Mjadala kati ya wanaoamini uwepo wa jehanamu na wasioamini

pauli jm

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
391
278
Za jioni watu wa mungu?.

Kume kuwa na maswali mengi sana juu ya uwepo wa jehanamu, au kuto kuwepo kwake. Wengi wanao sema hakuna kitu kama hicho hubebwa na hoja ya huruma ya mungu. Kwamba watu hao husema haiwezi kuwepo kwani mungu ni mwenye huruma sana.

Nawanao sema jehanamu ipo wao husema nilazima iwepo kwani watenda maovu nilazima wa adhibiwe. Nakwamba mungu hakosei na wala hakukosea kui weka jehanamun.
==========
"Lakini jee jehanamu ipo?? au jehanamu ndio nini??.

Kwamujibu wa vitabu vitukufu / vitakatifu, jehanamu kwasasa haipo nandio maana kuna siku inayo itwa siku ya mwisho /siku ya hukumu. Nasiku hiyo ndiyo siku ambayo kila mtu atajua kwemba nini alicho panda na nini malipo yake.
"Siku hiyo ndiyo siku ya mwisho nandio siku ya walio tenda mema wata fufuliwa na kupelekwa mbinguni/peponi. Nakwa watenda mabaya au maovu,ndio wa jehanamuni.

"Kwamujibu wa biblia , jehanamu, ita fanyika hapahapa duniani yani dunia ndio ita geuka na kuwa jehanamu baada ya watu wale walio tenda mema kuondolewa naku pelekwa mbinguni. Walio baki ndio haswa watakao chomwa moto wa milele.

"Lakini jee wewe niwaupande gani?? Jee wewe una amini nini ?? Kuwepo kwa jehanamu au kuto kuwepo kwake.

"MIMI BINAFSI"
Mimi huamini haitakuwepo, kwasabanu zifwatazo...

"Jehanamu! Haikutajwa mwanzo kabisa wa uumbaji wa dunia, kwani katika vitabu vya mwanzo kabisa haiku tajwa. Mfano katika vitabu vitabu vya Agano lakale haipo kabisa hiyo jehanamu.
"Watu wakale walipo kosea, wali pewa adhabu za hapahapa duniani Mfano , Adamu na Hawa walipo kosea wali pewa adhabu ya hapahapa duniani.
Na watoto wao pia hivyohivyo Mfano mtoto wa Adamu alipo.muua mdogo wake nayeye ali pewa adhabu tofauti na jehanamu.
Na visa vingitu vya kale vinaonyesha wazi jehanamu haiku tajwa mwanzo kabisa, tuna soma kuhusu Safina ya nuhu, Sodoma gomora, nk. Lakini kwote huko mungu hakusema mwisho mta tupwa motoni(jehanamu) .

"Jehanamu ! Ilianza kitajwa na Yesu kwa mijibu wa maandiko. Lakini Yesu haku itaja sana ali igusiagusia tu wanafunzi wake waka iendeleza nao hawaku itaja sana Muhammad(s.a.w) ndiye ali kuja kui taja sana katika Qur an.

"Uki fwatilia historia yake utagundua; kadiri ya siku zilivyokuwa ziki sogea mbele ndivyo neno jehanamu lilivyo kuwa likikolezwa kutajwa.
Nandio maana.
Uyahudi! Hauli tambui Neno Jehanamu na wala katika Uyahudi hakuna jehanamu.
Ukristo! Una litambua lakini katika ukrisito hali tajwi sana.
Uislam! Unali tambua sana nalina tajwa sana.

Hapo utagundua kadiri ya masiku yalivyo kuwayaki songa mbele ndio Jehanamu ilivyokuwa iki tajwa ili kuwa tia watu Hofu.

"HURUMA ya MUNGU.

Mungu nimwenye huruma mno, nasifikirii kama ana weza kutenda hilo ila nina jua kwamba, adhabu ya mungu ni kalipiya. Akiamuwa ana weza kutenda lolote alitakalo kwani daima kazi yake haina makosa.

Lakini kama mungu katika kipindi cha Nuhu alipo angamiza nchi kwa Gharika; Baada yakufanya, vile yeye mwenyewe aliona huruma nakusema "hato mtendea tena mwanadamu kama hayo kwani mwanadamu ni dhaifu". Kama Mungu aliona huruma kwa gharika jee Katika Moto wa milele hato ona huruma??.

"Makosa yote ya mungu yana Adhabu za dunia. Mfano.

Mali za zuluma na ukahaba.

Maranyingi watu wanao dhulumu watu , mali zao hupita kama upepo na mwisho huwa hawa faidiki na lolote zaidi ya nafs kuwa suta.
Ukahaba! Mara nyingi ukahaba nikama ume laaniwa, watu unakuta,wana ingiza pesa nyingi lakini hawafanyi cha maana zaidi yakutumika na mwisho hujikuta matatani.

Hiyo ni mifano tu ila kila lililo katazwa lina madhara ya mojakwamoja ya hapahapa duniani, nakatika maisha yetu ya kila siku.

Ngoja niishie hapo ilinisi wachoshe na hizo ndizo sababu chache kati ya nyingi zakuni fanya ni fikiri hakina jehanamu..

Nawewe kama una sababu zako ama zakukufanya uamini uwepo wake au zakuku fanya uamini hakuna kitu kama hicho zishushe hapa ili tujue mbivu na mbichi.
=======
===
=
MWENDELEZO NA AYA NILIZI ZITUMIA KATIKA ANDIKO LANGU HILO.

Nilipo sema kwasasa hakuna moto uwakao nili tumia Aya hii.
"Lakini mbingu na nchi za sasa zime hifadhiwa kwa neno la mungu , kwaajili yakuharibiwa kwa moto. Zime weka kwaajili ya siku ile watu wasio mcha mungu, wata hukumiwa na kuangamizwa(2petr 3:7).
Hapo tuna ona haupo kwa sasa ila utakuwepo hiyo siku ya mwisho. Napia utakuwepo hapahapa Duniani.

Watu wengi neno "milele" ndio huwachanganya lakini je ni milele kweli au milele ina maanisha uta teseka milele??
Sio kweli kwamba mtu ata teswa milele kwamuji wa aya zifwatazo.

"Kulingana na Yesu maneno yote mawili yaani mwili na roho huangamizwa katika jehanamu (mathayo 10:28).
(Zingatia neno kuangamizwa)

Katika (mathayo 25:41) Yesu ana zungu mzia juu ya moto wa milele , alio wekewa teyari Ibilisi pamoja na malaika zake. Je neno hili milele lina dokeza kuwa jehanamu hiyo ni yamilele??
(Yuda7) ana,eleza habari za Sodoma na gomora kuwa imewekwa kama mfano wa wale watakao pata adhabu yao katika ule moto wa milele . Ni dhahiri kwamba moto wa sodoma na gomora hau waki pakaleo. Nandio maana nina sema hakuta kuwepo na moto wa milele.

yona alikaa siku tatu ndani ya,tumbo la samaki "nyangumi."(mathayo12:40) akatoka na,taarifa yake kwamba alikuwa milele (yona2:6) Bila shaka zile siku tatu na lile giza lisilo na matumaini. Vilionekana kwake kana kwamba ni milele.

Kama bado huja ielewa hoja yangu hapo. Nikwamba moto (jehanamu ) hauta mteketeza mtu(mwovu) milele bali mtu(muovu) atakufa kabisa na wala hataonekana tena, iwe nikwenye roho au mwili.
Kutokana na aya hizi.

Semi zinazo eleweka wazi katika maandiko yote zina tuambia kwamba waovu wata angamizwa.

Waovu wata angamizwa (zaburi 37:28)
Wata angamizwa (2petr 2:12)
Wata toweka kama moshi(zaburi 37:20)
Moto ule utawateketeza kabisa hadi watakuwa kama majivu (malaki4:1-3).

Mshahara wa dhambi ni "mauti" sio uzima wa milele katika jehanamu.


(yohana3:16) Yesu ana eleza kwamba mungu aka mtoa mwanawe wa pekee, bali wawe na uzima wa milele yesu ana ilinganisha miisho miwili: uzima wa milele au kuangamia sio kuteswa milele.
Kimsingi katika bibilia moto unao tajwa uta angamiza waovu na neno kuangamizwa lina maana kuuwawa kabisa na sio eti kuishi jehanamuni milele huku una teseka.

Nandio maana maandiko yanasema msi waogope wauao mwili bali muogopeni mungu awezaye ku ua mwili na roho katika jehanamu. Ina maana mungu ata ua mwili naroho nasio kuzi tesa milele.

Huruma ya mungu.

Mungu anasema hivi "kama mimi nilivyo mimi Bwana mungu mimi sikufurahii kifo chamtu mwovu ,bali napena mtu aacha mwenendo wake mbaya apate kuishi milele(Eze33:11) hapo utaona mtu mwovu hato ishi milele ila mtenda,mema ataishi milele.
 
Unapaondika kitu kinachohusisha vitabu vitakatifu ni muhimu kuandika rejea (reference) ili kuhalalisha hoja yako. Vinginevyo unachoandika kinakua ni porojo tu.

Msijidanganyike Jehanamu ipo. Yaani mateso ya kuungua moto usiozimika kwa watenda dhambi wote. Wale ambao hawakukubali kumkubali Yesu Kristo kuwa mwokozi wao.
Mathayo 5: 29-30
Mathayo 18: 8-9
Luka 9 : 43-48

Maana hakuna Jina jingine walilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo isipokuwa Jina la Yesu Kristo pekee.
Matendo ya Mitume 4: 12
 
"ilinisi wachoshe" = ili nisiwachoshe. Umenichoooshaaa. Wewe endelea kutafuta wanachama ambao na wao wana imani kama yako. FUMBO LA IMANI
 
Imani ya mtu na mtu ina tofautiana, hivyo si rahisi wote kuamini sawa juu ya jambo fulani. Hivyo wewe kama una amini kuwepo au kutokuwepo simamia imani yako vinginevyo utachanganyikiwa kwani hakuna aliyekwisha kufa na kufufuka na kutushudia kama kuna jehanamu au la.
 
Jehanum ilikuwa ni eneo moja nje ya mji wa jerusalem miaka 3000 iliyopita ambako watoto walikuwa wakitolewa kafara na kuchomwa moto,ni wakati wa mfame josia ndipo eneo hilo likaanza kutumika kama sehemu ya kuchomea sanamu za miungu
ya kipagani na watu waovu,baadae enzi anazaliwa yesu eneo hilo lilikua linatumika kama dampo la kutupa takataka na hata wahalifu walipouawa walitupwa hapo na kuchomwa moto pamoja na takataka.
Kwahiyo eneo hilo miaka nenda rudi palikua panavuka moshi kwani moto haukuzima hapo.

Inasemwa sasa kuwa hapo na asili ya concept ya bwana wetu yesu kristo kuhusu jehanum ambako wasiotenda mema watatupwa na kuchomwa moto milele huku mwana wa adamu akitawala mji wa jerusalem mpya.
Waovu watatupwa jehanum na watakaojaribu kugonga hodi kuingia katika mji wa jerusalem kamwe hawatafunguliwa bali watachomwa milele na moto wa jehanum
 
Kuhusiana na ukweli wa jambo hilo kimaandishi huenda likaleta maana tofauti kwa kila msomaji wa vitabu hivyo vya dini tofauti.

Jambo la msingi kuhusu kuwepo kwa jehanamu au kutokuwepo hakuna anaefahamu zaidi ya vitabu vilivyopo duniani pamoja na dini zake.

Naona tunajaribu kuweka mafungu katika hili, mara huyu hakuzungumzia jehanamu mara Yule alizungumzia kidogo ila flani alizungumzia sana.. Ukweli upo kwa Mungu na tuisubiri hiyo siku ambayo inaitwa ya mwisho.

Japokuwa mimi najuwa Alikufa kafa hakuna jipya lingine...
 
Like Niku ADD
Anthony Lawrence
nalb
Maaghay
Kama kazz
Mshanajr
rubii

Someni nilicho ongezea kwenye uzi.
 
Unapaondika kitu kinachohusisha vitabu vitakatifu ni muhimu kuandika rejea (reference) ili kuhalalisha hoja yako. Vinginevyo unachoandika kinakua ni porojo tu.

Msijidanganyike Jehanamu ipo. Yaani mateso ya kuungua moto usiozimika kwa watenda dhambi wote. Wale ambao hawakukubali kumkubali Yesu Kristo kuwa mwokozi wao.
Mathayo 5: 29-30
Mathayo 18: 8-9
Luka 9 : 43-48

Maana hakuna Jina jingine walilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo isipokuwa Jina la Yesu Kristo pekee.
Matendo ya Mitume 4: 12

Soma nilicho ongeza kwenye mada
 
Ulipoanza mada ako nilijua utagusia vitabu vyote kutoka imani zote. Hata ivo nashukuru kua umegusia upande mmoja tu yaani ule wa kikiristo.
Kwa imani ya kiislam hakuna shaka yeyote juu ya uwepo wa cku ya malipo, uwepo malipo yenyewe na pia uwepo wa moto (jehannamu) na pepo. Rejea qur an:
1:24, 1:217, 1:214, 4:173, 5:80, 5:86, 97:6, 97:7, 97:8
Hizo ni aya chache sana miongoni mwa aya nying zilizozungumzia uwepo wa moto na pepo na pia wale watakaoingizwa humo
Pia hoja hii hata ukiangalia katika mtazamo wa kawaida tuu, bac ni lazma utabaini kua uwepo wa moto ni lazma jama vle uwepo wa pepo kwan kama ucngekuwepo moto mungu angekua si muadlifu kwa kuwalipa sawasawa waliomtii na wale waliomkanusha na kukataa maamrisho ake. Sifa ambayo kwa mujibu wa uislam mubgu hanayo.
Vilevile, uliguca kua hata jama uo moto upo c wa milele, kwa mujibu wa uislam kama utaizsoma vizuri aya 6,7 na 8 katika sura ya 98 qur an utakuta mungu alipozungumzia moto na pepo kamalizia kwa kusema milele.
Aidha uwepo wa adhabu ya moto ni miongoni mwa 7b za mcng zilizopelejea kuletwa kwa mitume ili wawahofishe watu mapema kabla awajafika nbele ya mungu na kuhukumiwa.
Pia ulizungumzia adhabu zilizowapata wale waliojufuru huko nyuma na kwamba kwa mtazamo wako wale ndo washapata adhab yao hapa dunian basi. Ukweli ni jwamba aya zote zilizozungumzia adhabu za dunian kwa kaumu mbali mbali, mwisho humalixia kwa kusema na kesho akhera watapata adhabu ya milele. Kwa hiyo ni kwamba mungu anathibitisha waz kua adhabu ya moto ipo hata kwa wale ambao waliadhivuwa hapa dunian...
 
Unaweza jitahidi sana kueleza jambo, lakini kumbuka umeumbwa na huyo aliyekuumba ndiyo mwenye dhamana na akili yako na uhai wako.
Itoshe kusema yeye ni kila kitu ndani ya kila kitu
 
Kwa hiyo kutakuwa na kundi la watu waliotenda mema watakaokuwa wakiishi raha mstarehe kwenye mji wa Jerusalemu mpya itakayokuwa hapa hapa duniani na wakati huo huo kukiwa na kundi jingine la watu waliotenda uovu wakilia na kusaga meno ndani ya jehanamu ambayo nayo itakuwa sehemu fulani (pengine hapa Tanzania) hapa hapa duniani?

Kingine ambacho ningependa kueleweshwa ni hivi watenda maovu wataunguzwa na kuteketezwa mara moja na moto wa milele (yaani moto wenyewe ambao ndiyo hautakuja kuzimika milele) au ni hao watu wenyewe watakuwa wakiunguzwa milele yote pasipo kuteketea? Na kama watenda maovu watateketezwa mara moja moto utakaoendelea kuwaka milele utakuwa umebaki kwa kazi gani? Au watu wakishateketezwa na moto nao utazimika? Lakini kama na huo moto utazimika kwa nini uitwe moto wa milele? Na kama ni mwanadamu kuunguzwa na moto katika hiyo jehanamu lakini bila kuteketea na hivyo kuendelea kuteseka milele yote kwa makosa yake yanayohesabika na pia katika idadi ya miaka yake michache (inayohesabika) aliyoishi duniani naona kama vile siyo "fair" sana ukizingatia kwamba hata kuja kwake duniani hakukuwa kwa hiari yake. Daah yaani haya mambo ni magumu sana na mwenyezi Mungu tusimamie.
 
Back
Top Bottom