nuru ya kweli, na sio kumtegemea mtu ambaye badala ya kuleta taswira ya change, anaanza kuwafanya watu wamuonee huruma. Kura za mahaba ni kitu kimoja, kusimamia mabadiliko na kuweza kuyaelezea kwa kirefu ni kitu kingine.
 
Inamaana msajiri wa vyama na serikali yake wanasajiri vyama vya kikabira hamna akili kabisa.
 
Unaweza ukawa na chembe chembe ndogo sana za hoja, lakini kwa hivi vyama vya Kichagga , Ccm bado inahitajika sana. CCM ni chama kizuri sana kilikuwa kinaharibiwa na Mafisdi na wale walioamini CCM ni wao na wao ndiyo CCM. Magufuli anarudisha hadi ya CCM, itachukua muda sana Upinzani huu wenye mrengo wa Ukabila, Udini na Ukanda kuiondoa CCM madarakani. Siyo mtazamo wangu, ni mtazamo wa Watanzania walio wengi. Ndivyo wasemavyo makazini, vijiweni, kwenye mikusanyiko ya starehe n.k.
Ccm inausajiri sawa na hivyo vyama vya kikabira.
 
kwa uandishi huu ni wazi shida ni itikadi za ccm na watu ambao ni matokeo ya hizo itikadi. Mnajua CCM haikwezi linda hoja wala shawishi watu.Zaidi ya nguvu za ziada ccm(Chaguzi za URAIS ZOTE SASA NI DONT ASK ,DONT TALK). Otherwise ni km Peugeot 304, ktk barabara za vijiji vyetu.
 
Tena wakabadilisha gia kwa sababu tu ya Ukanda , wakasahu uchafu wa wana UKANDA wenzao. Ni shiiida.
Macho yenu na akili zenu ndizo zinaona ukanda. UMESAHAU MIMI NDIE HUWA NAWAAMBIA CCM HUBUNI UONGO UNOTOSHA KUJIDANGANYA WAO WENYEWE? Hata kinywaji huwa mnasema ni wengine ,ila baadae nyie ndio mnakuja amini kwamba kiroba kinapandisha akili badala ya kujiuliza km kweli wapinzani wanakunywa kiroba.Sasa mnaishia umbuana. Hiyo ya Ukanda imerudiwa rudia sana hadi nyie nde mnaamini na kuona hivyo. "Self deceit " ndio practice ya upuuzi wa ujamaa.
 
Mwaka jana ulikuwa ni wakati muafaka sana kwa upinzani kusimama na kuwaeleza wananchi ni suluhisho lipi mbadala walilonalo, ili CCM iweze kuonekana imepitwa na wakati. Bahati mbaya sana kwa upinzani wakashindwa kuja na mawazo mbadala, wakashindwa kujenga hoja kwa vitendo ili wananchi wengi waweze kusema huu ni muda muafaka wa kuondokana na CCM.

JPM kupiga pushup jukwaani ulikuwa ni ujumbe mzito sana wa kisiasa, alionyesha watu kwamba mimi ninafanya hivi sasa mwambieni yule wa upande wa pili afanya kama nilivyofanya. Siku zote mpiga kura hutakiwa kuiona nuru ya matumaini kwa mgombea wa urais. Kati ya JPM na EL ni JPM aliyekuwa na nuru, aliyekuwa amebeba matumaini kwa maana halisi ya neno hilo. Ndio maana mwaka 2008 Barack Obama akaja na kauli mbiu ya Change, na alifanana na hayo mabadiliko.

Uchaguzi wa mwaka jana na matokeo yake ni somo tosha kabisa kwa upinzani, ni lazima wajipange ili waweze kupata mgombea mwenye nuru ya kweli, na sio kumtegemea mtu ambaye badala ya kuleta taswira ya change, anaanza kuwafanya watu wamuonee huruma. Kura za mahaba ni kitu kimoja, kusimamia mabadiliko na kuweza kuyaelezea kwa kirefu ni kitu kingine.
Kusomesha mjamaa na wengine wenye akili za asia ni hasara. Sasa umetumia akili nyingi hivi kuandika akili ndogo, na ujinga mwingine hata wewe mwenyewe huwezi uamini.Na hata hujui ukimaliza utapata reward gani?HIzo ndizo akili wa wajamaa tukose wote, mwishowe wanafaya kazi nyingi za bure.
 
Kusomesha mjaa na wengine wenye akili za asia ni hasara. Sasa umetumia akili nyingi hivi kuandika akili ndogo, na ujinga mwingine hata wewe mwenyewe huwezi uamini.Na hata hujui ukimaliza utapata reward gani?HIzo ndizo akili wa wajamaa tukose wote, mwishowe wanafaya kazi nyingi za bure.
Unasikitisha sana, kwa sababu wewe mwenye thread umeachana na hoja unaanza kuandika mambo yasiyohusiana na thread yako mwenyewe!!. Mlitaka mabadiliko kwa kutumia mwanasiasa ambaye alipaswa kuondoshwa na mabadiliko!!.
Mlitaka kutuingiza chaka baya sana, mlikosa strategies nzuri, jipangeni upya.
 
Sasa ndo umeandika nini? Tehetehetehetehe. Wapinzani bana! Kila siku mnahangaika na makapi ya CCM
mbona hujibu hoja zake moja baada ya nyingine? nadhani wakati mwingine huwa husomi vizuri mada, unakurupuka tu kukebehi.ni sawa na kuwa umevaa nguo chafu halafu ukiambiwa unajibu kuwa "hata kama ni chafu ni ya kwangu" wakati ambapo ilitakiwa ukaifue.
 
Unaweza ukawa na chembe chembe ndogo sana za hoja, lakini kwa hivi vyama vya Kichagga , Ccm bado inahitajika sana. CCM ni chama kizuri sana kilikuwa kinaharibiwa na Mafisdi na wale walioamini CCM ni wao na wao ndiyo CCM. Magufuli anarudisha hadi ya CCM, itachukua muda sana Upinzani huu wenye mrengo wa Ukabila, Udini na Ukanda kuiondoa CCM madarakani. Siyo mtazamo wangu, ni mtazamo wa Watanzania walio wengi. Ndivyo wasemavyo makazini, vijiweni, kwenye mikusanyiko ya starehe n.k.
mkuu, tuliaminishwa hivyo hivyo mwaka 2005 kuwaJMK ni mtu anayejua umasikini wetu maana alikuwa ana mazoea ya kukaa na wananchi vijiweni. je, maisha bora ya kila mtanzania yamepatikana? unauona ubaya wa huo unaouita mrengo wa upinzani wa udini,ukanda na ukabila tu, je mrengo wa CCM wa rushwa na ufisadi uliotufikisha hapa hukuuona?
 
Sasa ndo umeandika nini? Tehetehetehetehe. Wapinzani bana! Kila siku mnahangaika na makapi ya CCM
Nadhani hujaelewa , ngoja nikufundishe kwa urahisi , kwa mfano aliyetumia miezi miwili kuchambua watu ili apate mawaziri bora kabisa , tena wengine ilishindikana kuwapata ccm hadi akatoka nje kuwatafuta , lakini mwisho wa siku akamteua MTUKUFU KITWANGA , baada ya kitwanga kufahamika atalaumu kuhujumiwa ?
 
Back
Top Bottom